Maswali ambayo UKAWA huyakimbia

Maswali ambayo UKAWA huyakimbia

Tanzania kwa taarifa yako imebaki na sifa moja tu kisiwa cha amani na hakuna mahali kuna umaskini kukawa na amani,watz wameamka sasa na wameona kifuniko cha amani huku wakifa kwa umaskini ni kiini macho sasa wameamua kuondoa mfumo ccm na kuweka mfumo mwingine ili wanufaike na rasilimali zao na hawaitaji mambo mengi ni kuwezeshwa na kuonyeshwa dira only hayo tu ila ccm walingundua kwamba wanapendwa na watu maskini sana sasa wanajua watu wakitajirika wataichukia ccm,wanatakiwa kujua kwamba niheri kumsaidia mtu na akuchukie kuliko kumnyima haki yake na ukaendelea kukaa na yeye hilo ni bamu utakuwa umefuga na ipo siku litakuripukia
 
Kuna watu wanasema CCM haijafanya chochote kwa miaka 54. Ni sawa tu. Ila je, somo la Civics linafundishaje? CCM ilianzishwa 1961 au 1977?
¤Kama inazungumziwa tokea TANU basi ni kuanzia 1954 (kwa hiyo miaka 61). Kama ni CCM basi ni kuanzia 1977 (miaka 38).
Kama ni kuanzia mfumo wa vyama vingi (mwaka 1992) basi ni miaka 23. Kama ni tokea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi (1995) basi ni miaka 20.
¤Bila kujali ni 61, 54, 38, 23 au 20 kuna maswali magumu ma-3 (kama HARD TALK ya BBC enzi za Tim Sebastian)

1. Lowassa na Sumaye (walio UKAWA hivi sasa) walikuwa mawaziri wakuu kwa jumla ya miaka 13. Je, muda ambao CCM haijafanya lolote inajumuisha hiyo miaka 13?

2. Lowassa si anasema alisimamia shule za kata, kuvunja mkataba wa City Water, kuvuta maji Kahama kutoka Ziwa Victoria na ujenzi wa UDOM. Je, alisimamia akiwa chini ya chama gani? APPT Maendeleo?

3. Vyama vyote vikubwa na maarufu zaidi nchini vinatumia jina na sauti ya Mwalimu Nyerere kwenye matangazo yao ya audio na mabango. Miaka hiyo ambayo CCM haijafanya lolote je, inajumuisha miaka 23 ambayo Mwalimu Nyerere alikuwepo madarakani kama rais (1961/1962-1985)? Je, inajumuisha pia miaka mi-5 ya ziada ambayo Mwalimu Nyerere aliendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM (1985-1990)?

kama hujui kusoma angalia hata picha. utawala wa mkapa dola ilikuwa shilingi ngapi na sasa ni shilingi ngapi.
tukiwa na ccm kila rais akija anaongeza watu wa kuikamua nchi.
mfano japo haitatokea tena: kama lowasa angegombea akiwa ccm asingefanya cha zaidi maana hata kama angetaka kupiga kazi mafisadi wa ccm wangemwekea brake.

ndiyo maana ccm adui yetu sio magufuli. ni ccm

ccm wanataka waweke kilaka ikulu. kamtu hakajui hata mahusiano na nchi nyingine.
huyu atakuwa mtu wa ndio mzee.

kama magufuli angekuwa tegemeo au mchapa kazi tungemwona anashika nyazifa za juu kama waziri mkuu, waziri wa mambo ya nje,waziri wa fedha. wizara ya ujenzi sio wizara nyeti kiasi hicho.
Hata lowasa alipojiuzuru JK jakumfikilia magufuli kuwa waziri mkuu.
Hii nchi ni yakuongozwa na watu wenye busara kama Nyerere,sokoine na lowasa.

