MATAGA: Brilliant idea, poor execution

MATAGA ni nini?

Jibu fupi: Kwa uelewa wa laymen out there, ni motto (kaulimbiu) ambayo ni kifupi cha maneno "MAke TAnzania Great Again."

Hadi hapo hakuna tatizo japo jina hilo "limeibwa" kutoka katika kaulimbiu ya MAGA - Make America Great Again - ya Donald Trump.

Jibu refu: Yes, kwa wengi wenu MATAGA ni motto tu. However, kwa wanaofahamu yanayojiri nyuma ya pazia/chini ya kapeti, na kwa wenye uelewa wa "dark arts" (sanaa za kiza), MATAGA = (blend kati ya) "Watu Wasiojulikana" wa Daudi Albert Bashite + watu walioajiriwa rasmi na Kitengo kutoka private sector. Lengo la ajira kwa MATAGA lilikuwa kuchanganya intelijensia na utaalam mwingine. Kwamba, vijana wapya wa MATAGA walete kitengoni ujuzi wao katika sekta mbalimbali, hususan IT, na kitengo kiwapatie dozi ya taaluma nyeti ya intelijensia. Wazo zuri hadi hapo.

What went wrong?

Jibu fupi: virtually everything.

Jibu refu: Japo wazo lilikuwa zuri, utekelezaji ulikuwa zaidi ya mbovu. Kasoro ya kwanza ilianza kwenye wasifu wa waajiriwa. Takriban wote waliingizwa MATAGA sio on merit bali kwa kuzingatia ukabila/ukanda. Takriban MATAGA wote ni watu wa Kanda ya Ziwa.

Kasoro ya pili, uwezo dhaifu wa hao walioingizwa MATAGA. Badala ya kutafuta the smartest minds out there (katika fani zao kabla ya kuingizwa kitengo), ikafanyika "zoa zoa" tu na kupuuzia kigezo muhimu katika taaluma ya intelijensia, yaani uwezo wa hali ya juu wa AKILI (intelligence).

Kasoro ya tatu ni baada ya hao jamaa kuingia Kitengoni ambapo ikatengemezwa dharura flani kama excuse ya kutowapeleka kufanya JBC (kozi ya msingi/awali kwa maafisa wa kitengo). Matokeo yake, hadi sasa MATAGA wengi wapo wapo tu, hawajui kazi yao japo wana maslahi mazuri zaidi ya wana-kitengo wengi waliokuwepo kabla yao, na ambao walipitia "shuruba za Malindi."

Jiwe amenukuliwa mara kadhaa akieleza kutoridhishwa kwake na utendaji kazi wa MATAGA, ambao kwa sababu wengi wao wana ufahamu wa wastani kuhusu TEHAMA, wamegauza mtandaoni kuwa ndio eneo lao la kazi. Tuseme wamegeuka na-field officer wa mtandaoni. Ndio hawa wanaowasumbua hapa na huko kwingineko.

Kwa vile hawana uelewa wa A wala B ya intelijensia, wamejikita katika kuandama watu mitandaoni na kufanya propaganda za "Tanzania mpya" wakishirikiana kwa karibu na "watu wa buku saba wa Lumumba." Hata hivyo, makundi haya mawili si rafiki, kwani kila mmoja anamwona mwenzie anaingilia kazi yake.

Lakini pengine kosa kubwa zaidi, na ambalo lilichangiwa na huo "ukabila/ukanda" ni ukweli kwamba majirani zetu, hususan "Mtu Mrefu Paulo" walibaini mapema kuwa idea ya MATAGA ilikuwa fursa nzuri kwao kupenyeza watu wao. Na waliitumia vema.

So how is the situation right now?

Jibu fupi: depends on if you give a f*ck kuhusu mustakabali wa Tanzania.

Jibu refu: MATAGA is a time bomb. Ni disaster. It is a train wreck in slow motion. Na Jiwe anafahamu sana kuhusu hilo, no wonder analalamika kuwa ni wababaishaji wanaoweka mbele fedha kuliko uzalendo.

Ujio wa MATAGA umekuza kansa inayokitafuna Kitengo kwa muda mrefu: taarifa feki za kiusalama. Kwa MATAGA, taarifa feki zinawasaidia kwa namna mbili. Kwanza, uwezo wao duni wa kutafuta taarifa za kiusalama unapata ahueni. Pili, kwa vile wengi wao wanaishi kama "wazungu wa unga huko mtaani," taarifa feki zinawasaidia kupata fedha za operesheni feki na hivyo kuwa na uwezo wa "kumudu maisha yao ya ki-uzungu wa unga."

Lakini pengine kwa kuwatendea haki MATAGA, kansa kubwa zaidi inayokitafuna kitengo ni kujikita zaidi kwenye siasa na kutumika kama kitengo cha ulinzi cha CCM, na japo siasa ni moja ya maeneo lengwa ya intelijensia, key areas za UJASUSI (espionage), UZANDIKI (subversion), HUJUMA (sabotage) na UGAIDI (terrorism) zinakuwa wahanga wa hiyo politicisation of intelligence.

Sambamba na hilo ni mapungufu ya muda mrefu katika Intelligence analysis. Unaweza kuwa na best field officers lakini kama huna best intelligence analyst ni kazi bure kwa sababu mara nyingi taarifa ya kiusalama in their raw form hazina tija kwa consumption ya Sponsor (Rais) na/au policy makers kwa ujumla.

Na kuwategemea MATAGA kwenye intelligence analysis ni kama kutarajia kugema damu kwenye jiwe.

Way forward?

Jibu fupi: hardly any!

Jibu refu: moja ya sekta zilizodumaa kwa muda mrefu pasipo kujihangaisha na mabadiliko mbalimbali ni intelijensia (yetu). Wenzetu katika nchi nyingine wanahangaika kwenda na wakati ambapo tayari mataifa kadhaa yanajaribu kukumbatia teknolojia za kisasa kama artificial intelligence, machine learning, blockchain, nk

Kuna haja ya reforms kwenye sekta ya intelijensia, lakini hiyo ni ndoto hasa kwa kuzingatia symbiotic relationship kati ya Kitengo na CCM ambapo kila mmoja anamtegemea mwenzie for their survival. Mapungufu ya kitengo yanapata hifadhi katika kubebwa na CCM, na malipo yake ni Kitengo kuwa kama tawi la chama hicho tawala.

Lakini to be fair, hata kwa mataifa makubwa kiintelijensia kama Marekani, UK au Israeli, reforms kwenye sekta ya intelijensia hukumbana na kikwazo cha usiri unaotawala taaluma hiyo, japo mara nyingi kwa wenzetu usiri huo huambatana na professionalism ambayo bahati mbaya kwetu inakuwa politicised.

Ukipata wasaa soma hii kitu hapo chini ambayo kimzaha nime-wish MATAGA wangeweza kuja nayo (focusing on local stuff) kumuokoa Jiwe (he is in big trouble but that's a topic for another day)

Adobe Document CloudView attachment 1020553

Sent using Jamii Forums mobile app
Chahali bana, kwani lazima uandike unachoota?
 
Back
Top Bottom