Maswali kwa CWT (nimeileta ilivyo)

Conq'ueror

Senior Member
May 13, 2015
171
131
MASWALI KWA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT)
1.Mapato yatokanayo na vitega uchumi vya chama mfano: Mwalimu house na ofisi za CWT kila mkoa (rent), je vinamnufaishaje mwalimu ambaye ni mchangiaji mkuu?

2.Kwanini C.W.T wanakusanya michango kwa wanachama kila mwezi badala ya kukusanya mara moja kwa mwaka kama vyama vingine?

3.Kwanini kuna tofauti katika makato ya kuchangia mfuko wa C.W.T wakati huduma ni sawa? Kuna nini kinachoongezeka kwa anayekatwa zaidi na nini kinachopungua kwa anayekatwa chini? Tofauti hizo zinaletwa na mfumo wa asilimia zilizowekwa na hivyo kuweka wachangiaji katika matabaka yasiyo na tija wakati huduma ni sawa.

4.Je kuna uhalali gani wa kiinua mgongo cha mwanachama anayestaafu kwa uwiano na alichochangia toka uanachama wake hadi kustaafu? Ikiwa kiinua mgongo kilichopangwa na C.W.T kwa sasa ni mabati ishirini (20) tu.

5.Je C.W.T kwa mwaka inakusanya kiasi cha shilingi ngapi kwa waalimu wote Tanzania kwa makato ya asilimia mbili (2%) ya kila mshahara wa mwanachama ambayo pia inatofautiana kulingana na madaraja na fedha hizo zinatumikaje ilihali tayari kuna vitega uchumi?

6.C.W.T inawafanyakazi wangapi kwa kila mkoa na taifa kwa ujumla na posho zao zikoje?

7.Kwa kuwa waalimu wamekua wakinyanyasika na kudharaulika na kutosikilizwa katika halmashauri, Je C.W.T inafanya nini kurudisha hadhi ya mwalimu katika ngazi ya halmashauri ilihali mambo haya yanaendelea kumgandamiza na kumnyanyasa mwalimu?

Watag wadau wote wa Elimu.Plz share we need changes.
 
Tulia kijana!
Nakushauri ufike kwenye ofisi ya wilaya iliyokaribu na wewe utapata majibu ya maswali yako.

Au kama VP nipm nikupe majibu na vifungu vya sheria!

Karibu sana CWT!
Kero zenu zitashughulikiwa na tunaendelilea kutetea na kupigania haki na utu wa walimu kama wafanyakazi wengine wa Tz.
 
Kweli ndugu zangu ifikie wakati tuseme CWT basi maana bado inamnyonya mwalimu na hakuna faida kwasababu hatunufaiki nayo. Kama wangekuwa wanarejesha makato yetu pindi tunapostaafu basi cwt ingekuwa na maana
 
Ifike mahali kama huna lakuchangia utulie, si kila kitu uchangie.Harafu kwakuzingatia kuwa humu wamo watu kwenye heshima zao iweje Leo unageneralize kuwa walimu ni mapoyoyo.Ninaomba mamlaka ya mawasiliano wakuchukulie hatua uungane na mwenzako aliye mkashifu Mh.Rais.Teaching is the mother of all professions, therefore Teachers need respect and honour.Niwewe tu ama Kwa kutojua unaweza mtukana mwalimu.You are cursed!!
 
Ifike mahali kama huna lakuchangia utulie, si kila kitu uchangie.Harafu kwakuzingatia kuwa humu wamo watu kwenye heshima zao iweje Leo unageneralize kuwa walimu ni mapoyoyo.Ninaomba mamlaka ya mawasiliano wakuchukulie hatua uungane na mwenzako aliye mkashifu Mh.Rais.Teaching is the mother of all professions, therefore Teachers need respect and honour.Niwewe tu ama Kwa kutojua unaweza mtukana mwalimu.You are cursed!!

Yule dogo aliye watukana walimu wote ni mapoyoyo na wana IQ ndogo anastahili kuombewa na kusamehewa pamoja na watoto wenzake wenye mtazamo hasi kama wake.

Inawezekana amesahau au haelewi ya kuwa kuna aina mbili za walimu ambao ni wale wa mfumo rasmi na wale ambao sio wa mfumo rasmi mfano wazazi, ndugu na jamaa wengine waliotuzidi umri. Sasa kama unawatukana wazazi/walezi wako waliokufundisha maisha kwa ujumla tangu unazaliwa mpaka unakua! hakika mtu wa aina hiyo ni zaidi ya mwendawazimu.

Kuhusu mtoa mada ametoa maoni chanya kuhusu hao cwt. Binafsi siku nikipata nafasi ya kukutana nao laivu basi watanieleza tu kwa kina kuhusu huu uonevu wao kwa walimu.
 
NYACHA Unaleta Siasa Kwenye Maslah Ya Walimu? Eti Tembelea Ofis! Kwani alikwambia Hazijui Mpaka Akauliza Jf? Mjibu Hapa Tuone Uozo Wenu! Walimu Hii CWT ni Uozo Mtupu.
 
Back
Top Bottom