Magufuli kama anataka kazi afungue kampuni ya mayweather
 
Akiwa waziri magufuli alihonga nyumba za serikali. Sasa akiwa rais atahonga nn?
Kumbuka rais wa awamu ya tatu alihonga wizara ya fedha kwa ajili ya dili la mwanamke.
Rais wa awamu ya nne alikuwa anahonga wilaya na mikoa.
Ccm inanuka uchafu haisafishiki. Magufuli ni dodoki chafu

Hutockia sumaye wala Lowasa wamesimama wanaliongelea hilo mbele ya magufuli sababu wao ndio wa kwanza kununua hizo nyumba ala mbona kawajengea nyumba hao hao mikocheni mbona hamsemi
 
Acha kujifariji kwa hesabu rahisi kiasi hicho, tuambie kizuri kilichofanywa na CCM. Huduma za afya, elimu nchini zikoje!, thamani ya shiling yetu ikoje! uchumi je!
Ni kweli Mkuu hii ni Hesabu nyepesi sana ni kama ile ya kusema
Celtel na Zain Siyo Airtel, au Mobitel na Buzz siyo TIGO.
 
Mi naona bora wasitishiwe zile stahiki zao wanazopewa kama mawaziri wakuu wastaafu maanake huu ni ufisadi mwingine halafu ni sawa na kwamba wanatutukana tu.

Naongeza swali.

Je hawajui kuendelea kupokea stahiki zao kama mawaziri wakuu wastaafu ilhali wanasema hawakufanya lolote huo ni WIZI na UFISADI na ni matusi kwa walipa kodi?

Sumaye alidai ardhi anayohodhi aliinunua kupitia kiinua mgogo alicholipwa baada ya kustaafu.

Swali:Kama amekiri kutokufanya chochote for ten years,je mgongo uliinama kwa kupiga puli? (I mean kucheza pool table)

Kwa nini hakuyakataa hayo mafao kwa kuwa anajua hakufanya lolote?
 
Tatizo Hakuna SWALI La Msingi Hapo!! Hivi MAISHA Ya Mtanzania Ni Hayo Mafanikio Tu!!?? Au Ya Hapo!!!?? Kama Kumejengwa Barabara Nchi Nzima, Je, Mtanzania Wa Kigoma, Rukwa, Tabora, Kagera, Mara, Mwanza, S/nga N.k. Anamudu Kusafiri Au Kusafirisha Mazao Yake Kwa Njia Hiyo!!!?? Ambayo Gharama Kubwa Mno Kwake!! Ukilinganisha Na Treni!!!?? Maji S/nga Na Kahama!! Je, Isaka, Tinde, Geita Na Tanzania Yote Kuna Maji!!??? Ikiwa Hapa Dar Yenye Kila Kitu Maji Safi Na Salama Hakuna, WATU Tunakunywa Maji Machafu!! Je, Hali Ikoje Tunduru, Masasi, Urambo, Skonge, Busega, Ngudu, Nzega Igunga, Manyoni, Itigi, Singida!! Kila Kona Ni Kilio! Je, Hiyo Miaka Ya CCM 38 Ndio Tumefikia Hapa?? Hata Huduma Muhimu Tu, Zimewashinda!!!?? Kabla Ya UHURU Elimu Bora Ilikuwa Bure, Huduma Bora Za Afya Bure, Maji Safi Na Salama Bure!! Na J.K. NYERERE Alizikuta Hivyo Akaendelea Nazo!! Shida Ikaanzia Miaka Ya 80!! Sasa Kama Kabla Ya UHURU Hali Nzuri Ktk Huduma Za Kijamii, Na IMEKUWA HOVYO Miaka 20 BAADA Ya Kupata UHURU!!! Tunaenda Mbele, Tumesimama Au Tunarudi Nyuma!!!!!?? Ukilinganisha Hivi Sasa Tunatumia Rasilimali ZETU ZOTE, Ambazo Mwl. NYERERE Alidhihifadhi!! Alitumia PAMBA, KATANI, KAHAWA, KOROSHO, UFUTA N.k . Kuendesha Nchi, Na Huduma Bora Za Kijamii Zilipatikana!! Shida Ni Nini KWETU Hata Tukiwa Na Almasi, Tanzanite, Dhahabu, Makaa Ya Mawe, Chuma, Ulanga, Gesi, Uranium, Mbuga Za Wanyama, Bahari Yenye Bandari 3, Maziwa Makuu 3, Mlima K/njaro!! Hata Tunazidiwa Kiuchumi Na Nchi Kama Rwanda!!!!!?? ALAFU Leo Miaka 50 Ya UHURU Tukae Kitako Tujisifu Eti Tumepiga Hatua KUBWA Kiuchumi!! Huku Uchumi Huo Haukasi MAISHA Ya Mtanzania!!! Bali Ni Kundi 1 Lililo Na MAMLAKA Ya Kuongoza!! Ikiwa Leo Kuna Wtt Wa Makabwela Wanasoma Wakiwa Ktk Magofu, Chini Ya Miti, Chumba 1 Wtt. 100, Tena WAMEKAA Chini!! ALAFU Mnajadili Mafanikio Wkt. Mama Mjamzito Anaendelea Kufa Kwa Kukosa Huduma Bora Ya Uzazi!!! UPUMBAVU MKUBWA SAAANA HUO!!!
 
