Elections 2010 Maswali Magumu: Kikwete wa mtandao kageukia familia?

Labda nianze kwa kurejea makala iliyoandikwa na rafiki wa jk (si swahiba )katika gazeti la raia mwema la wiki hii inayosema JK NI MSAHAULIFU AU MZEMBE.
Nimevutwa sana na hoja za huyu jamaa mpaka nimejiuliza maswali mengi sana, hasa kitendo cha familia kuingia kwenye kampeni za chama moja kwa moja.
WAKUU ,INAWEZEKANA KUNA WATU WANAJUA MAJIBU YA HAYA NINAYOJIULIZA,NAOMBA MSAADA WENU.
MASWALI NINAYOJIULIZA NI HAYA:-
1. NI KWA NINI SISIKII WANACHAMA AU VIONGOZI WASTAAFU,AU MAARUFU WA CCM WAKIPANDA MAJUKWAA KUMPIGIA DEBE JK, NAAMINI WAO NDIO WANAZIELEWA VEMA SERA ZA CCM KULIKO FAMILIA. WASIWASI WANGU KASUSWA
2.WANAFAMILIA WANAPIGA KAMPENI ILI IWEJE,HAIWATOSHI JK KUWA BABA WA FAMILIA AU WANAZIELEWA SANA SERA ZA CCM KULIKO VIONGOZI NA WANACHAMA.
3.KUTOKANA NA HAYO HAPO JUU NASHINDWA KUELEWA JK NI MGOMBEA WA CHAMA,FAMILIA AU BINAFSI
4.
5.
NAJUA KUNA MENGI WENGI TUNAJIULIZA LIKIWEPO NA UBABE WA FAMILIA KUKITEKA CHAMA NA MENGINEYO.
WAKUU KAMA KUNA MTU ANA MASWALI AU MAJIBU NAOMBA MICHANGO YENU.
 
Majibu ni yote mawili.
1. Wazee wa CCM waliostaafu wenye heshima zao, bila shaka walimsusia JK kwa sababu ya uhuni wake. Wangejiabisha kumpigia debe mtu ambaye wanafahamu fika ni FISADI na kiongozi wa mafisadi ambaye ameifilisi serikali na CCM. Wanajua kuwa wangejitokeza kumpigia debe watanzania wangewadharau na wao pia. Uhujumu wa mali za Serikali na za CCM ni mfano wa wiki iliyopita CCM kumkodishia Salma ndege ya Serikali kwa 'hela ya CCM'. Mabilioni ya pesa ya CCM yanafujwa na wanafamilia ya JK, akiwawepo Ridhiwani na Salma wanaosambaza T-shirts, kofia na khanga mikoani.

2. Ni matokeo ya n.1, JK na familia yake wakijua kuwa JK aliongoza nchi kifisadi, hataungwa mkono na watu wengi wenye akili zao, wamejichukulia majukumu ya kumrudisha Ikulu kama familia.

Kwa kuwa CCM imemsusia kumpigia debe ya kumrudisha Ikulu JK kwa sababu zilizotajwa hapo juu,
na kwakuwa baada ya kuona hali hiyo JK na familia yake wameona wafanye juu chini walau wajaribu kumtetea,
na kwa kuwa hadi sasa hatima ya JK kurudi au kutorudi Ikulu itategemea maamuzi ya watanzania wenye busura na akili, na ambao watatoa hukumu ya haki kwa kila mgombea kulingana matendo yake,
na kwakuwa kuna uwezekano mkubwa wa JK kutoona Ikulu baada ya 31.10,


SWALI
Je, a) kama asiposhinda ataendelea kuwa m/kiti wa CCM, ilhali CCM ishamwona hafai na ikamsusia?
b) ikitokea, kwa sababu kudanganywa na tshirts, kofia, khanga, sh 2000, 1000, nk, wengi wakampa nafasi ya kurudi Ikulu, hata kama atapata 50.1%, atawatumikia wanaCCM? watanzania? au familia yake ilifanya juu chini kusambaza t-shirts, kofia, khanga nchi nzima ili kuhakikisha anarudi ikulu?
 
Wait a minute... these guys have joined the forces in squandering the National wealth!
Yaani ni kwamba baba ameona akichuma peke yake hazitatosha, mama nae aende akachote, na mtoto pia!~..ili baada ya kumaliza muda wao wawe na himaya yenye nguvu ya Pesa!
 
...Mkuu, Tupe mazuri matatu tu ya JK ambayo Ngurumo hayaoni na angeweza kuyaandika. Matatu tu!

Amejitahidi sana kuthamini nafasi ya mwanamke na vijana katika jamii....tumeona vijana wengi na wanawake wengi wakishika nafasi kubwa za madaraka nchini.
 
Mimi nafikiri JK ametumia wana CCM kusaka wadhamini kwa sababu mkewe ni CCM, Ridhiwan ni CCM labda tuseme ametumia wana CCM ambao ni ndugu zake wa karibu ingawaje sidhani kama mke ni ndugu wa mme au kinyume chake! Kimaadili hakutakiwa kufanya hivyo. Je, kwenye uchaguzi huu hata mawakala wa CCM watakuwa watu wa ukoo wake ambao ni wana CCM? Hivi mgombea akikataliwa na chama chake wanatafute mwingine kwenye kikao hicho hicho? Tume inasemaje kuhusu hili?
Nasikitika kwamba ulikuwa hujui unapost nini hapo juu. ila nadhani umejionea hali halisi baada ya kubinafsisha urais kwa wanafamilia.
Zidumu fikra za Nyerere. Rais hashauriwi na mkewe
 
Wewe kweli akili topetope, sisi hapa tunaongelea vitu vya msingi vya taifa wewe unaingiza upumbavu. wewe ni
mshenzi

punguzeni matusi basi!mshenzi maana yake nani?kuna ushenzi duniani kuliko yule anayechukua wake za watu kimabavu?na kumkana mkewe hadharani?ni aibu kwa mwanamme mwenye miaka zaidi ya 55 kusema eti na mchumba...huo ndio ushenzi!
 
Amejitahidi sana kuthamini nafasi ya mwanamke na vijana katika jamii....tumeona vijana wengi na wanawake wengi wakishika nafasi kubwa za madaraka nchini.
...hao wanawake wengi walipateje hayo madaraka? je walipaswa kuyapata kabla ya kupitia kwenye chujio au kwa kuwa madaraka hayo yalipaswa kupewa wanawake hivyo kila unayekutana naye unampa post? hebu nijuze zaidi
 
punguzeni matusi basi!mshenzi maana yake nani?kuna ushenzi duniani kuliko yule anayechukua wake za watu kimabavu?na kumkana mkewe hadharani?ni aibu kwa mwanamme mwenye miaka zaidi ya 55 kusema eti na mchumba...huo ndio ushenzi!

Hizo ndiyo zao hizo. Wanazungumzia protokali lakini zile za kuwatambulisha wake za watu kama wachumba zao hawaoni kama ni ushenzi.
 
Mtandao wamekaa pembeni kwa sasa, lakini kadri mambo yanavyozidi kuwa magumu kwa Kikwete tusishangae wakacheza rafu kali za chini chini katika mikoa ambayo Kikwete kabanwa mbavu na kuanza kutoa rushwa za hali ya juu.
 
Kwa heri sisiem kwa heri Iselamagazi. S iwezi tena kumkubali j.k katika maisha yangu yote, hebu mwambieni ukweli kwamba nchi imemshinda. Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamamu anayempigia kampeni kikwete. Wanaompigia kampeni ni wale wanaotegemea hisani ya kupewa vyeo. Kwa bahati mbaya wamechgua siko, kikwete hachaguliki acheni unafiki
 
punguzeni matusi basi!mshenzi maana yake nani?kuna ushenzi duniani kuliko yule anayechukua wake za watu kimabavu?na kumkana mkewe hadharani?ni aibu kwa mwanamme mwenye miaka zaidi ya 55 kusema eti na mchumba...huo ndio ushenzi!

Kuna ushenzi zaidi ya kugawa raslimali za nchi kwa mashemeji wageni, na kugawa vyeo hovyo kwa nyumba ndogo lukuki?, kutumia pesa za walipa kodi kutalii na dogodogo kila kona ya dunia bila haya wala soni? mkuu.. bora uishie hapo usirudishe hii ajenda ya siri za ndani, kwani hakika chamacha mafisadi ki ndani ya nyumba ya kioo!
 
Kwa heri sisiem kwa heri Iselamagazi. S iwezi tena kumkubali j.k katika maisha yangu yote, hebu mwambieni ukweli kwamba nchi imemshinda. Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamamu anayempigia kampeni kikwete. Wanaompigia kampeni ni wale wanaotegemea hisani ya kupewa vyeo. Kwa bahati mbaya wamechgua siko, kikwete hachaguliki acheni unafiki

mke wa mtu!? CCM oleeeeeeeee
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom