Maswali muhimu yajibiwe kwa hoja sio propaganda

Maswali muhimu yajibiwe kwa hoja sio propaganda

Isango

R I P
Joined
Jul 23, 2008
Posts
295
Reaction score
450
Swali kuu ambalo sisi tuliozaliwa ndani ya Muungano tunataka lijibiwe kwa ukweli kabisa ni ‘waasisi’ hawa wengine wa Muungano, akina Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Twala na Saleh Saadalla Akida kwa upande wa Zanzibar; na Oscar Kambona, Bhoke Munanka na Job Lusinde kwa upande wa Tanganyika walipotelea wapi na kwanini hawatajwi katika historia rasmi ya Muungano na waasisi wake? Kassim Hanga alikuwa Waziri Mkuu na baadaye Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; wakati Twala alikuwa Waziri wa Fedha wa Serikali hiyo na Saleh Saadalla alikuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. Kwa upande wa Tanganyika, Oscar Kambona alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar na baadaye wakati wa kuzaliwa kwa Muungano; Bhoke Munanka alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya usalama, na Job Lusinde alikuwa Waziri wa Serikali za Mitaa.
Katika Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!, Ghassany ameonyesha jinsi ambavyo akina
Hanga, Twala na Saadalla pamoja na viongozi wengine waandamizi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kama vile Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha Ubwa waliuawa na kuzikwa katika handaki moja katika sehemu inayoitwa Kama, nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Sisi wa kizazi cha Muungano tunataka kujua ukweli juu ya makosa waliyoyafanya hawa waasisi wa Muungano hadi wakauawa na kuzikwa katika kaburi au handaki moja. Tunataka kujua ukweli kama walifanya makosa walishtakiwa katika mahakama gani iliyowahukumu adhabu ya kifo. Aidha, tunataka kuambiwa ukweli kwanini mchango wao katika kuzaliwa kwa Muungano umefichwa kwa muda wote wa nusu karne ya Muungano huu
 
jibu ni rahisa sana na hoja yenye ujazo.

wewe nimchochezi umepewa hera chafu ili muuvunje muungano.

mnataka kutuletea machafuko .

na kama.mkiendelea kuzingua jeshi litachukua nchi.

simaneno yangu wajameni nimenukuu kwa wakubwa wakaya
 
Wanywa gongo na viroba waliotelekeza familia zao na kukimbilia kujificha dar nao siku hizi wanajiita great thinkers...for that matter najitoa jf
 
Mleta mada, nini umuhimu wa haya maelezo kwa uchumi wa taifa letu leo
 
Kuna intelligence gani katika haya maswali. Nadhani kila kitu huwa na faida kikienda na muda.. Hivi sasa ni miaka inaenda 60 tangu tuwe huru na tuwe na muungano..hao unaodai wameuwawa, hatujui ni nani aliwauwa...may be kama ungetaja muuwaji (to be specific) ili ku narrow mjadala watu waweze kujadili facts..kuishia kutaja majina ya watu na historia ya vifo vyao sidhani kama kuna umuhimu wowote kwa sasa...tundu lissu asikufunge akili yako katika chupa hadi ushindwe kuchanganya na zako
 
Jaman mleta mada anataka kujua ukwel coz kuna ki2 kimejificha katika muungano huu.
Xo nashangaa wa2 mnajibu kipropaganda zaid.
Plz let us hit da poit

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Swali kuu ambalo sisi tuliozaliwa ndani ya Muungano tunataka lijibiwe kwa ukweli kabisa ni ‘waasisi' hawa wengine wa Muungano, akina Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Twala na Saleh Saadalla Akida kwa upande wa Zanzibar; na Oscar Kambona, Bhoke Munanka na Job Lusinde kwa upande wa Tanganyika walipotelea wapi na kwanini hawatajwi katika historia rasmi ya Muungano na waasisi wake? Kassim Hanga alikuwa Waziri Mkuu na baadaye Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; wakati Twala alikuwa Waziri wa Fedha wa Serikali hiyo na Saleh Saadalla alikuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi. Kwa upande wa Tanganyika, Oscar Kambona alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar na baadaye wakati wa kuzaliwa kwa Muungano; Bhoke Munanka alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya usalama, na Job Lusinde alikuwa Waziri wa Serikali za Mitaa.
Katika Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!, Ghassany ameonyesha jinsi ambavyo akina
Hanga, Twala na Saadalla pamoja na viongozi wengine waandamizi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kama vile Othman Shariff, Mdungi Ussi na Jaha Ubwa waliuawa na kuzikwa katika handaki moja katika sehemu inayoitwa Kama, nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Sisi wa kizazi cha Muungano tunataka kujua ukweli juu ya makosa waliyoyafanya hawa waasisi wa Muungano hadi wakauawa na kuzikwa katika kaburi au handaki moja. Tunataka kujua ukweli kama walifanya makosa walishtakiwa katika mahakama gani iliyowahukumu adhabu ya kifo. Aidha, tunataka kuambiwa ukweli kwanini mchango wao katika kuzaliwa kwa Muungano umefichwa kwa muda wote wa nusu karne ya Muungano huu

MANAGING THE PAST OR COMING TO TERMS WITH THE PAST IS THE ONLY WAY OUT OF THIS QUAGMIRE.
Hiki ndicho WAJERUMANI walicho- na wameendelea kukifanya mpaka sasa, siyo kuikimbia historia!
 
