Maswali 11 juu ya ujio mpya wa Lipumba

Maswali 11 juu ya ujio mpya wa Lipumba

Na, Emmanuel Lukwaro.

Prof Ibrahimu Haruna Lipumba, Aliyekuwa mwenyekiti w Chama Cha Wananchi CUF, na kujiuzulu mwezi November mwaka jana. Ameibuka upya na kusema kuwa amemuandikia katibu mkuu wa chama hicho barua ya kuomba kutengua maamuzi yake ya kujiuzulu na kwamba arejeshwe kwenye nafasi yake ya uwenyekiti.

Prof Lipumba ametamka hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa hababari jijini Dar es salaam. Hata hivyo uamuzi huo wa Lipumba umenisukuma kufikiri na kutafakari kwa kina hatimaye kujiuliza maswali haya 11.

1.Tatizo kubwa na la msingi lililopelekea kujiuzulu kwa mujibu wa maelezo yake lilikuwa Lowasa kujiunga na ukawa,Je lowasa ameshaondoka ukawa? Au akirejeshewa nafasi yake ataitoa CUF UKAWA?

2.Prof Lipumba aliondoka wakati UKAWA wamemkariribisha Lowasa na kumpa nafasi ya kugombea uraisi ambayo naye aliihitaji. Je hakujivuwa uwenyekiti kwa hasira (kususa ) baada ya kukosa nafasi hiyo?

3.Prof Lipumba amekaa nje ya uongozi wa CUF kwa miezi takriban saba.Lakini katika kipindi chote hicho hakuona umuhimu wa kuongezea nguvu upinzani bali wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu wa chama. Je huu sio mkakati wa kukivuruga chama na UKAWA?

4.Je kati ya sasa na kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu ni wakati gani ambao upinzani ulihitaji nguvu ya ziada?
Prof amejenga hoja kuwa anataka kurejea nafasi ya uwenyekiti ili kuuongezea upinzani nguvu katika kipindi hiki.

5.Je Prof Lipumba kama msomi haamini kuwa mwanachama wa kawaida (asiye kiongozi), anaweza kuwa na mchango mkubwa kukijenga chama wakati mwingine kuliko hata kiongozi? au yeye hajazoea kuwa mwanachama wa kawaida?.

6. Je Prof Lipumba haamini kuwa CUF kuna watu wengine wenye uwezo wa kuongoza, hasa nafasi ya uwenyekiti isipokuwa yeye tu?. NB, amekuwa mwenyekiti kwa takriban miaka 20.

7. Baada tu ya uchaguzi alifanya ziara ya kwanza ikulu, kuonana na kuzungumza na raisi hatuwezi kujua kuwa walizungumza nini zaidi na kukubaliana nini. Je tunashindwaje kuamini kuwa amekosa matumaini juu ya kile kilichompeleka kule na/au makubaliano ya alichokuwa akikitaka yameshindwa kutekelezwa hivyo kuamua kurudia tu matapishi yake?

8. Je kwanini tusiamini kuwa katika ziara hiyo vilevile huenda mambo yaliyojadiliwa ilikuwa ni namna ya kuusambaratisha upinzani na hiki anachokifanya sasa (Kutaka kuureja uwenyekiti) ni sehemu ya mkakati huo?

9. Endapo atafanikiwa kurejeshewa nafasi yake, Je siku ikitokea tena akatofautiana na viongozi wenzake hatajiuzulu na kama hatajiuzulu hatawashughulikia anaotofautiana nao?

11. Amesema ameandika barua ya kutengua uamuzi wake wa awali baada ya kuombwa na kushawishiwa sana na viongozi wa dini pamoja na wanachama wa Chama Cha Wananchi CUF. Je kati ya wakati huu na wakati akijiuzulu ni wakati gani ambao hao wanachama na viongozi wa dini walimshawishi na kumuomba asijiuzulu?.

Wakati ule nakumbuka wanachama na wafuasi walizuia press confference yake mpaka awaambie kwanza kile alichokusudia kuzungumza na waandishi wa habari. Lakini kipindi hiki sijawahi kusikia hata maandamano ya watu kumi kumuomba arejee.

11. Mwisho, Wakati akijiuzulu nafasi ya uwenyekiti alituambia nafsi imemsuta kuisapoti ukawa ambayo imekiuka misingi ya uanzishwaji wake. Je akirudi nafsi haitamsuta kufanya kazi na viongozi wenzake wa CUF na UKAWA aliowaachia kazi ngumu ya uchaguzi na sasa kurejea baada ya kazi hiyo kukamilika?, Je atafanyaje kazi na wa wabunge na madiwani wa CUF na UKAWA ambao akiwa kama kamanda mkuu aliwatelekeza wakati wa mapambano?.

