Maswali kuntu kuhusu uchawi

Maswali kuntu kuhusu uchawi

Africa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
1,504
Reaction score
2,275
Hivi ni kweli wachawi wanaruka usiku na ungo?

Na kama wanaruka, nani aliwahi kuthibitisha kwa macho yake? (naked eyes)

Na wanasayansi mnazungumziaje suala hili la wachawi kuruka na ungo? Mnaliamini?

Teknolojia ya wireless ilitoka wapi? Idea yake....!??? Au ndio mliipata huku kupitia uchawi? Mtu yupo Kihonda Morogoro anamroga mtu yupo Masaki Dar es salaam

Au wachawi nao wanaminara ili kurusha mawimbi?

Nawasilisha!!!!!
 
Shida anataka ithibati za kisayansi kwenye mambo ya uchawi.. Haiwezekani

Uchawi (Magic/sihr), ni tawi moja la sayansi iliyojificha, ni sayansi ambayo haijawekwa wazi kwasababu aghalabu misingi yake inakiuka maadili na utu wa mtu.
 
eti inapoishia sayansi, uchawi ndio unaanzia hapo
 
Naweka nukta ili nipate muendelezo wa majadiliano ya uzi huu. Mshana namuamini katika haya mambo, kila siku hujiuliza mechanism gani hutokea nyuma ya pazia kufanikisha jambo.

1. Mfano mechanism gani hutokea ili mwanaadamu kupata nguvu ya kupaa?.

2. Kipi kinafanyika ili mwanaadamu anajua ama anagundua mwenzake anafikiri jambo fulani kichwani mwake.

Nna mingi sana ya kutaka kufahamu kuhusu physics inayotumika katika mambo haya, kiukweli mm sikubaliani na wale wanaoona taaluma hii sio nzuri, nilichogundua watu wanayoichukia hii elimu hawana uwezo wa kuipata na wale waliyonayo wanaitumia vibaya sana. Ila kama ingewezekana hii elimu inapaswa kuwekwa wazi na kupatikana kwa kila mwenye kuitaka.

Binaadamu anatakiwa awe na uwezo wa kupambana na kumiliki mazingira yake, wakati tunaanza shule tunasomeshwa hisabati, lugha, pamoja na masomo ya kijamii na mambo ya uwiyano wa dunia tunayoishi, ila hatufundishwa kitu sahihi hasa tunachotakiwa kuwa nacho ili kupambana na mazingira yetu.

Sitaki kuamini kinachoitwa uchawi ni taaluma mbaya na ovu, sio kweli; nnachoamini mm watu wenye mafanikio ama ya kibiashara ama kitaaluma (ugunduzi wa kisayansi katika fani za kidaktari, technolojia, mazingira na nyenginezo) kwa namna moja ama nyengine huwa wanataaluma wanazozijua ambapo hawako tayari kutoa kwa wengine kwa uoga wa kwamba wanatoa siri za mafanikio yao.

Taaluma ya kufanya mambo yatokee kwa kasi yaani kwa haraka na uhakika tena kwa wepesi zaidi mbele ya watu mara nyingi huitwa uchawi, wakati ndio elimu tuliyotakiwa kuwa nayo wanaadamu wote tunaojielewa.

Tanbihi; Mwanaadamu mwenye taaluma hii anapokosa uadilifu ndio huwa mchawi.
 
Uchawi mara nyingi ni uchafu unyama ukatili wa ajabu ndani ya jamii na mengi maovu maovu yasiyofaa hata kuelezeka,yenye formulae za ajabu ajabu ambazo mara zifanyapo viumbe wengine kama mashetani au majini ni lazima yasogee na hapo mchawi huamrisha atakalo.
mf.
-Ukichukua koromelo la swala pala kipande ukachoma moto ni lazima NYOKA WAJE FROM NOWHERE!
-Ukimwaga sukari chini ni lazima sisimizi watafika.
-Ukiweka mizoga ni lazima makunguru yatafika hapo.
-Ukimwaga nafaka ni lazima ndege watafika hapo..
 
