Prof_Adventure_guide
JF-Expert Member
- Dec 21, 2023
- 519
- 1,463
1. Utekaji na Uuaji
Kwa nini viongozi wa upinzani, wanaharakati na waandishi wa habari wanapotezwa au kutekwa, halafu serikali yenu inakaa kimya bila majibu ya wazi?
Mnaogopa nini hadi kufikia hatua ya kuua na kuteka watu wanaohoji mfumo wenu?
2. Utawala wa Sheria
Kama kweli mnajivunia demokrasia, kwa nini mahakama na vyombo vya dola vinageuzwa zana za kutisha badala ya kulinda haki?
Kwa nini polisi na usalama wa taifa wanatumika kulinda chama chenu badala ya kulinda raia?
3. Haki za Binadamu
Kwa nini mikutano ya kisiasa na maandamano ya wapinzani inazuiwa kwa mabavu, wakati ninyi mnaendelea kufanya mikutano bila vizuizi?
Ni lini mtakomesha tabia ya kuonea wananchi na wapinzani kana kwamba taifa ni mali ya chama?
4. Uwajibikaji
Kila mwaka kuna matukio ya ufisadi, wizi wa fedha za umma na ukandamizaji wa haki, kwa nini hakuna wahusika wakuu wanaowajibishwa?
Ni lini chama chenu kitaweka mbele maslahi ya taifa badala ya kulinda familia chache zinazofaidika na mfumo huu?
5. Hofu na Ukimya
Mnafahamu Watanzania wengi wanaishi kwa hofu ya kuhoji uovu wenu. Mnajisikiaje kutawala taifa linalowaogopa badala ya kuliheshimu?
Mtaendelea kudanganya mpaka lini huku wananchi wakiumizwa, kunyanyaswa na kukandamizwa?