Maswali Magumu: Kikwete wa mtandao kageukia familia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali Magumu: Kikwete wa mtandao kageukia familia?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bramo, Jun 27, 2010.

 1. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #1
  Jun 27, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  By Ansebert Ngurumo

  SWALI kuu la wiki hii ni hili: Kwa nini Rais Jakaya Kikwete ameogopa kuwatumia wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), badala yake akawatumia wanafamilia kutafuta wadhamini ili aidhinishwe kugombea tena urais mwaka huu? Tafsiri zimekuwa nyingi. Lakini kubwa kuliko zote ni kwamba Rais Kikwete hana imani na wanachama wenzake. Anawaogopa, nao wanamtilia shaka. Anaona ni vema kutumia wanafamilia – mkewe na mwanaye – katika harakati za kurejea Ikulu.

  Maana yake nini? Miaka mitano Ikulu haikuwa neema kwake na chama chake. Uhusiano wake na wapambe wake wa msingi umedorora. Chama kimejaa makundi yasiyoaminiana, yanayofitiniana.

  Kwa hiyo, wakati anajitapa kuwa amedumisha umoja na mshikamano, na kusema kwamba hili ni moja ya mafanikio yake yanayomfanya agombee tena urais; kitendo cha kuwakwepa wana CCM wenzake na kuwatumia wanafamilia kinaonyesha kwamba wana CCM hawana umoja wala mshikamano unaotosha kumwezesha yeye kupata wadhamini wanaoaminika.

  Baada ya siasa za wapambe na mtandao, sasa tumerudi kwenye siasa za baba, mama, mtoto na ‘mama mkwe.’

  Ukweli unabaki kuwa kwamba upepo wa kisiasa katika wiki mbili zilizopita unaonyesha kwamba JK wa mwaka 2005 si huyu wa mwaka 2010.

  Wana CCM wamesema –pembeni na hadharani. Wapambe wamejadili, na vyombo vya habari vimeandika. Utetezi na ufafanuzi wa chama na Ikulu vimetolewa. Lakini tunapotazama na kutafakari, tunaona kwamba hata zile shamrashamra za mwaka 2005 hazipo tena.

  Hazikuwapo siku alipotangaza kuchukua fomu. Kule kujiamini alikokuwa nako mwaka 2005 – aliposisitiza kwamba hafikirii kushindwa – hakupo tena.

  Sasa kuna hofu kwamba JK anaweza kushindwa; na kama atashinda itakuwa kwa asilimia ndogo.
  Nakumbuka baadhi ya mashushushu wake waliowahi kunisihi nipunguze makali, walikiri kwamba iwapo wananchi wataelimika na kuhamasika vya kutosha, rais anaweza kushinda kwa kura chache tu, jambo ambalo linaweza kuleta mzozo, kwani wananchi wanaweza kukataa matokeo ya kura; wakaandamana na kuleta zogo na kuifanya nchi isitawalike.

  Na wakasisitiza kwamba iwapo hilo litatokea, mimi nitakuwa nimechangia kuleta vurugu nchini – jambo ambalo niliwaomba walitafakari kwa kina.

  Ukweli huo umesemekana kuwa ulimfanya naye afikirie mara mbili, kama achukue fomu au aachie ngazi – hadi alipohakikishiwa na kushawishiwa na watu wake kwamba hawatampinga.

  Alijua, na alihofia, kwamba iwapo angejitokeza mgombea mwingine ndani ya chama, lolote lingeweza kutokea; kwani kuna wajumbe wa vyombo vikuu vya uamuzi ndani ya CCM ambao wana nguvu kubwa sana kuliko ya mwenyekiti wao.

  Alijua pia kwamba hata wanachama wa kawaida, kama wangepata mbadala, na kushawishiwa vilivyo, wangeweza kuandika historia kama ya chama cha ANC cha Afrika Kusini, ambacho kilimtosa rais aliyekuwa madarakani (Thabo Mbeki) kikamchagua Jacob Zuma.

  Hofu hii ndiyo ilimfanya asiruhusu maswali ya wananchi na waandishi wa habari, alipochukua fomu Dodoma, Jumatatu wiki hii. Alijua kuna maswali mengi yasiyojibika.

  Na hofu hii ndiyo inawafanya baadhi ya watu wake kusema kwa kujiamini kwamba hata kama utaitishwa mdahalo wa kisiasa kwa wagombea urais mwaka huu, JK hatashiriki. Anaogopa maswali.

