Maswali kuhusu mambo ya kiimani

Maswali kuhusu mambo ya kiimani

baharia 1

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
1,778
Reaction score
2,052
Maswali Kuhusu Uchawi na majina


1. Je, mtu mwenye jina la kimungu kama Yesu, Muhammad,Michael, au Gabriel anaweza kuathiriwa na uchawi?

2. Je, majina haya yana kinga yoyote dhidi ya uchawi au nguvu za giza?

3. Ikiwa mtu mwenye jina la kimungu atalogwa, je, uchawi huo unaweza kuwa na athari yoyote kwao?

4. Je, kuna imani au hadithi zozote zinazosema kuwa majina haya yana nguvu za kipekee za kulinda dhidi ya uchawi?

5. Je, unafikiri kuwa jina la mtu linaweza kuathiri uwezo wa uchawi kumdhuru?

Naombeni majibu maana nachanganyikiwa
 
Majina hayana Kinga yoyote dhidi ya mambo ya kiroho....

Mfano: Wewe jina lako ni Baharia, Hilo ni jina lako na sio wewe.

Wewe ni nani? Wewe ni roho inayoishi ndani ya mwili, Kwamaana hata huo mwili sio wewe bali ni nyumba unayoishi.

Kwa maana hiyo, mtu ni roho na sio jina Wala mwili, na kinachoweza kudhuru roho ni nguvu za kiroho pekee, eidha nguvu za Nuru au za Giza.
 
Sijawahi kuona mswahili anaitwa Yesu ila kule rwanda kuna Akayesu, Bizimungu. Kule hispania, ureno, argentina kuna watu wanaitwa Jesus, Angel, Maria. Maria hata waswahili wapo ila sijui watu hao kama kuna athari wanazipata kutokana na kuitwa majina ya Kiungu
 
Kuna wachezaji mpira wa miguu wa kimataifa wanaitwa majina ya Kiungu, kuna Angel Di Maria, Gabriel Jesus, Mohamed Salah ! hatujaona athari za majina hayo kwao. Labda ni watu wa kawaida tu kama wengine
 
Sijawahi kuona mswahili anaitwa Yesu ila kule rwanda kuna Akayesu, Bizimungu. Kule hispania, ureno, argentina kuna watu wanaitwa Jesus, Angel, Maria. Maria hata waswahili wapo ila sijui watu hao kama kuna athari wanazipata kutokana na kuitwa majina ya Kiungu
Rwanda hawajui varta kama DRC na Tanzania nyumba unaweza kuikimbia kwa vituko.
 
Huku mtaani unaweza kusikia mfanyabiashara karogwa au hata muuza chips au mama ntilie.
Mbona mapolisi wanaotesa watu hua hawarogwi? Mbona wanasiasa wezi, wauaji, wanaofuja mali za umma hawarogwi
 
1. Jina haliwezi kumkinga mtu na uchawi japo majina yenyewe nayo ni ya kichawi.

2. Nani kakwambia kuwa hadithi za paka na panya ni za kweli?

3. hapa umerudia swali la kwanza bila kujua?
Umerudia swali la tatu. Hivyo, jibu ushapewa.

5. Umerudia swali la pili pia na jibu ushapewa. Nakushauri ujifunze namna ya kuuliza maswali badala ya kurudia swali lile lile ukijiaminisha umeuliza maswali mengi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom