Maswali yaliyomfanya Nape azomewe Kakola-Bulyanhulu

Determine

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
257
79
Baada ya kumaliza kuhutubia watu wasiozidi 70, Nape alisikika akisema tofauti yangu na Mzee Slaa ambaye hajawahi kuwa hata katibu kata na hawezi kuwaruhusu kuuliza maswali,kwa sababu hawezi kuyatatua,ni kwamba mimi ndio msemaji wa chama tawala na akija mwingne ni feki,mimi ni kama baba naomba niwape nafasi muulize maswali. Watu wakajitokeza.

Swali la kwanza: Mh Nape, CCM ndio chama tawala,na hakuna chama kingne tena chenye serikali, tunafahamu kwamba nchi yetu inaendeshwa na sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria,lakn cha kushangaza sisi wafanyakazi wa mgodini hapa Kakola -Bulyanhulu tumekuwa tukifukuzwa bila taratibu za kisheria kufuatwa,mfano mimi niliwahi kuuliza swali katika kikao chetu tulichofanya hapa mgodini na waziri wa madini alipokuja mgodini, swali lilihusu maslahi yetu na hivyo nilijua nitafukuzwa na mapema kabisa nilimwambia waziri kuwa baada ya swali hli najua sitakuwa na kazi,na yeye mbele ya wamiliki wa mgodi ule na wafanya kazi wenzangu alinìhakikishia kuwa sitafukuzwa,lakini leo ninapoongea hapa tayari nimekwisha fukuzwa,na nimemtumia ujumbe waziri huyo wa CCM lakn hadi leo hajanitetea,je mhe Nape huoni kuwa serikali ya CCM imewekwa mfukoni na kampuni hii ya Barrick?

MAJIBU YA NAPE: Nataka nikuoneshe kuwa nafahamu tatzo hilo, kuna watu sita mmefukuzwa na nimewagiza wabunge wenu akiwemo Maige ambaye yuko hapa wawape ushrikiano ktk kudai haki zenu. Watu wakaguna.!

SWALI LA PILI, Mh Nape kumekuwa na tabia ya watu wakawaida kufungwa kila wanapokamatwa wameiba, lakn jambo hli limekuwa halitokei kwa mawaziri wanapokamatwa kwa wizi,na matokeo yake wamekuwa wakijiuzulu na kuendelea kukaa majukwaani kama ambavyo leo uko na Maige hapo jukwaani, je huoni kuwa huu ni uonevu zidi ya wanyonge?

JIBU LA NAPE. Serikali ya kikwete tangu iingie madarakani imepangua baraza mara 3,hii ni kithibitisho kuwa hatuvumilii ufisadi, na ukweli ni kwamba kuna mawaziri wameshtakiwa, wananchi wakasikika wakisema tunataka wafungwe si kushtakiwa tu.

Halafu wakazomea, wakati m/kiti wa mkoa ccm shinyanga bwana Mgeja alipofunga mkutano ule watu wale wasiozidi 70 wakaanza kuimba peoples power.,peoples power,na kuonesha vidole viwili! Na Nape akapanda Gx lake akitanguliwa na Maige akifuatiwa na Mgeja wote wakiwa ktk magari tofauti wakati wa kuondoka.

Source mimi mwenyewe nilikuwepo.. Sema sikuwa na Camera. Nape anajua nimeandka ukweli mtupu,naweza kuapa kwa jina lolote kuwa hvyo ndvyo ilivyokuwa
 
wananchi wameshachoka kama mkutano wao ulikuwa na watu wasiozidi 70.tuwekee picha mkuu
 
Toka lini kiongozi wa CCM akawa na uwezo wa kujibu maswali papo kwa papo, Mr. Dhaifu alisepa mjadala na Makamba kuzuia wagombea wao kuhudhuria midahalo, kuogopa aibu. Akili za kukariri ndio zinamshinda hata Pinda bungeni hizi, anaishia kulia.
 
