MATAJIRI HUISHI KWA IMANI

chief1

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,247
2,000
Wakuu habari,
Kuna ukweli uliojificha kwa wengi nataka kuusema hapa
Kama kichwa cha somo hapo juu kinavyosema,
Kuna matabaka matatu ya watu katika hii dunia
1.matajiri 2.daraja la Kati 3.Maskini
Nadhani madaraja hayo yanaeleweka Kabisa moja kwa moja.
Daraja la matajiri lina watu wachache ukilinganisha na madaraja mawili tajwa hapo juu, madaraja haya mawili yameendelea kuwa na watu wengi zaidi na yataendelea kuwa na watu wengi kwa sababu moja tu, "IMANI" matajiri wote siyo watu wa mchezomchezo kwenye imani, wana imani za kuhamisha milima, hapa kuna imani za aina mbili, 1.Imani kwa mwenyezi Mungu 2.Imani kwa shetwani
Hakuna tajiri ambaye anamiliki utajiri mkubwa bila kuwa na imani kwa Mungu au kwa shetani, japo utajiri wa shetani huwa unaishia kubaya na tajiri anayetumia nguvu hizo za shetani hawezi kuwa na amani na pesa zake!
Sasa hawa matajiri wana imani na wanatimiza matakwa yote eg kutoa sadaka nk kwa ukamilifu

Masikini na watu wa daraja la kati /kawaida hawa huwa wanaitwa Vuguvugu yaani hawaeleweki wapowapo kila sehemu, kanisani kidogo, msikitini kidogo, kwa mganga kidogo, na mali zinakuwa kidogo, watu wa kidogokidogo!

Sasa tujitathmini tuko kundi gani, ukitaka kuwa tajiri kuwa na IMANI kwa Mungu, usiwe vuguvugu,usiwe mtu wa kidogo kidogo
 

IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,212
2,000
Ningekuwa kweli basi walokole na wavaa visuruali vifupi wangekuwa mabilionea...lakn uhalisia wa mambo hauonyeshi hivyo.

.......uliyoandika ni hoja za kujifurahisha kama zilivyo nyiiiingi mtaani.

Ni hayo tu mkuu....kwa heri
 

chief1

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,247
2,000
Ningekuwa kweli basi walokole na wavaa visuruali vifupi wangekuwa mabilionea...lakn uhalisia wa mambo hauonyeshi hivyo.

.......uliyoandika ni hoja za kujifurahisha kama zilivyo nyiiiingi mtaani.

Ni hayo tu mkuu....kwa heri
Jaribu kuwafatilia matajiri wote maisha yao utagundua kitu,
Siyo kila mlokole au suruali fupi ana imani ya kutosha
Sitaki kukulazimisha
Fatilia wewe mwenyewe
 

Mwarukuni

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
355
500
Jaribu kuwafatilia matajiri wote maisha yao utagundua kitu,
Siyo kila mlokole au suruali fupi ana imani ya kutosha
Sitaki kukulazimisha
Fatilia wewe mwenyewe
Huyo jamaa alikusudia wale walevi wa dini...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom