Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,397
- 64,623
Kila mmoja anapenda kuitwa mke/mume wa fulani,hakuna mtu anayependa azeeke mwenyewe; kwa hiyo suala la kupata mume/mke linabidi lipelekwe kiutaalamu zaidi kama mtu anavyoomba kazi. kutokana na hilo ninawaletea baadhi ya maswali ya mahojiano ya kumpata mwenza sahihi:-
- Nitajie jina lako
- Ulizaliwa lini,na wapi
- Kiwango chako cha elimu
- Unajishughulisha na nini
- Je unaamini hizo shughuli unazozifanya zinaweza kusaidia ustawi wa familia
- Je una mtazamo wa kuanzisha familia hivi karibuni
- Nieleze kwa ufupi historia ya mahusiano yako ndani ya miaka mitano mpaka leo
- Unawezaje kumtunza mume/mke
- Ikitokea mume/mke akawa hana uwezo wa kuzalisha utafanyaje
- Ikitokea kipato cha mume/mke akikidhi mahitaji utafanyaje
- Ikitokea mume/mke amepata ajali na akashindwa kuchangia pato la familia utafanyaje
- Ikitokea muonekano wangu wa leo ukaharibiwa kwa ajali au mazingira yoyote utafanyaje
- Ikitokea leo niko kitandani sijiwezi,utafanyaje
- Ikitokea nimekufumania na mtu yeyote utafanyaje
- Unapenda familia yetu iweje
- Na washauri wa familia yetu unataka wawe wakina nani