Nape alisikika akisema tofauti yangu na Mzee Slaa ambaye hajawahi kuwa hata katibu kata na hawezi kuwaruhusu kuuliza maswali,kwa sababu hawezi kuyatatua,ni kwamba mimi ndio msemaji wa chama tawala na akija mwingne ni feki,mimi ni kama baba naomba niwape nafasi muulize maswali.
Wapi Papaa zomba, Ritz, chama, Tume ya Kubaka.....ooh sorry Katiba? Jibuni sasa maswali hayo ambayo Nape kachemka!

Chezea M4C wewe?
 
Last edited by a moderator:
Kweli huo mkutano ulikuwa nyomiiii. Watu 70 ni wengi si mchezo. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeezzzzzzzzzzzz ... itikieni basi...
 
Kazi kwelikwali, hadi 2o15 tutashuhudia yasiyowahi kutokea

Hivi wewe uliyeandika uzi huu umeuchambua sawasawa? Hao watu wanaong'ang'ania na kupiga makelele mawaziri wafungwe umewaona na kuwachunguza upeo wao wa uelewa? Yaani unadiriki kusema eti wakaanza kuimba "people's power", maana yake CHADEMA ndo itakayowakomboa? Usidanganywe kabisa...... Tena tafakari kwa umakini. Fanya hivi:- Waambie watu wa Kahama kwamba ukifika wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa CHADEMA wajaze fomu kisha wagombee nafasi ngazi ya Taifa. kisha akipatikana Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Taifa CHADEMA na viongozi wa ngazi za juu kitaifa za CHADEMA kutokea KAHAMA ndipo tutaamini kuwa ukombozi umekaribia... La sivyo kuchagua CHADOMO ni HASARA bora Mkoloni arudi kututawala! Usiku mwema.
 
Kitu kingne alichosema Nape hapo kakola ambacho ni cha kijinga kwa kujua kuwa hakuna atakayeripoti ni hchi hapa: alisema hvi, jamani msiwasikilize akina Slaa hao wanasumbuliwa na njaa tu, jamani kuna mtu alikuwa mpinzani kama Maalim Self zanzibar? Lakn leo yuko wapi? Tumempa serikali ya umoja wa taifa na sasa kashba ananyoa ndevu tu. Jamani njaa ni mbaya. Mwisho wa kunukuu
 
Sikuwa na camera, nilipigiwa simu tu Nape yupo kakola nikakurupuka toka shimoni niko katika machimbo ya Nyangarata hukuhuku karibu na mgodi wa Barrick Bulyanhulu natafuta kujikwamua nchi ilishauzwa hii, lakn nilichoandka ni ukweli mtupu. HAKI YA MUNGU

Mkuu sishangai uliyoyasema, kwani tulikuwa na huyu jamaa siku ya alhamisi akielekea Mwz, ana majibu ya Dharau, Kipuuzi na haoni tabu/tatizo viongozi(wa CCM) kukosa utu, ..sincerely Nape Nnauye ana matatizo.
 
Kitu kingne alichosema Nape hapo kakola ambacho ni cha kijinga kwa kujua kuwa hakuna atakayeripoti ni hchi hapa: alisema hvi, jamani msiwasikilize akina Slaa hao wanasumbuliwa na njaa tu, jamani kuna mtu alikuwa mpinzani kama Maalim Self zanzibar? Lakn leo yuko wapi? Tumempa serikali ya umoja wa taifa na sasa kashba ananyoa ndevu tu. Jamani njaa ni mbaya. Mwisho wa kunukuu

mmmmmh......
 
Nape Nnauye ni katibu mwenyezi wa CCM, Dr Slaa ni Katibu wa CHADEMA kama Mukama alivyo kwa CCM. Sieweli ni kwa misingi ipi Nape anaona yeye na Dr Slaa wako level moja. Pia, lugha aliyotumia Nape wakati anamtaja Dr Slaa inaonekana kuna tatizo kubwa sana la kimaadili ndani ya CCM. Nape anaongea kama kibaka! Kuna tatizo gani huko Lumumba?

