Matamshi ya Makamba yanakera

MushyNoel

Senior Member
Jan 13, 2011
104
9
Wakati Chama cha mapinduzi wakizindua maadhimisho ya miaka 34 ya chama hicho kongwe kejeli dhidi ya vyama vya upinzani ndizo zilizotanda na hasa madongo kwa chadema.Hakukuwa na lingine la kutafakari zaidi ya kila alieamka kuongea kuhusu uchaguzi mkuu na chama cha chadema chenyewe.Kulikuwa na viongozi wengi kama Makamu mwenyekiti wa CCM visiwani Dr Amani Karume,Makamba,M/kili CCM mkoa wa dar es salaam Ndg Guninita pamoja na katibu wake Kilumbe Ng'enda

Makamba alisema hivi namnukuu

1) Ushindi wa Jakaya kikwete wa kura Mil 5 dhidi ya mil 2 za dr slaa sio wa kubeza
na matokeo hayo yanaonesha kwamba Dr Slaa amejeuka mpangaji ndani ya
nyumba ya kikwete.

2) Dr Slaa atambue kuwa kashindwa..akauliza hivi mpangaji (dr slaa) anaweza
kumfungia mlango mwenye nyumba(kikwete)?

3) Kikwete ndio baba mwenye nyumba na hao wapinzani ni wapangaji tu na hao wabunge wa upinzani huko majimboni chumvi na binzari wanapata kutoka CCM

Akizungumzia kuhusu kupanda kwa nishati za mafuta,umeme na gesi alisema ni kitu cha kawaida akaongeza namnukuu " hapa sio peponi Mungu kasema kwa jasho lako utakula " .Kwa tafsiri nyepesi anasema kwamba- wale wanaolalamikia upandaji wa gharama hizo hawataki kufanya kazi ili kupata nguvu (purchasing power) ya kulipia bidhaa hizo muhimu.

Huyo ndio Makamba katibu wa Chama Cha Mapinduzi na chama kinachoshika dola tanzania.
 
Maskini mzee huyu amesharukwa na akili siku nyingi lakini waliompa dhamana hawajafungua macho na masikio kulibaini hilo! Kila akiongea mapenzi ya watu kwa chama chake ndiyo yanazidi kupungua!
 
that is his nature and he cant live out of it.
dawa yake ni kumpuuzia tu maana kila mtu anajua huyu mzee propaganda
 
Huyu Mzee muacheni alivyo amalizie muda wake uliobaki muda wake ndio unaisha hivyo na kuongea na kuropoka kwake ndio kunamsaidia kupeleka mkono kinywani
 
very cheap man, siamini kwamba bado anapewa nafasi ya kuvuruga nchi hii, mpeni salamu akamfikishie Ben Ali na Mubarak he is a gone case
 
Watu 5 (apparently & allegedly) wa JK ni kitu gani mbele ya watz mil 40? watu mil 5 ndio wanakufanya uwe baba mwene nyumba? pathetic.
 
Akizungumzia kuhusu kupanda kwa nishati za mafuta,umeme na gesi alisema ni kitu cha kawaida akaongeza namnukuu " hapa sio peponi Mungu kasema kwa jasho lako utakula " .Kwa tafsiri nyepesi anasema kwamba- wale wanaolalamikia upandaji wa gharama hizo hawataki kufanya kazi ili kupata nguvu (purchasing power) ya kulipia bidhaa hizo muhimu.

Huyo ndio Makamba katibu wa Chama Cha Mapinduzi na chama kinachoshika dola tanzania.[/QUOTE]

Hapo juu aliposema kwa jasho lako utakula...alimaanisha, kwa akili yako hapa duniani (YA KUIBA / KUWA FISADI) ndio utakula / utafurahia maisha na utaishi bila kuwa na malalamiko ya vitu muhimu kupanda bei...kwako utakuwa unachekelea tena wala hata mshipa hautashtuka bei ya bidhaa hata ikiwa inapanda mara mbili kila baada ya mwezi mmoja...its high time we Tanzanians take action...!!! Bado napenda MOVE ya Tunisia na Egypt, na more the way Egpyptian police force have been supporting the citizens to continue with the protest! - Time will come for TZ!!
 
Matamshi yake ni makamba kama jina lake.huyu mzee ni tahira fresh au kwa lugha nyingine ni fresh mental a.k.a yaliyomo yamo.
 
