Prezidah
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 750
- 182
HIZI NDIZO HOJA 10 ZINAZOMTAFUNA
LOWASSA. Soma hapa kujua:
1. Gazeti la Raia Mwema la Novemba 2010 , liliripoti na kuonyesha picha ya nyumba ambayo familia yako inamiliki Uingereza. Ukasema ni ya mwanao. Je, kwa nchi maskini kama ya kwetu, ni sahihi kwa kiongozi mkubwa kumiliki nyumba kubwa na ya kifahari nje ya nchi?
2. Mkapa alipounda Baraza la Mawaziri jipya mwaka 1995 alikuacha. Wengi wanasema kwamba Mwalimu alimwambia asikupe hata Uwaziri. Je, Kwanini mwalimu Alikukataa?
3. Tangu mwaka 1994, yaani miaka 20 sasa, Afrika ya Kusini imekuwa inakodisha nyumba yako Masaki kama Ubalozi wake. Kuna tetesi kwamba huko nyumba walitaka kuhama lakini wakaogopa kuihama nyumba inayomilikiwa na kiongozi mkuu na kuna tetesi kwamba sasa wanataka kuhama lakini wanatishiwa kwamba hamuwezi kuhama nyumba ya Rais ajaye. Ni kiasi gani cha fedha umepata kwa miaka 20 ya kukodisha nyumba hiyo ? Je, kiasi hicho kimeripotiwa kwenye fomu ya maadili?
4. Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo ya Masaki ambayo Mzee Mandela alikuja mwaka 1994 kuufungua ubalozi mpya wa Afrika ya Kusini ndicho chanzo kikuu cha Mwalimu kusema kwamba inakuwaje kijana wa miaka 41, akiwa mtumishi wa umma maisha yake yote na mshahara wake unajulikana, anamiliki hekalu kama lile na tena kulikodisha kwa Serikali ya kigeni. Je, unasemaje kuhusu hili?
5. Pia unamiliki ranchi kubwa sana kule Mzeri Handeni. Ranchi hiyo ilikuwa ranchi ya Taifa lakini ukajimegea na sasa umeipanua kwa kumega maeneo zaidi. Ranchi hiyo uliipata ukiwa bado kiongozi wa umma. Je, mtu aliyewahi kuwa Waziri wa Mifugo na Waziri Mkuu kujiuzia ranchi iliyokuwa ya Serikali inaendana na dhana ya uongozi safi na uliotukuka? Tukikupa madaraka makubwa zaidi hautajiuzia kila kitu? Vilevile, katika nchi ambayo wananchi wengi hawamiliki ardhi, kwa kiongozi anayetaka kuwa Rais wetu, kuhodhi eneo kubwa la ardhi, inatuma picha gani kwa
wananchi hao?
6. Kwenye sakata la Richmond, ujasiri ni kusema ukweli au kubwaga manyanga? Kama ungesema ukweli na usingejiuzulu kwenye Richmond, Chama kingeathirika vipi wakati unasema hakuna kosa lililofanyika?
7. Kwanini kwenye kila tukio la kitaifa ukisimama tu karibu na Kikwete unahangaika kutuma picha kwenye magazeti na mitandao?
8. Katika miaka yako 40 ya utumishi wa umma, kuna jipi jipya ambalo umelisahau na sasa utalifanya kwenye Urais?
9. Umekuwa Waziri wa Ardhi, mbona matatizo ya ardhi bado tele nchini? Umekuwa Waziri wa Maji, mbona matatizo ya maji bado tele? Umekuwa Waziri wa Mazingira, mbona kuna matatizo ya uchafuzi wa mazingira? Umekuwa Waziri wa Mifugo, mbona wafugaji bado maskini na wanahangaika? Huo urais unautaka wa nini kama uwaziri umekushinda?
10. Kwenye sikukuu ya Mwaka Mpya, kila MNEC kapata milioni 1, hizo ni milioni 370 na kila mjumbe 500, 000 hizo ni bilioni 2. Hizi pesa zinatoka wapi na zitarudishwa vipi? Je, kuna zoezi la usafishaji wa pesa chafu linalofanywa kupitia kampeni yako?
1. Mkuu mtu kuwa na nyumba nje ya nchi si neno bali ishu ya msingi ni kwamba ameipataje. Wapo watz wengi wengi wenye nyumba nje ya nchi hata miki au yule jamaa wa dubai.
2. Kuhusu kuachwa kwenye baraza la mkapa 1995 haimaanishi chochote kwa sababu haijaandikwa kwenye katiba kwamba kila baraza lazima edu awepo.
3. Usiamini sana tetesi maana ndo kazi kubwa ya wabongo waleo kuzusha maneno. Lakini tatizo liko wapi nyumba yake kukodishwa na ubalozi, mbona taasisi nyingi za umma na binafsi even international ones zipo kwenye nyumba za watu binafsi? ??? Au tatizo edu?
4. Miaka 41 si kidogo ndugu yangu wapo vijana siku hizi wanamiliki mijumba ya hatari at age of 23-30. Nenda kaangalie kwa msando alafu thamanisha.
5. Ranchi ya mzeri wala hajajimilikisha kama unavydhani wewe na kupotosha jukwaa. Ranchi ina shareholders 9 na mchakato ulifuata taratibu zote au ulitaka wazungu wawekeze. Kumbuka ufugaji ni asili yake so sioni tatizo.
6. Richmond majibu yake unayo but hulazimishwi kuamini
7. Suala la picha ni kama humu jf niambie kuna nyuzi ngapi zinazomhusu je ameziazisha yeye ???? Simple like that tofautisha picha ya kujipiga na iliyopigwa na mtu mwingine. Kiufupi imefika mahali magazeti hayauziki bila story ya mshikaji na ndiyo ishara ya kupendwa the same to jf.
To be continued. ..