Pili, Katibu mwenezi wa chama cha siasa anapata wapi mamlaka ya kuagiza watendaji wa serikali na wabunge? Hii tabia inaonekana kuota mizizi lakini inadhalilisha.
 
Hivi wewe uliyeandika uzi huu umeuchambua sawasawa? Hao watu wanaong'ang'ania na kupiga makelele mawaziri wafungwe umewaona na kuwachunguza upeo wao wa uelewa? Yaani unadiriki kusema eti wakaanza kuimba "people's power", maana yake CHADEMA ndo itakayowakomboa? Usidanganywe kabisa...... Tena tafakari kwa umakini. Fanya hivi:- Waambie watu wa Kahama kwamba ukifika wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa CHADEMA wajaze fomu kisha wagombee nafasi ngazi ya Taifa. kisha akipatikana Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Taifa CHADEMA na viongozi wa ngazi za juu kitaifa za CHADEMA kutokea KAHAMA ndipo tutaamini kuwa ukombozi umekaribia... La sivyo kuchagua CHADOMO ni HASARA bora Mkoloni arudi kututawala! Usiku mwema.

Free Speech, kila mtu yupo huru kutoa shauku yake. Mimi sijatoa oni hapa ila ni mshangao kwa yanayojilia na kuhisi tu kushuhudia mengi hadi 2015. Ningetoa kuali yangu kihoja nadhani maoni yako yangukuwa sahihi, lakini kwa maoni yako uliyoweka umejibu mshangao wangu ambao haukuonyesha kuegemea upande wo wote.
 
Nape Nnauye ni katibu mwenyezi wa CCM, Dr Slaa ni Katibu wa CHADEMA kama Mukama alivyo kwa CCM. Sieweli ni kwa misingi ipi Nape anaona yeye na Dr Slaa wako level moja. Pia, lugha aliyotumia Nape wakati anamtaja Dr Slaa inaonekana kuna tatizo kubwa sana la kimaadili ndani ya CCM. Nape anaongea kama kibaka! Kuna tatizo gani huko Lumumba?

Pili, Katibu mwenezi wa chama cha siasa anapata wapi mamlaka ya kuagiza watendaji wa serikali na wabunge? Hii tabia inaonekana kuota mizizi lakini inadhalilisha.

Kama rais ni legelege na dhaifu tuatazamie nini kama si kila anayejisikia ni kujichukulia mamlaka yasiyomhusu mikononi?
 
Mkuu sishangai uliyoyasema, kwani tulikuwa na huyu jamaa siku ya alhamisi akielekea Mwz, ana majibu ya Dharau, Kipuuzi na haoni tabu/tatizo viongozi(wa CCM) kukosa utu, ..sincerely Nape Nnauye ana matatizo.

Vichwa vyao vilikaa vikachambua na kuona kuwa yeye ndo jembe na ndo mpini!
 
Hivi wewe uliyeandika uzi huu umeuchambua sawasawa? Hao watu wanaong'ang'ania na kupiga makelele mawaziri wafungwe umewaona na kuwachunguza upeo wao wa uelewa? Yaani unadiriki kusema eti wakaanza kuimba "people's power", maana yake CHADEMA ndo itakayowakomboa? Usidanganywe kabisa...... Tena tafakari kwa umakini. Fanya hivi:- Waambie watu wa Kahama kwamba ukifika wakati wa uchaguzi wa kutafuta viongozi wa CHADEMA wajaze fomu kisha wagombee nafasi ngazi ya Taifa. kisha akipatikana Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Taifa CHADEMA na viongozi wa ngazi za juu kitaifa za CHADEMA kutokea KAHAMA ndipo tutaamini kuwa ukombozi umekaribia... La sivyo kuchagua CHADOMO ni HASARA bora Mkoloni arudi kututawala! Usiku mwema.

ukiwa na upeo mzuri wa kuelewa huwezi kuishi nchi hii kwa utawala huu wa ccm utajinyonga bora tu usiwe na uelewa ndio maana unaona maprofesa wanaomba ubunge,,,,kama huamini fikiri ni kwa nini watoto form one hawajui kusoma na kuandika

Back
Top Bottom