Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,943
- 1,015
Nyerere alisema Bila CCM imara nchi itayumba. Huyu ni mwanachama CCM mwenye kadi namba 01. Alikipenda Chama chake lakini mapenzi yake kwa Chama hayakuzidi mapenzi yake kwa Wananchi wa Tanganyika na Tanzania. Katika maandishi yake anaonyesha na kuelekeza namna ambavyo Chama kinatakiwa kuweka mipango ya maendeleo ya wananchi; alitumia zaidi wakulima na wafanyakazi. Lakini si maandishi yake tu bali hata maisha yake alimaanisha hivyo. Katika kauli yake hiyo hakumaanisha kuwa nchi ya Tanzania itapotea wala baada ya myumbo huo hakutatokea Chama kingine cha Siasa chenye kuweza kuithibitisha nchi isiendelee kuyumba.
Katika hotuba yake mwaka 1995 alitaja baadhi ya nyufa zilizokuwa zimeonekana ktika uongozi wa nchi hii (yeye, Nyerere, akiwa si Mwenyekiti tena wa CCM wal si Rais tena wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Sasa hivi ikiwa ni miaka 14 na miezi kadhaa, toka kufariki kwake yapo mambo kadha tumeyaona na kushuhudia nchi inavyoyumba kiasi cha kushindwa kuweza kubashiri hatima ya nchi miaka 10 ijayo endapo itakuwa chini ya CCM (au kundi la watu wanaojiita wana-CCM).
Nina maswali yamsingi kwa wapenzi na wanachama wa CCM ya sasa:
Ukiwa na akili timamu nakuomba ujibu hoja na wala si kuleta matusi au dharau. Kama huweizi wewe pita tu.

- Kwanini unalipenda kundi la watu wanaojiita wana-CCM wa sasa?
- Tuandikie mambo matatu (3) ya kujivunia ambayo CCM imefanya kwa watanzania wa leo kwa maslahi ya watanzania.
- Tuandikie majengo 10 ya matawi ya CCM iliyojenga kwa pesa za michango ya wanachama wake (wanachama hao walifanya michango ya ununuzi wa kiwanja hadi kulisimamisha jengo hilo) tangu mfumo wa vyama vingi uanze 1992.
Ukiwa na akili timamu nakuomba ujibu hoja na wala si kuleta matusi au dharau. Kama huweizi wewe pita tu.