Matamshi yaliyopotoshwa

Matamshi yaliyopotoshwa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,880
Reaction score
828,435
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe
________
Usiku wa kuamkia leo, tarehe 5/9/2025 watu “wanaojulikana” wamechoma moto gari la Mchungaji Melckisedeki Iromba wa Usharika wa Nyakasimbi, Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Gari hilo limechomwa kijijini Nyakasimbi, Kata ya Nyakasimbi, Wilaya ya Karagwe.

Uongozi wa juu wa Dayosisi ya Karagwe ukiwa katika kikao cha kujadili janga hilo, ukafikiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa na mkewe. Walipita kusalimia wakiwa njiani kuelekea kwenye kampeni zao.

Walipofika ikawa ni kama mbuzi kufia kwa muuza supu. Tukalalamika kwa kishindo kikuu juu ya kitendo cha gari la Mchungaji kuchomwa moto. Pia tukalalamika kwa kishindo chote juu ya matukio ya ubakaji kwa watoto wadogo katika eneo letu (watoto wanne wamebakwa mwaka huu) na wabakaji wameachiwa kwa dhamana.

Tukalalamika kwa Waziri juu ya watuhumiwa hao wa wabakaji kupewa dhamana na kutetewa kuwa wana haki ya kuwa uraiani. Tukasema kitendo hicho kinatishia usalama wa watoto.

Waziri akachukua hatua hapo hapo. Uongozi wa Polisi Mkoa ukafika ndani ya masaa mawili. Waziri akatusihi kuwa serikali haihusiki kuchoma moto gari la Mchungaji. Akasema isitafsrike kwamba kwa kuwa Askofu ana “mdomo mdomo” ndiyo sababu ya kuchoma gari la Mchungaji, badala ya kuchoma mdomo wa Askofu. Havihusiani.

Lakini Waandishi wa Waziri wakaacha kueleza hotuba ya Askofu kuhusu uhalifu (gari la Mchungaji kuchomwa moto na matukio ya ubakaji). Wakaacha kueleza majibu ya Waziri na hatua alizochukua. Badala yake wakaandika na kusambaza taarifa kuwa BAGONZA AOMBEA AMANI KWENYE UCHAGUZI.

Amani haiombewi. Haki ikipatikana, Amani itatiririka yenyewe na kupeana busu. TURUDI MEZANI.!
1757136938570.jpg
1757136932267.jpg
1757136928633.jpg
 
Waandishi wa waziri ni wahuni
Gari ilimechomwa moto na watu 'wanaojulikana' ina maana gani?sijaelewa
 
 
Tasnia ya uandishi wa habari imenajisiwa sana katika nchi hii, ni aibu kubwa.
Huwa naona aibu kusikiliza vyombo vya habari ambavyo ni mainstream media hapa Tanzania. Sababu huwa wanachoandika wanakijua wenyewe. Mungu wa mbinguni atusaidie
 
Kabla hamjawalaumu hawa waandishi, takeni kujua elimu zao na maslahi yao...
 
Mkuu, kamanda Baba Askofu Bagonza amewataja waliochoma moto gari? Kama "wanajulikana", kwa nini wasitajwe hadharani?
 
Asante kwa kuweka kumbuukumbi sawa ndugu askofu, maana tayari wahuni walikuwa wamekuwekea maneno yao mdomoni
 
Back
Top Bottom