Matamasha bora Tanzania

Matamasha bora Tanzania

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,312
Reaction score
12,198
Umofia
Haya ni baadhi ya Matamasha nayotamani sana kuja kwenda yashuhudia Tanzania. Na hizi ni long term goals za miaka 3 ijayo nilizojiwekea lazimma nije hudhuria matamasha yake:
  1. Zanzibar International Film Festival - ZIFF.
    IMG_20180317_152101_265.jpg

    Hili kwangu ni moja ya tamasha bora kabisa Tanzania kuwepo. ambapo kwa jina lingine yanajulikana kama Tamasha la Kimataifa la filamu Zanzibar ambapo watu kutoka mataifa mbalimbali hujumuika kulihudhuria. Ni tamasha lisilo la kiserikali liloanzishwa mwaka 1997 wakilenga kusaidia kukuza filamu na utamaduni wa Mwafrika.
  2. Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar.
    2016-11-25-PHOTO-00000044.jpg

    Tamasha hili hufanyika mwezi wa 2 kila mwaka kuanzia tarehe 8-11 na huwa ni onyesho la jukwaani ingawa kwa mwaka 2016 halikufanyika kutokana na uhaba wa fedha kuliandaa. Wasanii zaidi wa 400 hufanya shoo kwenye majukwaa 3 tofauti yanayokuwa yameandaliwa. Majukwaa kama Ngome kongwe na bustani ya Forodhani hutumika zaidi. Kwa miaka 13 limekuwa likiandaliwa.
  3. Swahili Fashion Week
    SFW.jpg

    Swahili Fashion Week ilianzishwa mwaka 2008 na malengo yake yalikuwa mengi yakiwepo kukuza au kuinua brand ndogo za fashion Africa Mashariki, Kuboresha ubora na uzalishaji wa mtindo kutoka Afrika Mashariki, Kujenga fursa za bidhaa za Afrika Mashariki katika masoko ya Kimataifa. Maonyesho ya siku 3 hufanyika Mwezi wa 12, tarehe 1-3 ambapo wadau wa fashion huonyesha uwezo wao katika ubunifu wa mavazi na fasheni mbalimbali.
  4. Kigoda cha Mwalimu
    IMG_20180317_152044_810.jpg

    Kigoda cha mwalimu nyerere ni taasisi inayohusika na kujadiri mawazo/fikra za Mwalimu J.K Nyerere. Hufanyikia katika ukumbi wa Chuo kikuu Dar es salaam, hapa utakutana na watu mbalimbali toka wasomi hadi wanafunzi, wafanyabiashara hadi wanasiasa wote kwa pamoja wakijadiri mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya nchi za Afrika kwa ujumla

    4. Tamasha la Ngoma za Kisukuma - MBINA
    3-640x400.jpg

    Hili hufanyika kila tarehe 31 ya mwezi wa mei (5) kila mwaka mkoani Simiyu wilayani Bariadi. Wasukuma huamini sherehe hizi, hukutanisha watu mbali mbali ambapo watu hupata fursa ya kutambuana, kubadilishana mawazo na pia kuimarisha utamaduni wa Msukuma. Tamasha hili hujaza sana watu wakija angalia ngoma mbalimballi za kabila la wasukuma. Haya ni mashindano ambapo vikundi vya ngoma za kisukuma huonyesha uwezo wao kucheza ngoma. Makundi mawili hasimu ya Wagika na Wagalu ndio huwa na upinzani mkubwa zaidi. Washindi hupewa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha na Ng’ombe.
  5. Makumbusho ya Kabila la Wasukuma.
    2.jpg
    8.jpg

    Kijiji cha makumbusho cha kabila la Wasukuma, Bujora kilichopo maeneo ya Kisesa,ni kama umbali wa km 20 hivi kutoka Mwanza mjini na kufika kwenye kijiji hicho,ambacho kimejengwa maalum kwa ajili ya kuhifadhi vitu mbalimbali vilivyotumika na kabila la Wasukuma enzi za ukoloni.
    Kijiji hiki kilianzishwa mwaka 1954 na Padri Daud Clement Fumbuka wa kanisa katoliki jimbo la Mwanza. Padri huyo hakuwa na nia ya kuanzisha kanisa mahali hapo yeye alipenda kujua mila na desturi za kabila la Wasukuma, Wakati huo alikuwa rafiki mkubwa wa Askofu Joseph Blomjons wa jimbo kuu la Mwanza wakati huo mwaka 1965. Mwaka 1968 palirasimishwa kuwa ni makumbusho rasmi ya Bujora na hatimaye kutambuliwa na Serikali.
  6. Tamasha la Wasukuma - BULABO
    _DSC0734.JPG

    PICHA: Makamu wa Raisi Dkt Mohammed Gharib Bilal akimsalimia Mwenyekiti wa Machifu wa Kisukuma Charles Ilago Kaphipa.

    Haya yenyewe hufanyika huko kituo cha Bujoro, kijiji cha Kisesa Wilaya ya Magu ni katika sherehe za Kimila za wasukuma. Hili lenyewe hadi viongozi wa kiserikali huenda lihudhuria mfano Waziri Mkuu Mizengo pinda na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal. Kampuni mbalimbali huwa zinayadhamini mashindano haya mfano kampuni ya bia ya Serengeti, yenyewe imeyadhamini kwa miaka nane (8) sasa.
    Katika sherehe za Bulabo vikundi vya nngoma vinavyoshiriki hushindana kwa mtindo wa mtoano ambapo vikundi viwili hukaa pande mbili tofauti za uwanja vikitenganishwa na bendera nyekundu, huku majaji wakiangalia ni kundi lipi lenye umati mkubwa hivyo ni kuashiria kuwa mwenye watu wengi zaidi ndiye mwenye mvuto zaidi na hapo kutangazwa mshindi. Kigezo kingine kinachowafanya washiriki waongeze jitihada katika kucheza na kujikuta wakiwapa raha zaidi watazamaji ni kile cha kundi linaloshindwa hutakiwa kutoa elfu thelathini katika laki mbili ambazo zilikuwa zikitolewa kwa kila kundi na kumpa mshindi.


Je wewe unatamani Matamasha gani kuja hudhuria Bongo!?.
 
kweli hata mimi nakuunga mkono! Pia baadh nayatamani isipokuwa hayo ya wasukuma
 
Back
Top Bottom