Sasa tuambie kama tanu na asp wameunda ccm wahusika si haohao usituletee danganya toto hata simba imeanzishwa 1936 na imepitia majina mengi je ilibadilishwa jina na kuitwa simba kwanini wanasema imeanzishwa 1936 tumia akili kura yangu ni lowasa.wameuza viwanda mashamba hospitali hakuna dawa vijana hakuna ajira dola iko juu maisha magumu kila mtu anajua kasoro wewe mtoa post na atakayewapigia kura apofuke macho na alaaniwe milele mungu mbariki lowasa mungu ibariki tanzania mtu yuko ccm anashangaa nini eti twiga kupanda ndege?
 
kama hujui kusoma angalia hata picha. Utawala wa mkapa dola ilikuwa shilingi ngapi na sasa ni shilingi ngapi.
Tukiwa na ccm kila rais akija anaongeza watu wa kuikamua nchi.
Mfano japo haitatokea tena: Kama lowasa angegombea akiwa ccm asingefanya cha zaidi maana hata kama angetaka kupiga kazi mafisadi wa ccm wangemwekea brake.

Ndiyo maana ccm adui yetu sio magufuli. Ni ccm

ccm wanataka waweke kilaka ikulu. Kamtu hakajui hata mahusiano na nchi nyingine.
Huyu atakuwa mtu wa ndio mzee.

Kama magufuli angekuwa tegemeo au mchapa kazi tungemwona anashika nyazifa za juu kama waziri mkuu, waziri wa mambo ya nje,waziri wa fedha. Wizara ya ujenzi sio wizara nyeti kiasi hicho.
Hata lowasa alipojiuzuru jk jakumfikilia magufuli kuwa waziri mkuu.
Hii nchi ni yakuongozwa na watu wenye busara kama nyerere,sokoine na lowasa.

Magufuli kama anataka kazi afungue kampuni ya mayweather

lowasa rais magufuli anapewa wizara ila ccm itoke tu haina jipya mfumo unatuumiza watz.
 
Acha kujifariji kwa hesabu rahisi kiasi hicho, tuambie kizuri kilichofanywa na CCM. Huduma za afya, elimu nchini zikoje!, thamani ya shiling yetu ikoje! uchumi je!

Bro umeyalewa maswali?
 
Hivi el alipigia kura ya ndio rasimu mupya ya katiba? Afu kwa nn hakutoka nje km ukawa walivyofanya maana tunaambiwa n mtu wa maamuzi magumu na katiba ilikuwa ni kwa watz wote tabia ya ujasiri haisubuli mpaka ukatwe ndio uhame
 
Huyo mzee ndiyo alikuwa mastermind kuhujumu rasimu ya katiba ya wananchi kwa sababu ilikuwa inampunguzia nguvu rais ajaye na ye anataka kuwa rais mwenye nguvu.
 
Hii ni kudhibitisha kuwa kama mtu hana akiri ya maiti ni ngumu sana kuwa mwanaccm au shabiki wa ccm.

