matamshi kiinglish tunayakosea kwa kurithishana

matamshi kiinglish tunayakosea kwa kurithishana

ok. jina PIUS matamshi yake ni Payas..

Sawa kabisa. Pia nakumbuka kuna mchezaji mpira wa zamani (sikumbuki timu yake) alikuwa anaitwa Titus bandawe...ni mtangazaji mmoja tu, marehemu Chilambo Dominic, ndiye aliyekuwa analitamka vyema jina lake, huku akiendana na kasi ya kabumbu uwanjani...Taitas
 
Graduation wengi husema Gra-de-she-ni badala ya Gra-dyu-e-shen.

Mimi huwa kuna neno nikisikia watu wakitamka roho hutaka kunitoka"Education"wengi hutamka edukeshen baadala ya e dyukeshen
 
Data = Deita.

nami hapo sikujua.japo kwenye dictionary yangu nimeona option tatu 1 .data =deita au da:ta kwa British Eng na ya American kwenye' a' ya kwenye' da' matamshi yake huwani muunganiko wa 'ae'.
nashukuru nimefahamu pitia kwako kwamba mtu akitamka deita akimaaanisha data anakua hajakosea
 
Nahili sahihi linatamkwaje? "schedule"
Je ni sheju au skeju?
Kuna mzungu mmoja anasema tunawacheka hawajui kutamka "ng'ombe" wanasema "ngombe" eti na wao wanasema wabongo wengi hili neno "terrible" tunachemka sana jinsi linavyotamkwa.
 
Sawa kabisa. Pia nakumbuka kuna mchezaji mpira wa zamani (sikumbuki timu yake) alikuwa anaitwa Titus bandawe...ni mtangazaji mmoja tu, marehemu Chilambo Dominic, ndiye aliyekuwa analitamka vyema jina lake, huku akiendana na kasi ya kabumbu uwanjani...Taitas

Unanikumbusha Solomon Mugera wa BBC Focus on Africa kwenye kipindi cha "Have your say" alimtaja Mnijeria "Pius" aling'aka "I'm not 'Piusi'" "I'm Paias."
 
chauffer nae ni chauferi ama ni shufer?

Cafe=kafee ama kefu?

Haya bas hii ndio ilinmaliza nikiwa denti...bureau jamaa aliambiwa asome hilo neno akadaisha bureyao! Ha ha.

Na mkumbuke huawei ni huwei..sio huwaweyi.
 
chauffer nae ni chauferi ama ni shufer?

Cafe=kafee ama kefu?

Haya bas hii ndio ilinmaliza nikiwa denti...bureau jamaa aliambiwa asome hilo neno akadaisha bureyao! Ha ha.

Na mkumbuke huawei ni huwei..sio huwaweyi.

maneno mengine yametoholewa kwenye lugha nyingine. Mfano 1: Chauffer(shofer) hii ni verb ya kifaransa which means to heat or to warm 2:
 
neno ''access'' kimakosa wanasema ases badala ya '''akses''
pia 'accept' wengine kimakosa wanasema asepti badala ya ''aksept''
neno 'important' kawaida zile herufi za mwisho(nt) wanafinya kidogo hawatamki kabisa kabisa wale wenye british accent(lafudhi) badala ya kusema importantii.
kuna makosa ya matumizi ya L kwenye R mfano neno craming wengine kimakosa wanatamka kleming na library wengine wanakosea wanatamka laiblali.
vilevile tunatabia ya kuwaona wanaotamka vizuri kiingereza kama wenye nyodo na majivuno, hili ni tatizo.
nlipokuwa shule kuna mwalimu aliuliza is it right? wakati anatamka alisema is it light. darasa hakueleweka kwa wengi walidhania ani anaulizia kama kuna umeme unawaka mchana. watu wakaanza kuangalia soketi kumbe yeye alimaanisha kama anachosema kipo sahihi
 
Ukiwa na pua nyembamba ndo unatamka namna hiyo, si pua zetu nene bana! Acheni ukoloni
 
Birthday ni neno linalokosewa sana Tanzania. Wabongo hulitamka "bathdei".

Hiyo "a" haipo kwenye matamshi sahihi. Sasa sijui watu huwa wanaitoa wapi tu!


Matamshi mabaya ya kiingereza yanazidi kuenezwa n Wakenya:

Happy wanasema "Hapi" badala ya "Hepi". Kuna kipindi cha watato nadhani ITV utakuta watoto wanaimba "Hapi Bathdei"
 
neno question - tunatamka kweshen badala ya kwes'chen
'' consumer - '' konshuma
badala ya konsyuma
'' producer - '' prodyuza badala ya prodyusa
'' assume - '' ashum
badala ya asum au asyum
'' every - '' evere " evri

hayo ni maneno machache katika mengi ambayo nimeshuhudia yakiendelea kukosewa siku hadi siku hadi na walimu wa lugha husika.Mimi nilikua mmoja wa waathirika tokana na aina ya shule nilizosoma ,japo namshukuru Mungu baada ya kufika A level nilisoma Kiingereza katika Combination yangu na kusoma topic ya phonology inayohusisha matamshi ya lugha na kanuni zake ndipo nikagundua nilipokua nakosea na wengine wengi wamekua wakikosea.

Mwenye uelewa wa maneno mengine ya english ambayo ameyasikia yakikosewa na wa Tz ni vyema ayaweke ili tuboreshe lugha kidogo kimatamshi angalau.

Kuna lile tangazo la "Star Times" yule mtangazaji anatamka vibaya "Staa Taimzi"
 
Back
Top Bottom