  Kama mwaka 2005 aliogopa kushiriki akiwa mpya na mweupe, atawezaje kukubali akiwa ameshachafuka kwa matope ya miaka mitano ya utendaji usioridhisha?

  Vyovyote itakavyokuwa, na ingawa hadi sasa JK anaonekana mgombea pekee wa urais kutoka CCM, yeye hana amani kwamba hatapingwa. Inawezekana naye anajua moyoni, ingawa mdomoni anasema atashinda, kwamba anaweza kupita kwa nguvu ya dola au kwa ushindi wa asilimia ndogo sana isiyokubalika kwa wananchi.

  Na yeye binafsi angependa kujua kama hadi mwisho wa mwezi huu hatajitokeza mtu mwingine (asiyeogopa utabiri wa Sheikh Yahya Hussein) wa kumpinga; na kama vyama vya upinzani havitaweza kumpata mgombea anayekubalika anayeweza kuleta tumaini la Watanzania kuondokana na ombwe la uongozi.

  Hakika, miaka mingine mitano chini ya ombwe ni laana isiyokubalika kwa taifa la watu wanaozidi milioni 40. Na ndiyo maana nimekuwa nawauliza wana CCM wanaoogopa kugombea na JK: Hivi Tanzania imeishiwa na watu wema, wenye uwezo na upeo, wanaoweza kuwa viongozi bora?

  Tungepata waandishi kumi kama Ngurumo,walah Wa Tanzania woote wangeamka kutoka usingizini.
   
 2. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ngurumo ni miongoni mwa waandishi wachache wenye uwezo wa kuelezea hoja kwa lugha rahisi inayoeleweka.

  JK ana hofu kubwa sana kwani anakumbuka kauli za kina Mateo Qares, Joseph Butiku na Warioba kuwa nchi haina kiongozi kwani JK hajachua hatua madhubuti ya kushughulikia matatizo ya wananchi. Hastahili kuwa rais hata kidogo. Angeachia ngazi amwachie Mwanaccm au mgombe mwingine toka kambi ya ya upinzani.

  Huku mtaani ni kwamba JK hakubaliki ila kuna wanaccm wanaoandaa mazingira ya JK kushinda kiurahisi mfano Vitisho, rushwa na kutumia watumishi wa umma kufanikisha udanganyifu.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nani anayetaka kufa?...Hujasikia safari hii kwamba mambo yote ya uchaguzi ya huyu mtu yanasimamiwa na nguvu za ugagura?
   
 4. k

  kiuno Member

  #4
  Jun 27, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mna ugagura,kama kungekuwa na ugagura wangefanya south africa au nigeria washinde kombe la dunia,ni imani tu tu za kijinga, na hii imani ilivyotuingia wabongo hakika tungekuwa tunaamini mambo ya msingi zaidi ya ugagura tungefika mbali na ccm isingeongoza miaka 5 ijayo
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  usiwe na mtazamo mfupi na upembuzi dhaifu, ugagura upo, Mungu mwenyewe anajua na amewaasa watu wake kuwa watiifu kwake na kuhahakisha wanaupiga vita, na kuushinda ikiwa tu utamwamini yeye (Mungu), haya mambo ya ugagura yapo na ni ya watu kwa ajili ya watu, huko unakosema uanajua vipi wanavyofaidika na ugagura? kwa kuwa kwanza hauna takwimu za kidunia, this is local issues how can you obtaine its usefull and unusefull and it gols to the society?
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mh.. i see you have gone for the jugular kabisa

  kweli PJ umeamua mwaka huu
   
 7. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ngurumo ni mwandishi makini na mwenye upeo binafsi..nampongezaa kwa makala zake imara zenye ujumbe makini.

  ni kweli JK hajiamini na wenzake ndani ya CCM hawamkubalii wala kumwaminii..amewagawanya kulikoo kipindii chochote cha historia ya chama chao. amemtumia shekh yahya kuwatisha na huenda amefanikiwaa kiasii..

  miaka 50 baada ya uhuru wa kisiasa bado watanzania hatujiaminii kuletaa mabadilikoo..nilistaajabuu kama wale wanchama imara ndani ya ccm wamenyweaa kirahisii kumwachiaa tena JK ngwee hii.. adhabu yao inakuja..atawatapanyaa zaidii na kuwararuaa zaidii ya kuwagawaaa..
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ngurumo ametumia muda karibu wote tangu 2005 kuangalia MAPUNGUFU tu ya JK. Sidhani kama huo ni uandishi uliotukuka. Bahati nzuri hajawahi kusema yeye alimwona nani angefaa zaidi ya JK.
   
