Maswali yanayokutatiza - 1

salimkabora

JF-Expert Member
Nov 10, 2012
2,445
1,225
SWALI: Kuna msanii mmoja maarufu sana alifariki siku za hivi karibuni na watu wakasema eti alitabiri kifo chake kwa kuwa alicheza filamu yenye matukio yanayofanana kabisa na yaliyotokea kwenye kifo chake ingawa alifariki kabla filamu yenyewe haijatoka. Je ni kweli mtu anaweza kujitabiria kifo au kujua kimbele kwamba atakufaje?


JIBU: Hakuna utabiri wowote uliojitokeza katika hilo. Unachokipanda akilini mwako ndicho kinachozaliwa kwako na ndicho utakachovuna. Ukitengeneza taswira akilini mwako ya matukio ya kijambazi na kwamba watu wanauwawa, unaumba tukio hilo nalo likidumu akilini muda wa kutosha utakabiliwa na ujambazi au wewe mwenyewe kutekeleza tukio hilo.
Msanii anapotengeneza muvi ambayo yeye mwenyewe anagombana na mpenzi wake anayemsukuma na kugongesha kichwa ukutani, kisha kuanguka sakafuni na kufikwa umauti, inamtokea kiukweli. Hiyo mbegu imepandwa na kama tahadhari hazitachukuliwa kuifuta mapema itaota mizizi na kuchipua na msanii atakufa katika mtiririko huohuo wa matukio na maiti yake kupimwa na daktari yuleyule na mwili kubebwa na gari ileile.
Ufahamu wako wa ndani ni kiwanda kinachofyatua oda zako unazozitoa kama meneja. Akili yako ni meneja na inapotoa oda kwamba ufahamu wako wa ndani ufyatue mtiririko wa umauti wako hauulizi ni umauti wa filamu au wa ukweli. Wewe ndie mkuu unayetakiwa kujua nini kinahitajika, ukiuambia zalisha vyura hauulizi vyura ni wa kazi gani wakati samaki ndio watamu, kwa nini tusizalishe samaki. Waandika vipande au script muwe makini sana na suala hili kwa maana mnakufa kirejareja sana bila kutambua mzimu wa hatari uliopo nyuma yenu kuwatafuna.
Tabia nyingi za ovyoovyo mnazoigiza katika baadhi ya vipande hugeuka na kuwa tabia zenu kiukweli katika maisha. Ufahamu wako wa ndani haujui lolote kuhusu mizaha na usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako. Kuhusu kujua kimbele kuwa mtu atakufaje ni kitu kinachowezekana. Tumesema lolote limpatalo mtu amelitengeneza mwenyewe na wala Mungu hafurahii kifo chake yeye afaye. Kutegemeana na kiasi cha ukaribu wako na Mungu, ndivyo utakavyoweza kujua yote yajayo kukupata katika maisha. Kila ulalapo picha ya matukio ya kesho yake na siku zijazo yanafunuliwa kwako kama ndoto. Kwamba kesho utaenda kazini, bosi wako atakufokea, ukitoka utapitia kwa hawara yako, n.k.
Mungu anakuonesha kile ulichofanikiwa kukiumba mwenyewe na ambacho hakina budi kukupata. Sasa kama ukaribu wako na Mungu si wa kutosha, picha hizi zinakuwa na giza, hazionekani vizuri na zinafutika, zinakuwa na chenga na ukiamka hukumbuki kitu. Tena ni afadhali ya hivyo kwa maana ulivyo mbali na Mungu, picha zitakuwa na matukio ya kutisha sana na ni bora hukuzitazama au vile haziko wazi na huzikumbuki.
Kusudio zima la kukuonesha muhtasari wa yale yatakayokupata ambayo tayari yameumbika katika ulimwengu wa roho ni kwamba uweze kuchambua na kufuta yale yasiyofaa kwa toba na maombi.-Imetolewa ktk gazeti la Imani weekly @ www.quasserer.com -email: quasserer4me@yahoo.com
 

kisukari

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
4,525
2,000
hiyo movie mimi nimeiona.haina ukweli wowote kuhusu story ya kwenye movie na kifo chake.ni vitu tofauti mno
 

salimkabora

JF-Expert Member
Nov 10, 2012
2,445
1,225
Hazungumziwi mtu specific bali it is in case huo ndio mtiririko wa fikra za anyone, na zikaunganishwa na yale yanayoongelewa kuhusu utabiri, maelezo yake ndio hayo. Script writters wametahadharishwa, pia maelezo yametolewa kwann wasanii wa filamu huwapata yanayowapata maishani: ulevi, ugomvi, kutotulia, aibu, lawama, nk
 
Top Bottom