Uchawi (Magic/sihr), ni tawi moja la sayansi iliyojificha, ni sayansi ambayo haijawekwa wazi kwasababu aghalabu misingi yake inakiuka maadili na utu wa mtu.
sayansi ambayo haijawekwa wazi kwasababu aghalabu misingi yake inakiuka maadili na utu wa mtu.mmh hapana sio kweli kabisa
 
Uchawi hauna ithibati za kisayansi kwakuwa hizi ni kaliba mbili tofauti

Mkuu, Mshana jr, mimi natofautiana na wewe, with due respect, nasema kwamba Uchawi/Magic ni tawi moja la Elimu ya sayansi lakini kwa kipindi hiki ni elimu ambayo haipo wazi kwasababu inakiuka morality ya ubinadamu ili ifanye kazi na pia principle ya kiubinadamu ni kwamba chochote chenye manufaa huwa kinapata maendeleo, (whatever useful must be developed and won't be kept a secret over long time).

Mfano, wachawi hutumia dawa/ nguvu ya kutokuonekana pindi wanapofanya mambo yao ya "kihalifu" (invisibility power), inakuwa vipi??, mimi sijui wanatumia vitu gani kujipakaza mwilini, lakini ni kwamba mchanganyiko materials wanazotumia kujipaka mwanga unapogusa (strike) hizo material mwanga unaorudishwa (reflected ) unakuwa umebadilika mawimbi yaani maeimbi hayo yanakuwa nje ya ile inayoitwa visible spectrum ya uwezo wa macho ya mtu kuona na ndiyo maana kuna viumbe wengine wanaweza kumuona mchawi wa aina hiyo kwa sababu wao visible spectrum yao ni kubwa kuliko ile ya mtu.

Nadhani unajua ni jinsi gani sisi binadamu tunaweza kuona vitu.

Mfano huu unafanana na stealth fighter jet ambayo radar inashindwa kuiona/ku-detect kwa sababu inameza mawimbi ya radar au inayarudisha katika mawimbi mengine kuweza kutambuliwa na radar.

Hapa swali ni mchanganyiko wa material zipi zinafanya mchawi asionekane??!;, ukiuliza unaweza kuambiwa huo mchanganyiko na ukashangaa na ukajuta kwanini uliuliza.😷😷🤫
 
Mkuu, Mshana jr, mimi natofautiana na wewe, with due respect, nasema kwamba Uchawi/Magic ni tawi moja la Elimu ya sayansi lakini kwa kipindi hiki ni elimu ambayo haipo wazi kwasababu inakiuka morality ya ubinadamu ili ifanye kazi na pia principle ya kiubinadamu ni kwamba chochote chenye manufaa huwa kinapata maendeleo, (whatever useful must be developed and won't be kept a secret over long time).

Mfano, wachawi hutumia dawa/ nguvu ya kutokuonekana pindi wanapofanya mambo yao ya "kihalifu" (invisibility power), inakuwa vipi??, mimi sijui wanatumia vitu gani kujipakaza mwilini, lakini ni kwamba mchanganyiko materials wanazotumia kujipaka mwanga unapogusa (strike) hizo material mwanga unaorudishwa (reflected ) unakuwa umebadilika mawimbi yaani maeimbi hayo yanakuwa nje ya ile inayoitwa visible spectrum ya uwezo wa macho ya mtu kuona na ndiyo maana kuna viumbe wengine wanaweza kumuona mchawi wa aina hiyo kwa sababu wao visible spectrum yao ni kubwa kuliko ile ya mtu.

Nadhani unajua ni jinsi gani sisi binadamu tunaweza kuona vitu.

Mfano huu unafanana na stealth fighter jet ambayo radar inashindwa kuiona/ku-detect kwa sababu inameza mawimbi ya radar au inayarudisha katika mawimbi mengine kuweza kutambuliwa na radar.

Hapa swali ni mchanganyiko wa material zipi zinafanya mchawi asionekane??!;, ukiuliza unaweza kuambiwa huo mchanganyiko na ukashangaa na ukajuta kwanini uliuliza.
Uko vyema Mokaze, hapo panapo huo mchanganyiko ndio nipatakapo mm.
 
To break the evil effects of black magic. Recite the following Dua;
“Bismillahi wa billahi bismillahi wa maa shaa-allaahu bismillahi wa laa hawla wa la quwwata illa billah qaala moosa maa ji-tum bihis sih;r innallaha sayubtiluh innallaha laa yus’lih’u a’malal mufsideen fawaqa-a’l h’qqu wa bat’ala maa kanoo ya’-maloon faghulibo huna lika wanqalaboo s’aagghireen.”
 
Back
Top Bottom