Matajiri hawawezi leta Mabadiliko- Polycarp Kadinal Pengo

Milindi

JF-Expert Member
Mar 3, 2009
1,467
750
Hakika ametoa mahubiri(homilia) nzito sana muda mfupi uliopita. Ndio maana hata ujio wa Yesu waliopewa habari njema walikuwa wachungaji maskini!.Kwenye siasa watu wanaaminishwa kuwa wanaoweza mabadiliko ni matajiri!


Dar na mabadiliko ya kweli
Mkoani Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alisema mabadiliko ya kweli yanaletwa na watu ambao wako tayari kufanya kazi kwa dhati usiku na mchana na si matajiri.

Akitoa mahubiri yake kwa waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph lililoko Posta jijini Dar es Salaam, katika Ibada ya usiku wa Mkesha wa Sikukuu ya Krismasi, alisema katika fikra za mabadiliko, watu wa kawaida waliaminishwa kwamba hawana mchango wanaoweza kuutoa katika mabadiliko.

?Mara nyingi sisi watu wa kawaida tulisadikishwa kwamba hakuna mchango tunaoweza kuutoa ili kuleta mabadiliko katika jumuia yetu, tulisadikishwa kwamba watu wanaokuwa na fedha na mali nyingi hao ndio wanaoweza kuleta mabadiliko katika jumuiya yetu,? alisema Pengo.

Alisema sasa mawazo hayo yamekwishatambuliwa kuwa hayakuwa sahihi, kwani watu wenye mali si wanaoweza kuleta mabadiliko yanayotakiwa katika jumuiya ya watu.

?Watakaoleta mabadiliko ni wale ambao haidhuru nafasi yao ni ipi katika jumuiya, lakini wako tayari kufanya kazi usiku na mchana, ili kuhakikisha kwamba hali ya kibinadamu inakuwa nzuri zaidi na huo ndio ujumbe unaopaswa kupokelewa kutoka kwa malaika aliowaendea wachungaji na kuwaambia msiogope,? alisema Pengo.

Askofu Pengo alisema na kupitia ujumbe huo wa malaika, Tanzania inaambiwa usiogope, kwani unayo habari njema, ambayo ni kuwa tayari kufanya kila linalokuwa ndani ya uwezo wake ili hiyo habari njema iifikie.

Aliwataka Watanzania wamuombe Mungu awajaalie neema ya kutambua kila mmoja anaweza kuwa chimbuko la habari njema na mabadiliko, si tu katika mazingira ya imani ya kidini, lakini katika mazingira hata ya kiuchumi na kisiasa.

Alisema watu hawapaswi kuogopa, bali kulinda makundi yao wakisubiri habari njema na habari hiyo si kwa ajili ya matajiri wanaoishi katika majumba ya kifahari, bali kwa ajili ya wote, habari ambayo ni ya furaha ambayo ni chimbuko la heri kwa wanadamu wote.

?Habari hii siyo kwa ajili ya matajiri, siyo kwa ajili ya wale wanaoishi katika majumba ya kifalme ni habari ya furaha ambayo itakuwa chimbuko la furaha na heri kwa wanadamu wote, Mwenyezi Mungu atujaaliye hilo katika Taifa letu,? alisema Pengo.

Source:mpekuzi.com
 
Hakika ametoa mahubiri(homilia) nzito sana muda mfupi uliopita. Ndio maana hata ujio wa Yesu waliopewa habari njema walikuwa wachungaji maskini!.Kwenye siasa watu wanaaminishwa kuwa wanaoweza mabadiliko ni matajiri!

Alichokisema ni hakika, maana mabadiliko duniani yamekuwa yakiletwa na tabaka maskini. Refer mapinduzi ya ufaransa.
 
Angenena maneno haya kwenye sakata la Escrow na maaskofu wa Mkombozi bank kumegewa fungu ningemuona ni mtu wa maana.
 
Inashangaza sana kwa haya maneno:
1.Mabadiliko ni nini?
2.kwani matajiri sio wananchi?
3.Mbona anajenga matabaka!?
4.Kama ?mtu wa Mungu antakiwa kuja na jibu na sio top layer.
NB:
Ameongozwa na Holly Ghost kuyasema haya au upeo wake?
Kama amefanya kukopi kwa Yesu kuwa Tajiri hatauona ufalme wa mbinguni,je yeye anamanisha tajiri wa mali?Na ni kweli matajiri wote wakimwomba Mungu msamaha hawasamehewi!Kwa andiko lipi?
Yesu aliaanisha Tajiri kwa mali tu au waliokumbatia ulimwengu huu na kumsahau Mungu.
Kwasababu hata viongozi wengi wetu leo hii wameukumbatia Ulimwengu na kumsahau Muumba.
Ndio maana Injili ya leo ni pesa,magari,mafanikio,biashara!?Utajiri.!!
 
Yohana mbatizaji alianza injili kwa kusema:-
1.tubuni dhambi zenu
2.yesu kristo aliianza injili kwa kusema:-
tubuni dhambi zenu!
Sasa injili ya matajiri inatoka wapi wakati watu wamejaa na dhambi na wanatafuta wa kuwaongoza ili wawezefika katika toba ya kweli na wawe huru!!?
 
Back
Top Bottom