Majibu ni yote mawili.
1. Wazee wa CCM waliostaafu wenye heshima zao, bila shaka walimsusia JK kwa sababu ya uhuni wake. Wangejiabisha kumpigia debe mtu ambaye wanafahamu fika ni FISADI na kiongozi wa mafisadi ambaye ameifilisi serikali na CCM. Wanajua kuwa wangejitokeza kumpigia debe watanzania wangewadharau na wao pia. Uhujumu wa mali za Serikali na za CCM ni mfano wa wiki iliyopita CCM kumkodishia Salma ndege ya Serikali kwa 'hela ya CCM'. Mabilioni ya pesa ya CCM yanafujwa na wanafamilia ya JK, akiwawepo Ridhiwani na Salma wanaosambaza T-shirts, kofia na khanga mikoani.
2. Ni matokeo ya n.1, JK na familia yake wakijua kuwa JK aliongoza nchi kifisadi, hataungwa mkono na watu wengi wenye akili zao, wamejichukulia majukumu ya kumrudisha Ikulu kama familia.
Kwa kuwa CCM imemsusia kumpigia debe ya kumrudisha Ikulu JK kwa sababu zilizotajwa hapo juu,
na kwakuwa baada ya kuona hali hiyo JK na familia yake wameona wafanye juu chini walau wajaribu kumtetea,
na kwa kuwa hadi sasa hatima ya JK kurudi au kutorudi Ikulu itategemea maamuzi ya watanzania wenye busura na akili, na ambao watatoa hukumu ya haki kwa kila mgombea kulingana matendo yake,
na kwakuwa kuna uwezekano mkubwa wa JK kutoona Ikulu baada ya 31.10,
SWALI
Je, a) kama asiposhinda ataendelea kuwa m/kiti wa CCM, ilhali CCM ishamwona hafai na ikamsusia?
b) ikitokea, kwa sababu kudanganywa na tshirts, kofia, khanga, sh 2000, 1000, nk, wengi wakampa nafasi ya kurudi Ikulu, hata kama atapata 50.1%, atawatumikia wanaCCM? watanzania? au familia yake ilifanya juu chini kusambaza t-shirts, kofia, khanga nchi nzima ili kuhakikisha anarudi ikulu?