Naomba nikusaidie na akiri zako za maiti,
1.Ccm ilitokana na muungano wa vyama viwili(TANU na ASP) kwa maana nyingine ni kuwa wanachama waliokuwa wa TANU na ASP ndo hao hao walikuja kuwa wanachama wa ccm.
2.Sera za TANU na ASP ndo hizo hizo zilizokuja kuwa sera za ccm
3.Mwenyekiti wa TANU wa wakati ule ndiye huyo huyo ndiye alikuja kuwa mwenyekiti wa kwanza wa CCM
4.Rasilimali zilizokuwa za TANU na ASP ndo hizo zilikuja kuchukuliwa na ccm
5.Madaraka waliyokuwa nayo TANU na ASP ndo hayo hayo yaliridhiwa na ccm

Kwa kifupi kilichobadilika ilikuwa ni jina tu yaani toka TANU na ASP na kuwa CCM-Chama cha Mafisadi au Chukua Chako Mapema.

Kuhusu swala la Lowassa na Sumaye ni kwamba,matarajio ya watanzania tulio wengi ni kwamba ccm ina mfumo/system ya kuongoza nchi na watu waliomo kwenye huo mfumo/system wanafanyakazi kama timu moja.Lakini kwa maelezo yako hapo juu na hali halisi tunayoiona kwenye kampeni ,inaonesha ama ccm ilitengeneza mfumo mbovu kabisa wa utendaji serikalini kiasi kwamba si rahisi watu serikalini kufanya kazi kama team moja na ndo maana unaulizia individual achievements au kwa miaka 54 ya uhuru ccm imeshindwa kabisa kutengeneza mifumo dhabiti ya utawala na uongozi wa nchi yetu.AIBU HII AIBU HII

Kumbuka-TEAM work-Together Every one Achieves More-sasa kuulizi Lowassa na Sumaye kutofanya chochote hii ni kuivua nguo ccm

Hiyo ya vyama kutumia kutumia audio ni upofu tuliosababishiwa na ccm kiasi kwamba inaonekana katika watanzania 45 milioni hakuna mtanzania mmoja mwenye akili anayeweza kufikiri tofauti au zaidi ya Nyerere.Hii ni shida nyingine kwa mtazamo wangu tuliyosababishiwa na ccm
Yaani tunamwabudu mwanadamu mwenzetu

umeacha kusoma vizuri uelewe umekimbilia kujibu kwanza
 
Sasa tuambie kama tanu na asp wameunda ccm wahusika si haohao usituletee danganya toto hata simba imeanzishwa 1936 na imepitia majina mengi je ilibadilishwa jina na kuitwa simba kwanini wanasema imeanzishwa 1936 tumia akili kura yangu ni lowasa.wameuza viwanda mashamba hospitali hakuna dawa vijana hakuna ajira dola iko juu maisha magumu kila mtu anajua kasoro wewe mtoa post na atakayewapigia kura apofuke macho na alaaniwe milele mungu mbariki lowasa mungu ibariki tanzania mtu yuko ccm anashangaa nini eti twiga kupanda ndege?

ona ulivyokurupuka... swali ni hiyo miaka 54 umeanza kuhesabu lini na kwanini
 
Hutockia sumaye wala Lowasa wamesimama wanaliongelea hilo mbele ya magufuli sababu wao ndio wa kwanza kununua hizo nyumba ala mbona kawajengea nyumba hao hao mikocheni mbona hamsemi

Bahati mbaya nahitaji muda wa kutosha kukuelewesha. Sijasema walionunua. Soma tena hapo chini
Akiwa waziri magufuli alihonga nyumba za serikali. Sasa akiwa rais atahonga nn?
Kumbuka rais wa awamu ya tatu alihonga wizara ya fedha kwa ajili ya dili la mwanamke.
Rais wa awamu ya nne alikuwa anahonga wilaya na mikoa.
Ccm inanuka uchafu haisafishiki. Magufuli ni dodoki chafu
 
Sasa tuambie kama tanu na asp wameunda ccm wahusika si haohao usituletee danganya toto hata simba imeanzishwa 1936 na imepitia majina mengi je ilibadilishwa jina na kuitwa simba kwanini wanasema imeanzishwa 1936 tumia akili kura yangu ni lowasa.wameuza viwanda mashamba hospitali hakuna dawa vijana hakuna ajira dola iko juu maisha magumu kila mtu anajua kasoro wewe mtoa post na atakayewapigia kura apofuke macho na alaaniwe milele mungu mbariki lowasa mungu ibariki tanzania mtu yuko ccm anashangaa nini eti twiga kupanda ndege?

Kwahiyo toka 1961 huoni kitu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom