Swali la kwanza.
Muumba alisema "adamu ukila tunda hakika utakufa", sasa suala lakujua mema na mabaya ndiyo chanzo cha kifo chake.
swali la pili.
Tuliumbwa wakamilifu ila baada ya jamaa kula tunda akatuchomesha, hivyo ukamilifu na utakatifu wetu ukapotea na umauti ukaanza kutuwinda.
Swali la tatu.
Kuhusu suala la farao kufanywa moyo mgumu, Muumba huamua kutuonesha ukuu na nguvu zake kwa namna yeyote aipendayo,
Mfano,
Aliruhusu shetani kumtesa ayubu hadi kuua watoto wake kisa wanataka kuthibitisha imani ya ayubu.
Alimkataza Musa kuingia nchi ya ahadi na WA Israel kisa alishikwa na hasira pale waisrael walipolilia maji jangwani ila Muumba zaidi ya mara moja alikasirika na kutaka kuwateketeza wanawa Israel wote pale walipokufuru, ila Musa aliwaombea msamaha, ila yeye akakosa wa kumuombea msamaha.
Kisa cha daudi kutembea na mke wa askali wake na akamuua, ila Muumba akamwambia hatompatia adhabu yeye (Daudi) ila kizazi chake na ukweli aliwaua watoto wake Daudi.
Visa ni vingi ila vyote kuonesha ukuu wake .
Asante