Wakati Chama cha mapinduzi wakizindua maadhimisho ya miaka 34 ya chama hicho kongwe kejeli dhidi ya vyama vya upinzani ndizo zilizotanda na hasa madongo kwa chadema.Hakukuwa na lingine la kutafakari zaidi ya kila alieamka kuongea kuhusu uchaguzi mkuu na chama cha chadema chenyewe.Kulikuwa na viongozi wengi kama Makamu mwenyekiti wa CCM visiwani Dr Amani Karume,Makamba,M/kili CCM mkoa wa dar es salaam Ndg Guninita pamoja na katibu wake Kilumbe Ng'enda

Makamba alisema hivi namnukuu

1) Ushindi wa Jakaya kikwete wa kura Mil 5 dhidi ya mil 2 za dr slaa sio wa kubeza
na matokeo hayo yanaonesha kwamba Dr Slaa amejeuka mpangaji ndani ya
nyumba ya kikwete.

2) Dr Slaa atambue kuwa kashindwa..akauliza hivi mpangaji (dr slaa) anaweza
kumfungia mlango mwenye nyumba(kikwete)?

3) Kikwete ndio baba mwenye nyumba na hao wapinzani ni wapangaji tu na hao wabunge wa upinzani huko majimboni chumvi na binzari wanapata kutoka CCM

Akizungumzia kuhusu kupanda kwa nishati za mafuta,umeme na gesi alisema ni kitu cha kawaida akaongeza namnukuu " hapa sio peponi Mungu kasema kwa jasho lako utakula " .Kwa tafsiri nyepesi anasema kwamba- wale wanaolalamikia upandaji wa gharama hizo hawataki kufanya kazi ili kupata nguvu (purchasing power) ya kulipia bidhaa hizo muhimu.

Huyo ndio Makamba katibu wa Chama Cha Mapinduzi na chama kinachoshika dola tanzania.

Mkuu uliona umati ule wa kina mama wasio na uhakika wa ubwabwa wa kulisha familia zao Usiku?Mi sometym naona Nchi hii inamabwege!..Unavaa tishirt,kofia,khanga,kwenda kushabikia vijembe,eti kwajasho utakula!!? Maana nyingine kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake,Au hata Mafisadi ndani ya CCM akina rostam wanakula kwa urefu wa kamba zao,Acheni kubwabwaja!!..ama kweli!.
 
Haya tuone maana Mramba aliwahi kusema ndege ya raisi lazima inunuliwe hata kama Wa Tz watakula nyasi naona karibu ataisalimia segerea
 
Ukikuta mwanamke au mwanaume anataja taja jina lako ujue amekuzimia na unamkosesha usingizi... endelea kukomaa kuna siku utambenjua. Kibaya zaidi ukute anakutajataja akiwa na mpenzi au mme/mke wake hapo ujue ndoa yao imeingia shubiri.

CCM kutumia zaidi ya nusu ya muda wao kwenye mkutano wa uzinduzi wa sherehe za miaka 34 ya chama chao kuongelea Chadema na Dr Slaa siyo kitu kidogo, Dr Slaa na Chadema inawanyima usingizi wamezimika hawaoni mbele wala hawaambiwa na mtu, wameoza na wanasubiri Chadema awachukue wawe wake milele

Hongera CHADEMA na Dr SLAA kwa mabadiriko haya
 
Nilipita pale viwanja vya Biafra, nilikuwa nikipiga story na jamaa mmoja aliyekuwa amevalia T-shirt ya njano na kofia kijani alinitamkia waziwazi kwamba sehemu kubwa ya walokubali kuvaa yale manguo alilipwa Tshs10,000 akadai "nipo kibiashara zaidi, hujanivalisha haya magwanda bila malipo". Sasa najiuliza kama hayo ni ya kweli hivi kuna haja gani ya kuwalipa watu Pesa nyingi kiasi hicho? unataka nini?
 
Kwa wale wanaitakia mema CCM kipindi hiki ni kipindi cha kuelekeza mikakati ya chama kutatua matatizo yao sio kipindi cha kejeri kwani siasa za aina hii zimeanza kupitwa na wakati. hakuna jambo la hatari kisiasa na kiusalama wakati chadema wanapita huku na kule kueleza mikakati yao Makamba anatoka kivingine.

jambo la msingi tu analotakiwa kukumbuka mzee wetu makamba ni kwamba, kuna wafuasi wa vyama vya upinzani wengi tu ikiwemo chadema waliwachagua wagombea wa CCM walipoona inafaa kufanya hivyo kwa ajili ya maendeleo yao, hasa pale mgombea wa CCM alipoonekana ana sifa na vigezo zaidi ya wale wa upinzani. Ni kasumba ya zamani za kale katika zama za vyama vingi kufikiri wagombea lazima wachaguliwe na wafuasi wa chama husika.
 