 9. J

  Jafar JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mungu ibariki Tanganyika

  Sasa ana mambo mawili
  1. yeye mwenyewe kujihakikishia ndani ya CCM
  2. kumpata raisi wa Zanzibar kupitia mikononi mwake, akilegea na kuchekacheka Zanzibar moto utawaka ndani ya CCM.
   
 10. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #10
  Jun 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Sala zangu ni kuwa hilo litokee,..tuombe Mungu hilo litokee
   
 11. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Mkuu, Tupe mazuri matatu tu ya JK ambayo Ngurumo hayaoni na angeweza kuyaandika. Matatu tu!
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kuteua sura mpya za mawaziri badala ya zile zilizozoeleka tokea enzi za Nyerere
   
 13. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kusogeza elimu ya Sekondari hadi ngazi ya kata tofauti na zamani ambayo shule zilikuwa kwa ngazi ya Kanda mf. Singida, Arusha, Moshi, Tanga - kupokezana kuingi Mawenzi Secondary.
   
 14. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Uhuru wa habari-enzi za nyerere kwa sentensi yako ungekuwa Lupango
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri JK ametumia wana CCM kusaka wadhamini kwa sababu mkewe ni CCM, Ridhiwan ni CCM labda tuseme ametumia wana CCM ambao ni ndugu zake wa karibu ingawaje sidhani kama mke ni ndugu wa mme au kinyume chake! Kimaadili hakutakiwa kufanya hivyo. Je, kwenye uchaguzi huu hata mawakala wa CCM watakuwa watu wa ukoo wake ambao ni wana CCM? Hivi mgombea akikataliwa na chama chake wanatafute mwingine kwenye kikao hicho hicho? Tume inasemaje kuhusu hili?
   
 16. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Alichofanya ni sahihi kabisa kwani Uraisi hauna ubia. Kutumia watu wengine kumsaidia aingie ikuli baada hao watu watahitaji fadhila kwa maana ya vyeo aidha serikali au kwenye chama. Kutuma jamaa zake ni sawa tu kama ameenda peke yake. Pili, kama gharama za kusaka wadhamini ni zake kwa nini atapanye kile alichonacho wakati na wanafamilia wa kufanya hiyo kazi?
   
 17. m

  mozze Senior Member

  #17
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kweli tuko tayari kuongozwa na Mtu anayesema Uraisi ni Suala la Kifamili?
  Nomba majibu hasa kutoka kwa wana CCM na mashabiki wa Kikwete Pale wanafamilia wanapofanya mambo bila ya idhini ya vikao vya chama, wanapoingilia shughuli za serekali tutapata matunda gani?
  CHadema hii ni Agenda nzuri sana, waelezeni watanzania jinsi hii familia inavyoingia kwa kasi kwenye kuendesha nchi! Tunapoenda kunaweza kutokea machafuko kuanzia ndani ya CCM, mana nina uhakika wengi wananung'unika tu na kuwa WANAFIKI kwa kufikiria Kikwete ni mzuri kwao. 2005 alikuwa karibu na Mafisadi, huu ni muhula wake wa mwisho anataka kuwa karibu na Familia yake...huyu mpindisha Sheria anaweza kubadili katiba ili aweze kurithisha URAIS kwa familia yake!!!
  Hafai kabisa kuogoza nchi!!
  Inauma sana mkuu wa mkoa anapoamriwa kumfuata mtoto wa raisi, au mtoto/mke wa raisi kudai report kutoka kwa mkuu wa mkoa au kiongozi wa serekali!
  Wana CCM msione aibu kumkataa Kikwete. Mkimkataa itakuwa ni kwa manufaa yenu, familia zenu na taifa kwa Ujumla!
   
 18. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,460
  Likes Received: 1,334
  Trophy Points: 280
  Katiba yetu inamapungufu mengi na hili la madaraka ya rais ni tatito kubwa, nchi inaendeshwa kifalme sasa
   
 19. e

  emalau JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nchi haina protokali za kueleweka, hata huyu salama eti naye anapokewa na mkuu wa mkoa ! Maajabu ya musa !
   
 20. V

  Vaticano Member

  #20
  Sep 18, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli hakuna protokali. Mgombea anamsimamisha mke wa mtu na kumnadi mchumba wake!
   
Loading...