Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,349
- 26,162
Mwishoni mwa juma lililopita, nilikutana na Wakili Msomi mmoja (jina lake nalihifadhi) katika Mahakama moja hapa jijini Dar es Salaam. Kwakuwa ni 'classmate' wangu wa Shahada ya Kwanza ya Sheria-UDSM (2009), tuliongea mengi. Nikamchokoza kuhusu kudaiwa kwake na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Nikamwita 'Mdaiwa Sugu'.
Rafiki yangu huyo Wakili Msomi akanijibu 'uchokozi' wangu kwa maswali mawili. La kwanza, kwakuwa Bodi ya Mikopo tangu mwaka 2005 (tulipokuwa mwaka wa kwanza) ilikuwa inawakopesha wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kifedha/kiuchumi, imethibitishaje kuwa kwasasa waliokopeshwa wana uwezo wa kifedha/kiuchumi ili walipe mikopo yao?
Swali la pili, kwakuwa Bodi iliwakopesha waliokuwa wanafunzi wakati huo na mkataba wa mkopo humtaka Mkopeshaji atoe notisi maalum kwa Mkopaji pale ambapo Mkopaji ameshindwa kulipa mkopo wake kwa muda unaopaswa, ni lini Bodi ya Mkopo imewapa notisi maalum Wakopaji wake kabla ya kutangaza nia ya kuwapeleka Mahakamani badala ya kutoa matangazo tu kwenye media?
Wajuzi karibu tujadiliane kuhusu maswali hayo mawili ya Wakili Msomi.