Maswali mawili ya msingi kuhusu ubunge EALA

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,534
SWALI: Uchaguzi wa wabunge wawili wa EALA kupitia CHADEMA utafanyika lini?

JIBU: unapaswa kufanyika muda wowote haraka iwezekanavyo. Hii ni kwa sababu wabunge waliochaguliwa jana (wa CCM na CUF) hawawezi kuwa halali mpaka pale wabunge wa CHADEMA watakapopatikana na kutimia 9.

Mkataba wa Afrika Mashariki (Ibara ya 50) na sheria ya uchaguzi wa wajumbe wa bunge la Afrika Mashariki ya mwaka 2011 zinapiga MARUFUKU nchi mwanachama wa EAC kupeleka wabunge wasiotimia 9 kwenye bunge la EALA. Kwa maana hiyo wabunge waliochaguliwa jana hawawezi kuapishwa, hawawezi kushiriki kikao chochote cha EALA, hawawezi hata kutambulishwa hadi wabunge wawili wa CHADEMA wachaguliwe ili watimie 9.

Kwa mantiki hiyo, uchaguzi wa wabunge wawili wa CHADEMA unapaswa kuitishwa haraka iwezekanavyo.

SWALI: Je wagombea waliokataliwa jana wanaweza kugombea tena?

JIBU: Kwanza ieleweke kuwa kuna "loophole" ya kisheria kwenye kanuni, kwa sababu tukio lililotokea jana halijawahi kutokea wakati mwingine wowote tangu kuanzishwa kwa bunge la EALA. Hata hivyo hakuna popote ambapo kanuni zinazuia mgombea aliyekataliwa awali kugombea tena. Hivyo Masha na Wenje wanaweza kuruhusiwa kugombea tena ikiwa tu CHADEMA itaongeza jina la mgombea/wagombea wengine. Unless CCM waamue kucheza na kanuni.
 
Sawa Brother umesomeka..Lakini nilisikia hawajapeleka Mgombea wa jinsi ya kike?? Ndio maana au
 
Mkuu Malisa naona kama umeruka swala la uchaguzi ndani ya Chama ili kupata majina ya wagombea yatakayopelekwa bungeni.
 
aisee sisi huku tuko bize kusigana kivyama wenzetu wanaangalia namna gani wawakilishi wao watazitendea haki nafasi zao kwa manufaa ya nchi zao!
Kweli tz kichwa cha mwendawazimu
 
Napendekeza aongezwe Kafulila ili maCCM yasijui ni yupi wa kumchagua kwani wagombea wote watakuwa na sifa zinazofanana katika ujengaji wa hoja.
 
Kanuni za bunge la Afrika mashariki zinasemaje kuhusu kesi za kupinga uchaguzi? Je watasubiri kesi ikwishe au hao saba wataendelea?
 
Namwona Salum Mwalimu, Naibu katibu mkuu Zanzibar akiongezeka..
 
Eti na wewe ulitaka kugombea ukakatwa chini kwa chini?

I guess sasa hivi huna lingine bali kujigonga ili upewe chance kwa kuandika blah blah.
 
Malsa na wengine naomba kujua. Chadema wana nafasi mbili. Kwa mfano wakijitokeza wagombea wawili tu inakuwaje?
 
Hivi kwenye kupata wabunge wa EALA kwa nini hakuna uhalali wa mtu kupita bila kupingwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom