Maswali 10 kuhusu magaidi wa Amboni, Tanga

Maswali 10 kuhusu magaidi wa Amboni, Tanga

Amalinze

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2012
Posts
6,780
Reaction score
5,325
maswali 10 kuhusu magaidi wa amboni.

samahani kama nitawakwaza wengine lakini binafsi siamini hicho kinachoitwa magaidi wa amboni. Mi naona kama ni sinema tu ambayo serikali (ya ccm) imeamua kuicheza ili kuwahamisha watu kwenye hoja za msingi kama daftari la kudumu la kupiga kura, na katiba mpya.
hebu tujiulize maswali yafuatayo kwa tafakuri pana;

1. Gaidi alijirushaje pangoni na pingu mkononi? Tuliambiwa polisi walimkamata gaidi mmoja na akawapeleka mapango ya amboni kuwaonesha walipoficha silaha. Eti alipofika mapangoni akajirusha ndani. Kivipi alijirusha na alikua na pingu?

2. Na kama hakuwa na pingu, polisi wanapaswa kujieleza kwanini hawakumfunga pingu gaidi? Mtu mnamshuku kuwa gaidi mnambeba kama bwana harusi? Huyu alitakiwa pingu za mikono na miguu. Au pingu zipo kwa wafuasi wa ukawa wanapoandamana?

3. Kwanini askari wamezuia waandishi kufika eneo la tukio kupiga picha na kuchukua matukio? Wanahofia nini? Waandishi wa kenya wanaingia hadi somalia "kulipo kitovu cha ugaidi" na wanacover story, wakati mwingine wanafanya interview na viongozi wa al-shabab, sembuse hawa vibarua wa amboni? Kwanini polisi wanazuia waandishi?

4. Kwanini polisi wanavujisha rekodi zao za sauti kuhusu hawa waitwao "magaidi wa amboni?". Juzi nilisikiliza clip moja ya sauti kati ya mtu aliyejiita polisi akiongea kwa simu na askari mwenzie aliyeko tanga akimueleza juu ya magaidi hao. Jana imevuja clip nyingine ya askari polisi wakiongea kwa simu juu ya mikakati waliyonayo kuwamaliza hao magaidi. Hivi inaingia akilini mikakati kupangwa kwenye simu? Hakuna radio call? Na hata kama ni simu kwanini wavujishe? Hivi hawaoni kuvujisha ni kuuza ramani kwa adui? Mi naona huu ni usanii tu.

5. Kwanini askari aliyeuawa hajatajwa jina wala waliojeruhiwa? Wanaficha nini? Luteni rajabu mlima alipofia vitani huko drc vyombo vya habari viliripoti na akatajwa majina yake kamili. Baadae akaja kuzikwa kwa heshima kama shujaa aliyefia kwny mapambanno. Vp huyu aliyefia amboni mbona hatajwi? Tunaambia tu, askari mmoja amepoteza maisha. Nani huyo? Kama mnaweza kuwataja wanaofia vitani nje ya nchi huyu wa amboni vp??

6. Hao magaidi wameingia lini huko mapangoni? Na walikua wakifanya nini huko muda wote, mbona hawakuwahi kufanya uhalifu wowote hadi askari walipowatibua?

7. Hao magaidi wanakula nini siku zote huko mapangoni? Au ndio kusema kwenye mapango ya amboni kuna shopping centre kama 'mlimani city?'

8. Halafu mapango ya amboni yanasimamiwa na mamlaka ya makumbusho ya taifa. So kuna watumishi ambao wapo kule mapangoni kila siku. Kuna wahifadhi, kuna walinzi, kuna mkuu wa makumbusho na watumishi wengine. Hivi hawa watu hawakuweza kugundua magaidi walioingia? Au labda wakati magaidi wanaingia watumishi wote walikua likizo?

9. Kwanini chagonja na igp wanapingana hadharani? Voa jana wamemnukuu igp mangu akisema askari aliyekufa alikuwa ktk mapambano na magaidi. Lakini chagonja jana kaongea na media na kusema askari aliyekufa alipigwa ambush. Yani wakati wamemkamata adui wanampeleka huko mapangoni akawaoneshe silaha zilipo; ile kufika tu wakiwa hawajui hili wala lile wakashambuliwa na risasi kutoka mapangoni hivyo mmoja kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa. Sasa hapa tumuamini nani kati ya mangu na chagonja?

