wakimataifa.
JF-Expert Member
- Jun 7, 2015
- 1,625
- 554
Sasa hivi wakala wa feitoto Jasmin anazunguka kwenye vyombo vya habari kutafuta hurumaMaswali magumu kwa Feisal
By Ramadhan Elias
Mwananchi Communications Limited
Dar es Salaam. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana kupita mashauri mbalimbali yaliopelekwa mezani kwao ikiwemo lile la mchezaji Feisal Salum 'Fei Toto' akiomba kuvunja mkataba na klabu yake ya Yanga unaomalizika Mei 30, 2024.
Feisal aliaga rasmi Yanga, Desemba 24 mwaka jana, kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram siku chache baada ya koondoka kambini hapo na mechi yake ya mwisho ndani ya jezi ya Wananchi ilikuwa ya Ligi Kuu dhidi ya KMC iliyomalizika kwa Yanga kushinda 3-0, huku Feisal akifunga bao la tatu, mengine yakifungwa na Fiston Mayele.
Uongozi wa Yanga ulimshitaki Feisal kwenye kamati hiyo, ambayo ilizisikiliza pande zote mbili na kuamua Feisal kubaki Yanga, lakini kiungo huyo na wasimamizi wake wakakata rufaa ambayo pia haikutengua chochote.
Jana jioni, kamati ya Hadhi za Wachezaji iliahirisha shauri hilo hadi Mei 4, kwa ajili ya kulitolea uamuzi baada ya kukusanya vielelezo vya pande zote mbili.
Wakili anayemwakilisha Feitoto, Fatuma Karume alisema jana kuwa hakuna kilichofanyika zaidi ya kuambiwa warudi tarehe iliyopangwa.
Katika barua yake, Feitoto alisema kuna klabu inampa ushirikiano na kujali maslahi yake tofauti na Yanga ambao ni waajiri wake, ni klabu gani na imewezaje kuzungumza naye kabla ya mkataba kumalizika au kubakiza miezi sita?
Lakini kama amekiri kwa maandishi yake mwenyewe kuwa kuna klabu inampa ushirikiano na kujali maslahi yake, kamati itachukua hatua gani kwa klabu hiyo kwa vile kikanuni ndiyo ipo nyuma ya uamuzi wa Feitoto kuikacha Yanga?
Kama alikuwa haelewani na Yanga kwa muda mrefu (kama alivyoandika katika barua yake) na kupitia manyanyaso, kwanini alikubali kusaini mkataba mrefu huku akijua hana uhusiano mzuri na miamba hiyo?
Na je Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ina mamlaka ya kuvunja mkataba mchezaji kwa sababu nyingine tofauti na zile zinazoainishwa katika muongozo wa hadhi za wachezaji wa kimataifa?
Swali jingine ni kama alikuwa ananyanyaswa kwa muda mrefu, amewahi kuwasilisha malalamiko kwa kamati hiyo na vyombo vingine vya soka ambayo yanaweza kutumika kama uthibitisho wa maombi yake ya kuvunja mkataba?
Kuna mambo mengi ambayo yanahitaji majibu na huenda Feitoto angeweza kuyaangalia kuwa anajiweka hatarini kabla ya kuamua kuandika barua hiyo iliyoaminika kuwa iliandikwa Machi 6, mwaka huu.