Wakati Chama cha mapinduzi wakizindua maadhimisho ya miaka 34 ya chama hicho kongwe kejeli dhidi ya vyama vya upinzani ndizo zilizotanda na hasa madongo kwa chadema.Hakukuwa na lingine la kutafakari zaidi ya kila alieamka kuongea kuhusu uchaguzi mkuu na chama cha chadema chenyewe.Kulikuwa na viongozi wengi kama Makamu mwenyekiti wa CCM visiwani Dr Amani Karume,Makamba,M/kili CCM mkoa wa dar es salaam Ndg Guninita pamoja na katibu wake Kilumbe Ng'enda

Makamba alisema hivi namnukuu

1) Ushindi wa Jakaya kikwete wa kura Mil 5 dhidi ya mil 2 za dr slaa sio wa kubeza
na matokeo hayo yanaonesha kwamba Dr Slaa amejeuka mpangaji ndani ya
nyumba ya kikwete.

2) Dr Slaa atambue kuwa kashindwa..akauliza hivi mpangaji (dr slaa) anaweza
kumfungia mlango mwenye nyumba(kikwete)?

3) Kikwete ndio baba mwenye nyumba na hao wapinzani ni wapangaji tu na hao wabunge wa upinzani huko majimboni chumvi na binzari wanapata kutoka CCM

Akizungumzia kuhusu kupanda kwa nishati za mafuta,umeme na gesi alisema ni kitu cha kawaida akaongeza namnukuu " hapa sio peponi Mungu kasema kwa jasho lako utakula " .Kwa tafsiri nyepesi anasema kwamba- wale wanaolalamikia upandaji wa gharama hizo hawataki kufanya kazi ili kupata nguvu (purchasing power) ya kulipia bidhaa hizo muhimu.

Huyo ndio Makamba katibu wa Chama Cha Mapinduzi na chama kinachoshika dola tanzania.

Hivi hiki kizee ni lini kitaachana na kunukuu kutoka katika msaafu usichokihusu?????!!!! Kinasema hapa si peponi..... kwa akina nani??? Kinasema kupanda bei ya bidhaa muhimu ni kawaida... mbona hata kifo ni kawaida???? Yaani chochote kikiwa cha kawaida hata kama upumbavu tukubali tu???!!! Yaani hiki kizee nacho ni msiba mkubwa mno kwa Jamii!!!!
 
Wakati Chama cha mapinduzi wakizindua maadhimisho ya miaka 34 ya chama hicho kongwe kejeli dhidi ya vyama vya upinzani ndizo zilizotanda na hasa madongo kwa chadema.Hakukuwa na lingine la kutafakari zaidi ya kila alieamka kuongea kuhusu uchaguzi mkuu na chama cha chadema chenyewe.Kulikuwa na viongozi wengi kama Makamu mwenyekiti wa CCM visiwani Dr Amani Karume,Makamba,M/kili CCM mkoa wa dar es salaam Ndg Guninita pamoja na katibu wake Kilumbe Ng'enda

Makamba alisema hivi namnukuu

1) Ushindi wa Jakaya kikwete wa kura Mil 5 dhidi ya mil 2 za dr slaa sio wa kubeza
na matokeo hayo yanaonesha kwamba Dr Slaa amejeuka mpangaji ndani ya
nyumba ya kikwete.

2) Dr Slaa atambue kuwa kashindwa..akauliza hivi mpangaji (dr slaa) anaweza
kumfungia mlango mwenye nyumba(kikwete)?

3) Kikwete ndio baba mwenye nyumba na hao wapinzani ni wapangaji tu na hao wabunge wa upinzani huko majimboni chumvi na binzari wanapata kutoka CCM

Akizungumzia kuhusu kupanda kwa nishati za mafuta,umeme na gesi alisema ni kitu cha kawaida akaongeza namnukuu " hapa sio peponi Mungu kasema kwa jasho lako utakula " .Kwa tafsiri nyepesi anasema kwamba- wale wanaolalamikia upandaji wa gharama hizo hawataki kufanya kazi ili kupata nguvu (purchasing power) ya kulipia bidhaa hizo muhimu.

Huyo ndio Makamba katibu wa Chama Cha Mapinduzi na chama kinachoshika dola tanzania.

You are wasting your calories with this nut,why don't find something else useful to do.To him the end justies the means,no matter what.
 
Jamani ninani mwenye personal email ID ya huyu Makamba nahamu nimpandie hewani niweze kumjibu refer haya matamshi alyoyatoa kuhusu katibu mkuu wa Chadema Dr.Slaa!!:angry:
 
Back
Top Bottom