Kuna intelligence gani katika haya maswali. Nadhani kila kitu huwa na faida kikienda na muda.. Hivi sasa ni miaka inaenda 60 tangu tuwe huru na tuwe na muungano..hao unaodai wameuwawa, hatujui ni nani aliwauwa...may be kama ungetaja muuwaji (to be specific) ili ku narrow mjadala watu waweze kujadili facts..kuishia kutaja majina ya watu na historia ya vifo vyao sidhani kama kuna umuhimu wowote kwa sasa...tundu lissu asikufunge akili yako katika chupa hadi ushindwe kuchanganya na zako
hujajibu bado naona una gaa gaa tu, jibu basi hata moja tu na sio ujanja ujanja
 
Mleta mada, nini umuhimu wa haya maelezo kwa uchumi wa taifa letu leo

Leo ndio unawazia umuhimu wa uchumi kwenye swali ulilo shindwa?? Mbona kwenye maswala ya uchumi nako mnakimbilia matusi? Kwani hoja bil 200 ulitoa mchango gani wenye maslahi kwa uchumi??au mdio yale yale ya kutumia kumuenzi nyerete kwa kutafuta ushindi badala ya kujibu hoja kwa data?? Ccm ni sawa na yai viza inanuka na watu wake wananuka na walemavu kiakili.
 
hapo Mh. Lisu kawashika pabaya. mtaisoma number mwaka huu.
 
CCM hawawezi kujibu maswali ya TL, labda kama unataka matusi na wananchi ndio tunazidi kupata mwanga wa Kwa nini kero za muungano haziwezi kuisha Kwa serikali mbili.
 
Kuna intelligence gani katika haya maswali. Nadhani kila kitu huwa na faida kikienda na muda.. Hivi sasa ni miaka inaenda 60 tangu tuwe huru na tuwe na muungano..hao unaodai wameuwawa, hatujui ni nani aliwauwa...may be kama ungetaja muuwaji (to be specific) ili ku narrow mjadala watu waweze kujadili facts..kuishia kutaja majina ya watu na historia ya vifo vyao sidhani kama kuna umuhimu wowote kwa sasa...tundu lissu asikufunge akili yako katika chupa hadi ushindwe kuchanganya na zako

Utaifa gani unao Kama umeshindwa kujali Damu ya hao waliouawa ?hivi kifo kinajali mda? Je?hao waliokufa wangekuwa ndugu zako ungelisema hayaa? Hakuna aliyefungwa Akili kwa Hilo Watu wamechoka kusikia Kero za Muungano hazimaliziki ! Huku Pesa ya kumaliza Kero ikitengwa na kuliwa na Wajanja kisha wanazidisha kero ili Fungu la Kero liongezeke na wao wazidi kuneemeka .huu muungano kwa sasa upo Kimagumashi kwa masilahi ya wajanja wachache tu, watu wanataka Uleee muungano Oligino wa wizara 11 tu , Pia Tanganyika irejeshwe.
 
hapo Mh. Lisu kawashika pabaya. mtaisoma number mwaka huu.

Ni kweli kawashika Penyewe huku Wananchi nao wamechoka kudanganywa sasa wanajitambua hawakariri Kama zamani ! Tiba pekee ni Tanganyika huru , kinyume na hapo Kero zitazidi Mara 1000 .
 
Utaifa gani unao Kama umeshindwa kujali Damu ya hao waliouawa ?hivi kifo kinajali mda? Je?hao waliokufa wangekuwa ndugu zako ungelisema hayaa? Hakuna aliyefungwa Akili kwa Hilo Watu wamechoka kusikia Kero za Muungano hazimaliziki ! Huku Pesa ya kumaliza Kero ikitengwa na kuliwa na Wajanja kisha wanazidisha kero ili Fungu la Kero liongezeke na wao wazidi kuneemeka .huu muungano kwa sasa upo Kimagumashi kwa masilahi ya wajanja wachache tu, watu wanataka Uleee muungano Oligino wa wizara 11 tu , Pia Tanganyika irejeshwe.

Ukitaka kufukuza LB7 team wambie wajibu hoja kama hawatabadilisha Mada eti umetukana waasisi.
 
Wanaojua hao watu ni SMZ na JMT kawaulizeni, kama hakuna jibu kafungueni kesi mahakamani kujua waliko japo binaadamu hatuishi milele,
Mtu mpaka kuhoji hivyo inamaana jibu alipewa na aliempa Data, Sasa kuuliza ni kutafuta choko choko ili kuleta vurugu nchini, watu hawaijui vurugu tunaiona kwenye TV tu, nawaambieni mnaoshabikia mtajuta na hao wanaowajaza ujinga watakimbia kwa wafadhiri wao wa uchochezi, kama mtu anataka madaraka tumia njia husika, shawishi watu kwa hoja siyo kwa uchochezi, nasikitika kuona mnatumiwa vibaya sana.
 
Back
Top Bottom