Maswali magumu kwa viongozi wa CWT

mwanakijiji lugusi

Senior Member
Apr 13, 2016
128
96
MASWALI KWA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT)
1.Mapato yatokanayo na vitega uchumi vya chama mfano: Mwalimu house na ofisi za CWT kila mkoa (rent), je vinamnufaishaje mwalimu ambaye ni mchangiaji mkuu?

2.Kwanini C.W.T wanakusanya michango kwa wanachama kila mwezi badala ya kukusanya mara moja kwa mwaka kama vyama vingine?

3.Kwanini kuna tofauti katika makato ya kuchangia mfuko wa C.W.T wakati huduma ni sawa? Kuna nini kinachoongezeka kwa anayekatwa zaidi na nini kinachopungua kwa anayekatwa chini? Tofauti hizo zinaletwa na mfumo wa asilimia zilizowekwa na hivyo kuweka wachangiaji katika matabaka yasiyo na tija wakati huduma ni sawa.

4.Je kuna uhalali gani wa kiinua mgongo cha mwanachama anayestaafu kwa uwiano na alichochangia toka uanachama wake hadi kustaafu? Ikiwa kiinua mgongo kilichopangwa na C.W.T kwa sasa ni mabati ishirini (20) tu.

5.Je C.W.T kwa mwaka inakusanya kiasi cha shilingi ngapi kwa waalimu wote Tanzania kwa makato ya asilimia mbili (2%) ya kila mshahara wa mwanachama ambayo pia inatofautiana kulingana na madaraja na fedha hizo zinatumikaje ilihali tayari kuna vitega uchumi?

6.C.W.T inawafanyakazi wangapi kwa kila mkoa na taifa kwa ujumla na posho zao zikoje?

7.Kwa kuwa waalimu wamekua wakinyanyasika na kudharaulika na kutosikilizwa katika halmashauri, Je C.W.T inafanya nini kurudisha hadhi ya mwalimu katika ngazi ya halmashauri ilihali mambo haya yanaendelea kumgandamiza na kumnyanyasa mwalimu?
 
Ninakubaliana na wewe Kwa asilimia 50 ya hoja zako hasa kuhusu tofauti iliyopo katika makato Kwa vile sasa asilimia 2 ile inaufanano na PAYE.Pili katika marekebisho ya katiba ya hivi karibuni haijatamka kiinua mgongo Kwa wastaafu Bali mkono Wa kwaheri Kwa mwanachama anayestaafu.Hata hivyo nami sioni mantiki ya mabati 20 kwani mstaafu hizobati anaishia kuziuza Kwa bei yakutupa.
 
Back
Top Bottom