Crucifix
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 1,651
- 588
Kwanza umenishangaza na title ya thread kuelekeza swali kwa Mnyika amabaye sikumbuki kama niliona jina lake miongoni mwa wanakati waliokwenda Ikulu. Kama alikwenda, utasahihisha. Pia Mnyika si kiongozi wa juu kabisa kiuongozi au kiutendaji. Swali lako lilipaswa kuelekezwa kwa Mbowe.
Pili, CHADEMA hawakutoka bungeni eti kwa sababu ya kupingana 100% na yaliyokuwemo ktk muswada, bali walitaka usomwe kwa mara ya kwanza ili upatiwe fursa ya kuuchonga vizuri. Kwa serikali kuusoma kwa mara ya pili, ilikuwa na maana kuwa marekebisho yamefanyika & no room for further editing. Ilikuwa wazi kwa uwingi wa CCM na wapenzi wao CUF kuwa muswada ungepita tu. So ingekuwa kazi bure kukaa na kuchangia.
Baada ya muswada kuwa umepita bungeni (kwa sababu CDM wasingeweza kuuzuia) njia iliyobaki ilikuwa ni kumwona rais na kumsihi asiusaini muswada ili mapendekezo ya CDM yajumuishwe. Kwa hiyo ilikuwa sahihi kumkimbia shangazi, kwenda kwa mjomba. Mjomba akakataa ushauri wa CDM.
Swali lako sasa unapaswa kuwauliza CUF wanaotaka kwenda kuuza sura ikulu wakidhani ile mipicha na rais imewaongezea umaarufu viongozi wa CHADEMA. Hawana sababu ya msingi kwenda ikulu kwa sababu kabrasha lao walishampa mkuu siku nyingi. Wanakwenda kutafuta umaarufu wa magazeti na TV.
Kimsingi, CHADEMA imenufaika na kukutana na rais kwa sababu kimeonesha kuwa mamlaka inajua umuhimu wake na hivyo kukubali haraka haraka ombi la kumwona mkuu. Endapo JK angegoma kukutana na CDM tungekuwa tunaongea habari nyingine sasa hivi. Hata mkuu wa mabalozi wa Euro (Tim) aliishauri serikali kukaa na CDM kwa sababu alihisi CDM ni moto wa kuotea mbali japo yeye ni raia wa kigeni.