Maswali yangu kwa CCM

Maswali yangu kwa CCM

uttoh2002

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
19,703
Reaction score
38,005
Ni saa 10 na nusu alfajiri na nimewaza sana usiku Huu, Kwa hiyo ninatamani kuwauliza wanachama wa CCM maswali machache!

Kuna wamachama wengi sana wa CCM wenye akili, busara, Ufahamu na uwezo lakini ninaona kama wameacha uwezo wao wa kufikiri mahali!

Maswali:
- Mmekuwa na dola (serikali kwa miaka 5 ); kwa nini mnakosa cha kuonyesha jamani mlichofanya mpaka mlete fujo na kweli dhuluma za Wazi kwa vyama vingine?

- Mmekuwa na fedha za kodi zetu, Kwa nini mnazichezea kwa kiwango hiki na kweli Hakuna namna mnatusaidi, Hivi kweli wana CCM mnaamini ndege za Rais zina mchango wowote ki uchumi?

- Kwa nini mlizulumu korosho za watu na hamtaki kuwalipa? Hapa kweli nawaza mpaka basi, watu walime, wavune, muwakataze wasiuze, muwapore, then msiwalipe?

- Hivi chadema wamewakosea nini? Lissu kawafanya nini kibaya jamani? Mpaka mnawatesa namna hii, na mnajipanga kuleta fujo na kuvuruga uchaguzi? Kwa nini tusigombane kwa Hoja?

- Kwa nini Mmeua sector binafsi jamani? Je serikali inataka kufanya biashara? Hamuoni kwamba uchumi ni Imara mkifanya kazi bega kwa bega na sekta binafsi? Kwa pamoja?

- Kwa nini mliua biashara za bureau De change? Kwa nini hapa Kuwa na uwazi kabisa katika ile operations ndugu zangu wana CCM!

Sisi ni Watanzania, nyie na sisi wote na tunaisoma namba pamoja, maisha magumu sana kwetu wote, Hebu kwa moyo wa ukweli niambieni haya:

- Hivi mnajua Mungu yupo kweli? Na anawalipa watu kadri ya matendo yao?
- Hivi mnajua mkisimama na ukweli mtakuwa na aman na kuishi vyema?
- Hivi mnajua future na ustawi wa hii nchi Upo mikononi kwenu?
 
Hao CCM wenye akili hapa hawawezi kujitokeza kujibu kwakuwa wanajua kwa hakika hakuna cha kujibu, badala yake watajitokeza vijana barobaro wasio na mbele wala nyuma wanaolipwa ujira dhalili kwa ajili ya kukipamba chama mitandaoni.
 
Hao ccm wenye akili hapa hawawezi kujitokeza kujibu kwakuwa wanajua kwa hakika hakuna cha kujibu ...badala yake watajitokeza vijana barobaro wasio na mbele wala nyuma wanaolipwa ujira dhalili kwa ajili ya kukipamba chama mitandaoni...
Hivi Mshana Jr umeona ule mpango wa kumuengua Maalim kule katikati ya bahari? Unataka kuniambia wale wengine wooooooote wamejaza form zao vizuri isipokuwa Maalim tu? Nawaza kwa kinywa na kwakufikiri
 
Tusi makini kabisa...wale 16 wote hawajakosea hata nukta
Only in NEC, ZEC and CCM against CHADEMA and ACT Wazalendo. Halafu ninachojua mtu akikosea form anarekebishwa ili aendelee. Anayetakiwa kuenguliwa ni mwenye jinai na ambaye sio Raia wa Kuzaliwa wa Pande husika (Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania)
 
Ccm hawana majibu juu ya maswali yenye maslahi kwa nchi
Watakuja na SGR na ndege hata kijijini hukoo
 
Hao ccm wenye akili hapa hawawezi kujitokeza kujibu kwakuwa wanajua kwa hakika hakuna cha kujibu ...badala yake watajitokeza vijana barobaro wasio na mbele wala nyuma wanaolipwa ujira dhalili kwa ajili ya kukipamba chama mitandaoni...

Hapa naelewa!
 
Nakutukana. Hivi Mshana Jr umeona ule mpango wa kumuengua Maalim kule katikati ya bahari? Unataka kuniambia wale wengine wooooooote wamejaza form zao vizuri isipokuwa Maalim tu? Nawaza kwa kinywa na kwakufikiri
Sasa ni wakati wa vitendo uonevu huu haukubaliki na ccm ndio wa kulaumiwa kwa yatakayotokea.
 
Hakuna mtu Mwenye akili timamu hata kidogo anayeweza kuwapa kura CCM Especially nafasi ya uraisna Ubunge.

Kwa aliyoyaona miaka mitano hawezi kuthubutu.

Kuna kila aina ya ugumu wa maisha na viashiria vya udikteta vyote vikithibitika kwa macho.

Jpm anampango wa kuwa Rais wa milele.
Watanzania Tuamke
 
Masahihisho: kuwa mhadhiri wa uchumi chuo kikuu, haikufanyi kuwa na uwezo wa kupanga na kuratibu ukuaji wa uchumi. Elimu ya maprofesa wengi ni ya kutunga maswali, kusahihisha, na kukamata tu.
 
Back
Top Bottom