10. Taarifa za kusikitisha zilizotolewa na jeshi la polisi leo ni kuwa eti baadhi ya magaidi hao wamekamatwa na wengine wametoroka. Tehtehteh kweli hii sinema aliyeandika script atakua cha-gonja maana huyu jamaa ni hopeless kabisa. Wametorokaje? Wamepita wapi? Askari wetu wakiwa wapi? Au kuna barabara huko ndani ya mapango zinapita hadi somalia?

nashauri polisi wajipange upya wanapotunga sinema zao za kujaribu kuwahamisha watanzania kwenye mijadala muhimu. Na wakitaka sinema yao iaminike na watanzania, wamtafute mtu mwenye akili sana awaandikie script, sio kumpa 'kichaa-gonja'

i rest my case.. J.pili njema.


Malisa G.J || your partner in critical thinking.!
 
Huu mchezo wa CCM kuwatishia wananchi wanaogope kwenda kujiandikisha .Haiwezekani waandishi wa habari wazuiwe kufika eneo la tukio wanaficha nini sasa mpaka majeruhi wamewakataza kwenda kuwaona.

Wanaficha nini hizi ni mbinu chafu za CCM kuwaogopesha wananchi na kukataza maandamano au mikutano ya upinzani kwa sababu za ugaidi lakini ukweli utabaki kuwa ukweli hakuna ugaidi wowote nchini.
 
1. Gaidi alijirushaje pangoni na pingu mkononi? Tuliambiwa polisi walimkamata gaidi mmoja na akawapeleka mapango ya amboni kuwaonesha walipoficha silaha. Eti alipofika mapangoni akajirusha ndani. Kivipi alijirusha na alikua na pingu?

Nakumbuka yule gaidi wa Arusha alivyotoloka on the spot alipigwa risasi fasta na pingu yake ila huyu gaidi wa amboni aliruka akaingia kwenye pango.
 
Possibly kwa maana hakuna jina la askri wa Jw aliyeuwawa tunambiwa tu askari mwenye cheo cha Sgt. Na je kwa nini waandishi wa habari wasitoe covarage ya tukiozima kwa maana jana kwenye taarifa ya saa mbili ya ITv tulimsikia FFU yule akimfokea mpiga picha ali asiendelee kurecord tukio ili lenye utata.

Je, magaidi walikuwepo huko Tanga ?? au Ndo sarakasi za Kutuweka roho juu wakati tunapokuwa tunaelekea kwenye Chaguzi na Mshemishe zinazokuja muda si mrefu.
 
Upinzani msikubali upuuzi huo, ni janja ya CCM kuwatisha wananchi kuwa wapinzani watapoteza amani. Subiri, upinzani utahusishwa, just wait and see!
 
Huu usanii wa polisiccm ni wa kipumbavu sna.Kilichonishangaza mm ni waandishi wa hbr kuchukua picha za tukio.Hata kule hospitali walipopelekwa majeruhi hawakuruhusiwa kwenda kuchukua picha na kuhoji majeruhi:
Huenda kuna mawili;

1.Labda ni usanii tu wa polisi kujifanya kuna ugaidi kwa malengo yao wanayoyafahamu ikiwa ni pamoja na kuwahamisha wananchi kwenye issue muhimu kama katiba,kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ,kuzuia mihadhara na maandamano ya upinzani,n.k.Hivyo basi Amboni walikuwa wanalipua mabomu tu kuaminisha wananchi,na hapakuwa na magaidi ndo maana waandishi walikatazwa kwenda huko.

2.Huenda magaidi walikuwepo wakawachakaza askari wetu na kujeruhi idadi kubwa ambayo wameamua kuweka siri na kutoa idadi ndogo kwenye vyombo vya hbr,ndo maana waandishi walikatazwa kwenda hata hospitali kuwajulia hali pamoja na kuwahoji.

N.B.Polisi mmechemka,tafuteni issue nyingine tena mjipange vzr kuja kudanganya wananchi.Acheni kutumika kisiasa!
 
Acheni kujifanya mnajua sana, acheni ongea vitu hamna uhakika navyo.
Sasa tofauti ya ambush na wakiwa kwenye mapambano na magaidi ni nini.
 
Mimi hata sielewi , ila napatwa na wasiwasi sana. Na vipi kwa nn wasitumie mbinu ingine wakaamua kutumia ndugu zetu waislam???
 
Nipo jirani na eneo la tukio, mimi ni raia tu.Askari wa JWTZ aliyekufa namjua vizuri ni msambaa wa maeneo ya Korogwe Bungu kwa jina ni Kajembe.