Chama cha wananchi CUF kinapokwenda kufanya maamuzi kuhusu hoja hii ya lipumba, ni muhimu kuwa makini sana na kufanya tafakari ya kina ili kufikia maamuzi yatakayokuwa na afya katika ustawi wa demokrasia na harakati za UKAWA kukamata dola 2020.
Kuna tetesi kwamba alipewa kitita ili kusaliti na alionekana kigali akiwa njwii akipiga mtindi ( mwislam feki ) , hapo kwenye no 7 unaweza ukawa umegonga penyewe , maana ziko tetesi kwamba aliahidiwa ushauri wa mambo ya uchumi , baada ya kupigwa chini hana pa kwenda na kibaya zaidi hata zile taasisi za kimataifa zilizokuwa nafanya naye kazi zimemkataa .

Kuna tetesi kwamba wiki ijayo hasa baada ya tamko la viongozi wa cuf atahamia rasmi ccm .

Atapewa kazi fulani lumumba ya kufufua mashirika ya chama kama marehemu SUKITA , Hii ni aibu sana kwa maprofesa wengine wa nchi hii.

Leo nimejua kwanini Dr Rutengwe alimwaga machozi .
 
Kwani ukawa ni chama
Kipindi hiki kila mtu anaimarisha chama chake ndio maana waliokamatwa kahama na mwanza sio ukawa ni viongozi wa chadema cuf wanasiasa zao za ndani waacheni waamue nini hatma yao kisiasa ukawa sio chama.
 
Huyu baba hata simwelewi,
Kwasababu sababa za yeye kuondoka bado hazijarekebishwa
Sasa je ameamua kurudi hivyo hivyo ili apambane na hizo sababu?
 
Lipumba ndio msomi pekee mwenye maono toka lipumba akae kando CUF imeyumba sana
Unaizungua CUF ipi? Hii ambayo chini ya uenyekiti wa Lipumba kwa takribani miaka 20 iliambulia wabunge wawili bara.Na nje ya Lipumba imejizolea wabunge 9 bara.Rudi tena kajipange umeshindwa kuwashawishi GT
 
Si ajikalie kama mwenzake mrema wote hawa walisaliti vyama vyao kwa ahadi hewa , mrema kila kukicha analilia job yake aloahidiwa LIPUMBA amkomalie MWIGULU alimuingiza choo cha kike
 
Nafasi aliyoahidiwa ya mshauri wa rais wa mambo ya uchumi imeshindikana
 
Ma professor wa namna hii wanapatika ktk nchi ya mwendokasiiiiiii tuuu
Lipumba amekurupuka, katika hali ya kawaida ni ngumu sana kukubaliwa kwa kuwa wakati alipohitajika zaidi aliwasaliti wenzake pamoja na usaliti huo bado wenzake wamefanya vizuri kuliko wakati wote alipokuwa nao,hii inathibitisha kuwa hata siku za nyuma hawakuwa wanafanya vizuri kwasababu yake kwa hiyo yeye alikuwa tatizo katika mapambano ya chama.Ni busara zaidi kwake sasa kuendelea kuangalia wenzie namna wanavyopiga kazi, alikuwepo miaka ishirini hakuleta tija alipotoka miezi miwili tu chama kikaleta matokeo mazuri zaidi ya yale ya miaka 20 ya prof. Ni busara kwa Lipumba aendelee na tafiti kama alivyoutangazia umma mwezi August 2015.
 
cuf na lipumba wananikumbusha hadith ya "kama mnataka mali mtazipata shambani"
 
Good news ni kwamba jamaa kwakua barua yake haikujadiliwa na mamlaka husika, then he is mwenyekiti by now. Hii nayo analeta maswali kwanini tangu pale alipoandika barua haikujadiliwa na kutolewa maamuzi?
 
,,,,alinikera xanaili kuna tetesi Maalim kampiga chini na kama kwl n maamuz sahihi kabisa,,,,,huu jamaa anatumika na wala si vinginevyo
 
Lipumba ndio msomi pekee mwenye maono toka lipumba akae kando CUF imeyumba sana

Wewe ndiyo kituko kweli kweli wakati Lipumba yupo CUF ilikuwa na wabunge wangapi huku bara na baada kuisaliti CUF imepata wabunge wangapi, au kwa vile unajua kugonga gonga key board basi unajiropokea tu, abakie tu huko CCM hatumtaki tena huku.
 
Na mbatia aliyeshiriki kindaki ndaki ndani ya ukawa kaambulia kamoja tu chake mwenyewe
Mbona hamsemi hilo
 
Sasa kwani lowassa kashaondoka ukawa.. Au 2020 tena ataondoka
Anataka kuwa mwenyekiti wa CUF sio UKAWA.
Alipinga Lowassa kuwa mgombea wa UKAWA na sio kuwa mwanachama wa CHADEMA.
Au CHADEMA inataka uchaguzi ujao pia mgombea urais atoke kwao na lazima awe Lowassa???
 
Back
Top Bottom