Maswali kwako Samwel Sitta na naibu wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali kwako Samwel Sitta na naibu wako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msanii, Dec 20, 2009.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mnapopitisha BAJETI ya serikali, bunge linakaa kama kamati ya matumizi ili kupitia kipengele kwa kipengele makadirio ya bajeti kwa wizara husika. Pamoja na kuvipitia vipengele kila mwaka mnapata maelezo ya ufafanuzi wa baadhi ya vipengele tata kutoka kwa mtoa hoja, na baada ya kupitisha hizo bajeti za wizara kunakuwa na after party kwa wizara husika. Maswali yangu yanakuja kwa mtindo wa hoja kama ifuatavyo:-


  • Mmekuwa mnatumia muda mwingi kuchangia hoja hotuba za bajeti ijayo lakini hamjatenga muda wa kutosha kupitia utekelezaji wa vipengele mlivyopitisha bajeti iliyopita. Mnapowaidhinishia watendaji bajeti mnakuwa mmetumaliza maini yetu kwani baada ya bunge la bajeti mwendo huwa ni mdundo I mean matumizi kwa kwenda mbele. Mmekuwa mnapata na kupokea ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali kuhusu matumizi ya serikali ktk bajeti iliyopita. Sehemu kubwa ya ripoti ni mapungufu katika kuyutilaizi fedha za bajeti. Barabara zinajengwa chini ya kiwango kwenu si shida kwani mtasema mlitaka lami na tumewatandikia mpaka milangoni. Kwenu suala la viwango na durability ni kupoteza wakati. Sijasikia mtendaji wa serikali (WAZIRI) akiwajibika au kuwajibishwa au hata kuwekwa kilingeni kujibu hoja zitokanazo na uzembe au ubadhirifu wa kasma ya bajeti iliyopita. Mbona kuna miradi inatengewa fedha halafu haitekelezwi kisha next bunge la bajeti mnatenga tena fedha bila ya wahusika kurejesha hazina fedha iliyobakia? Hivi zile sherehe za jioni za kila wizara inapofaulu kupitisha bajeti yake inatoa ujumbe gani kwetu? Nina shaka kwamba wanaleta bajeti BOMU ambayo wanajua haitapita hivyo ikipita ni lazma wajipongeze. Mbona hizo fedha za kupongezana hazipo ktk bajeti au wanatumia mshahara wa waziri? Au ndo ile kasma ya viburudisho na chai?
  • Kwa nini huduma za jamii kama afya, elimu, miundombinu, maji na umeme viombwe kutoka serikali kuu?? Ina maana jukumu la serikali ni kutawala tu? Utasikia mbunge anasema ‘mheshimiwa waziri naomba uwaangalie watu wa jimbo langu katika hili na lile…’ je Maendeleo ni hisani au wajibu? Nashindwa kukuelewa WEWE na bunge lako kwamba mnashindwa kukaa na serikali kama partners wa maendeleo zaidi mnakuwa beggars sana kwa watu wanaowajibika kikatiba kutekeleza masuala muhimu kwa ustawi wa taifa. Je ni jukumu letu sisi wananchi kujiletea maendeleo ilhali tunalipa kodi zetu kwa serikali ambayo inapaswa kuweka mazingira bora ya kuprosper?
  • Bunge lako linamissuse funds zetu kwa kutumia muda mwingi kusifia na kupongezana badala ya kupresent issues za maana kwa ustawi wa watu. Waeleze wabunge wako kwamba kama kweli wana nia ya dhati kutoa shukrani kwa wananchi waliowapigia kura wafanye hivyo majimboni mwao kwa kuwatembelea na kukaa nao wakitatua kwa pamoja masuala yanayowakinza. Na njia nzuri ya kuwashukuru wananchi ni kuwasababishia maisha bora na si maneno matupu kwenye vipaza sauti vya bunge letu tukufu. Pia uwaelekeze au uweke katika kanuni kwamba kama mbunge anaunga mkono hoja basi asiseme “naunga mkono mia kwa mia”. Mnatuchanganya sana kwa mwenendo wenu wa BUNGE kukaa kishabiki zaidi ya kiufanisi.
  • Kuna usemi kwamba wabunge wanawajibika kwa vyama vyao vya siasa wawapo bungeni. Je huoni huo ni wizi wa fedha zetu? Mimi ambaye ni CCM halafu mbunge wangu ni CHADEMA je maslahi yangu kama raia yatakuwa at stake kwa kuwa si mwanachama wa chama cha mbunge wangu? WABUNGE mlipigiwa kura na SISI – WATU, kama mnawajibika kwa vyama vyenu vya siasa basi badilisheni katiba wekeni kipengele kwamba mbunge anaapishwa baada ya kushinda kura ya maoni ya chama chake mpigiane kura ninyi kwa ninyi halafu futeni uchaguzi wa wabunge ili tutekeleze kaulimbiu yenu ya kuwajibika kwa chama.
  • Katika kanuni za bunge (sijui kipengele) mmeanisha wazi kwamba mbunge anapoleta taarifa, au hoja ambayo itathibitika si ya kweli bungeni amewekewa penal ambayo ataitumikia baada ya kamati ya uongozi kutathmini athari za upotoshaji ule. Lakini bunge lako limeshaletewa mara nyingi tu taarifa za uongo na upotoshaji kutoka kwa MAWAZIRI (wabunge wenye wasaidizi kibao) lakini hata ikithibitika kuwa haikuwa taarifa hakiki mtakaa silent kwakuwa kwa makusudi kabisa mmeepusha kuweka code kwa serikali inapoleta wrong message mbele ya bunge. Mbona hamko realistic katika hili?? Mheshimiwa (najua unapata taarifa za humu jukwaani) naomba uijibu hoja hii kivitendo zaidi.
  • Kwa nini unaidhinisha posho kwa wabunge ambao hawahudhurii vikao vya bunge? Unakuta robotatu ya waheshimiwa hawapo ktk session lakini ktk vocha zenu za malipo inaonesha mmewalipa wote. Je mtamkemeaje mtumishi wa UMMA ambaye katika muda wake wa kazi anakwenda mtaani kupiga deal zake ilhali ninyi hamuoneshi mfano bora? Una muda mchache sana kuelekea uchaguzi mkuu. Najua unaweza kubadilisha bunge ktk kipindi hiki.
  • Kama mliwapatia madiwani code ya mavazi (kikanuni/kisheria) katika vikao vyao, kwa nini ninyi mnapata shida sana na kigugumizi ifikapo suala la vazi rasmi la mbunge?? Mbona wewe una vazi maalumu ambalo linakupendeza kweli, wavike wabunge wako ili kudumisha best appearance (kwa kuwa best performance imeshindikana).
  • Nakupa thumb up kwa kufanikisha kuibana serikali bungeni ili iwajibike kwa umma na kuwa kinara wa spika wote niliowafahamu wa bunge la Tanzania kwa kusimamia kidete maadili na vita dhidi ya ufisadi. Lakini kwa jinsi ulivyowasulubu mhula huu, usione wanakuchekea-chekea. Ujue wanahesabu siku zako za kukaa ofisini. Wanaona spika wa aina yako hawafai kwa ustawi wao. Hivyo una kibarua kigumu kweli kurejea ktk kiti chako cha uspika. Waligundua dakika ya mwisho kwamba utawaangusha ndo maana mzee aliyeapa kutorudi ktk siasa za bunge (Msekwa) alipiga big roundturn na kupeleka jina lake lipigiwe kura ktk kinyang’anyiro cha uspika. Nasema your days are numbered in speakerhood ya bunge la Tanzania. Jipe moyo, sisi wapiga kura tunakuheshimu na kukuona kwetu ni baba mwenye huruma na upendo ingawa hakuna asiye na mapungufu. Harufu ya kinyesi haimzuii mwenda haja kuingia ******.

  Nina hoja nyingi sana ila hizi chache nimejitahidi kuzipangilia. Najua wabunge mnasoma humu na mtamsaidia mzee Sitta kuweka sawa masuala mawili matatu ikibidi.

  Naunga mkono hoja
   
 2. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mhhhh, hapa hata jibu nin?
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kila doti ina swali moja. anapaswa kujibu kwa vitendo ndo maana nilisema kwamba maswali yangu yapo kama makala hivi.
   
 4. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Chukua Chako Mapema(CCM)
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Na hapa ndipo TAKUKURU walitakiwa kulichunguza bunge zima kwa kuchukua posho bila kufanya kazi. Ni aibu kwa wabunge kutokuwa bungeni wakati hoja zinajadiliwa - na wengine si ajabu wanakuwa kwenye sehemu sehemu na machangud.. au vibin.. Shame kabisa!!
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Inauma kweli kuona wanafunzi wanakosa walimu kisha hakuna mishahara ya kuwalipa halafu kuna watu wanalipwa bureee kwa nyadhifa zao. Labda malipo ya wabunge ni kama takrima kutoka serikali kuu. Labda, labda, labda
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi ati mbunge wa Tanzania anapata Milioni Tisa (9,000,000/-) kwa mwezi kipato kwa ubunge wake? 35,000,000/- kiinua mgongo kila baada ya miaka mitano?

  Leka
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kuhusu mshahara sijajua figa kamili ila ukiunganisha na poshoz na alawansiz inafikia jirani au zaidi ya hapo.
  Ila kuhusu pensheni ni yes yes yes! five years makumi ya mamilion ambapo mjenga nchi atapiga kazi miaka 40 apate japo hiyo milion 15 ambayo akishaipata tayari ameshakuwa kibogoyo hawezi kuivunjia mifupa sana sana atanunulia unga apike uji akanywe huku akijihisi anazo sana (after 40 yrs?)
   
Loading...