Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,945
Uchawi ulianza kabla ya Sayansi, Vitabu vya dini vinauzungumzia uchawi kuwa upo na kutukataza tusiufanye. Qur an inauzungumzia uchawi kama ni dhambi kubwa sana kuitenda kuliko dhambi zote za duniani, yaan ukifanya uchawi umefanya dhambi kubwa ziadi kuliko zote duniani, then inafata ushirikina, japo ushirikina na uchawi ni baba mmoja mama tofauti. Hizi ni dhambi kubwa kuliko kuua. Naomba niwasihi ndugu zangu waislam wasitamani kuujua wala kuufanya uchawi ila wajue tu kuwa upo na wajue namna ya kujikinga nao.
Wanasayansi wanaujua uchawi na wanaufanya pia, katika sayansi zao lazima washirikishe na uchawi pia, kwamfano ndege kupaa juu kupasua mawimbi... Bila kushirikisha uchawi mwanasayansi hafanikishi hili,
Ujenzi wa barabara, kuna sehemu barabara zinapita inakatwa miti mikubwa.... Miti ambayo wachawi wanaitumia katika mambo yao, hivyo basi mkandarasi kama hajafanya uchawi na kwenda nao sawa hawezi kufanikisha jambo lake, wachina wanaojenga barabara kubwa na madaraja makubwa nao ni wachawi sana tena sana.
Muelevu hawezi kunipinga, mjinga anaweza kunipinga kutokana na kutokujua kwake.
Note: Uchawi upo, utakuja kuujua kama upo yakikufika mambo, ipo siku.
Mkuu, umeandika baadhi ya mambo usiyo na elimu nayo. Umechanganya uchawi na ushirikina, pia unasema katika uislamu dhambi kuu ni uchawi, pia unasema wazungu hurusha ndege angani kwa kutumia uchawi, pia unasema wajenzi wa barabara na wanapong'oa miti hutumia uchawi.
Sio kweli mkuu.



