Matangazo kwa umma kupitia mabango na video sasa ni lazima yapate kibali cha bodi ya filamu kabla ya kuwekwa hadharani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,944
141,919
Bunge limepitisha sheria mpya ambapo kuanzia sasa mabango na matangazo yote kwa njia ya video ni lazima yapitiwe na bodi ya filamu na kupewa kibali.

Msemaji wa kambi ya upinzani Salome Makamba amepinga utaratibu huo kwa sababu utaleta urasimu usio wa lazima.
Mbunge Mtulia wa CCM ameunga mkono sheria hiyo mpya ila ameonya pasiwepo na tozo wakati wa kuomba kibali hicho.

Source ITV habari
Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi kweli tutasonga mbele kama kila kitu kitakuwa kinatengenezewa mazingira ya urasimu? Biashara za watu zitaendelea kweli, lazima turudi kwenye ujima tu.. tusitegemee kucompete na nchi nyingine kabisa. Tutadumaa mpaka tuwe viazi kabisa.

Sijajua hawa watu wanaotunga hizi sheria wanawaza nini?
 
Awamu hii imetunga sheria nyingi za tumkomeshe yule, tumbane huyo, tuwadhibiti wale,.....nk, no,..... Ilitungwa sheria inayo ruhusu mtumishi wa umma kuhamishiwa popote...imevuruga sana huko maofisini.
 
Bunge limepitisha sheria mpya ambapo kuanzia sasa mabango na matangazo yote kwa njia ya video ni lazima yapitiwe na bodi ya filamu na kupewa kibali.

Msemaji wa kambi ya upinzani Salome Makamba amepinga utaratibu huo kwa sababu utaleta urasimu usio wa lazima.
Mbunge Mtulia wa CCM ameunga mkono sheria hiyo mpya ila ameonya pasiwepo na tozo wakati wa kuomba kibali hicho.

Source ITV habari
Maendeleo hayana vyama!
tumeisha fika North Korea. yaani kama matangazo haungi mkono juhudi hayataruhusiwa kutangazwa. kwa maneno megine wapizani Tanzania nia wasahau kuonekana kwenye tv
 
Back
Top Bottom