OLESAIDIMU
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 19,139
- 9,575
Mi nilifikiri barua zinatoka posta moja hadi nyingine kwa kupitia kwenya bomba kuubwa lililochimbiwa ardhini.
Mimi sikuwahi kuwa na maswali yasiyo na jibu. Nikijiuliza swali natengeneza na jibu hapo hapo. Nilikuwa najua for sure mimba inapatikana baharini, chini ya mnazi. Mwanamke anasimama anaegemea mnazi, halafu mume anamshika tumbo anamuambia uwe na mimba ya mtoto wa kike. Afu wanarudi nyumbani (sikujua kama kuna kufanya 'matusi')
ya kwangu yalikuwa haya:
1. je mtu akifa anapandia wapi kwenda mbinguni?
2.je raisi anakunya?
Haha haaa mi nilifikiri simu ndio iko hivo yaani mnaongea kupitia bomba!!!
Mimi niliteseka na kujua kazini wanafanya kazi gani???!!!
Kama ni hesabu zoezi la ngapi??!!!!
Kama ni sayansi mada gani???!!
Madaftari wanapewa na nani???!!
Wasahishiwa kama sisi shuleni???!!!
Mbona hawavai yunifomu???!!
Yaaani nilidhani kazi ni kusoma, kuandika na kusahishiwa tu maana wanabeba mafaili na mikoba na kila nikichungulia wa mzee naona makabrasha kibao!!!!
Kumbe wewe ni wa juzi tu wakati wa kizazi cha TV. Mimi niliamini kuwa ndani ya redio wako watu ingawa wana umbile dogo lakini wana uwezo wa kuzungumza. Siku moja kuna mtu alinidanganya kuwa baba yake alifungua redio na ndani walikuwako watu wawili.
la kwangu ni kwa nini umeme haukatiki kwenye magari
..kwa nini watoto wakiume hawavalishwi teitei kengele zagongaaa..while wa kike wanavalishwa mda wote?
hahahaha umenikumbusha ule mchezo wa bomba mmoja anaweka sikioni mwingine mdomoni mnaongea kwa zamu lol
mm nilikuwa najua manesi na madaktari huwa hawaumwi.