Tukio halikutokea ndani ya mapango ya Amboni bali ni pembeni kidogo,kwa wenyeji wa Amboni wataungana nami Kuwa ardhi ya Amboni imetawaliwa na mwamba chokaa hivyo yapo mapango mengi zaidi ya mjuavyo japo yanayotumika kwa utalii ni 2 tu kati ya 70, haya 68 bado hayajafanyiwa utafiti.

Kufika maeneo ya tukio:

Ukitokea Tanga Mjini kuelekea Horohoro kwenye barabara kuu Mara tu uvukapo daraja la mto Zigi mbele kidogo kulia kuna kijimlima wakati chini ya kijimlima ni mapango.
 
CCM wana hali mbaya,Sasa naona griini gad wameamua kujifanya magaidi wenye misimamo mikali ya kidini.
Tutawateketeza wote we endeleeni tu.
 
maswali 10 kuhusu magaidi wa amboni.
Amalinze umenisononesha mno kwa pumba ulizoandika.

Maswali yako kumi hayana mashiko hata kwa ndururu. Ati gaidi alijirushaje pangoni!! Kumbuka magaidi wanayo mafunzo ya kijeshi na wanajua namna ya kutoroka na kujificha. Ndiyo alifungwa pingu na ndiyo alijirusha pangoni kwa sababu anayajua vyema mapango hayo na alijua akijirusha ndani hakuna atakayethubutu kumfuata.

Hata hivyo umejichanganya mwishoni kuhusu kuuawa kwa askari mmoja, hutaki kukubali kuwa walipokuwa mle mapangoni walikuwa na ulinzi wa doria vilevile na waliposhtukizwa na polisi wakawahi kufyatua risasi ikampata askari mmoja na ikampa nafasi mwenzao ajirushe na kukimbia hata kama alifungwa pingu za miguu bado angeweza ku-sommersault na kwenda mapangoni ambapo wenzake wangekata pingu hizo kwa risasi.

Swali kwamba walikuja lini humo mapangoni, ungewauliza wao wenyewe kwani hawakutoa taarifa walipokuja.

Swali kwamba mapango yako katika hifadhi, ni kweli ila sio yote ni mawili tu yanayotumiwa sana na watalii na ndio maana wao walijua wakijificha kwenye mapango mengine hawataonekana.

Swali kwamba walikuwa wanakula nini, hilo ni swali la kitoto kabisa kwani wana uwezo wa kumtuma mmojawao akaenda marikiti akanunua maankuli ya mwezi mzima akakodi pickup mpaka kijiji cha jirani akashusha mzigo ukawa unakuja kubebwa kwa kichwa na mamluki ambao ni raia wenzetu kuwapelekea huko mapangoni.

Mimi nakushauri tu kuwa uwe unatafakari kabla ya kukurupuka kwani ugaidi ni janga la kitaifa na likifika kwako ndio utajua kweli ni janga hivyo usilete mambo ya kitoto kuita eti senema.

Tengeneza wewe script yako uandae senema yako ya dizaini hiyo ndio tuamini kuwa na hii nayo ni senema lakini ukiwafufua na kuwaponyesha wale waliokufa na kujeruhiwa maana kwenye senema sterling hauawi.
 
Last edited by a moderator:
Tatemahunda

Shukrani mkuu kwa taarifa,Marehemu anaitwa Kajembe tu hana Initials au Surname? Maswali yapo kumi umejibu swali moja tena nusu jibu alijakamilika? Anitwa kajembe nani? Namba yake ya JWTZ,Majina ya Majeruhi pia?
 
Last edited by a moderator:
maswali 10 kuhusu magaidi wa amboni.

Kama Mtanzania Mohamed Ghailani asingetiwa hatiani na Mahakama ya Marekani kwa Ugaidi,Kama Mapadre wasingeuawa Zanzibar,Kama Makanisa yasingechomwa Mbagala,Kama Mchungaji asingechinjwa Geita,Kama Kanisa Katoliki Olasiti lisingerushiwa Bomu mbele ya Balozi wa Vatican,Kama Mkutano wa CHADEMA huko Arusha usingerushiwa Bomu,Kama vituo vya Polisi visingevamiwa,Ningekuwa wa kwanza kusema hii ni Janja ya CCM.Tofauti na hapo naona ni Janja ya baadhi ya watu kupumbaza vyombo vya Dola ili Ndugu zetu katika Imani wasikamatwe.
 
Hivi aliyekufa ni askari wa akina chagonja au JWTZ? jana Clouds wamesema ni wa JWTZ.
 
laiza

#. Mkuu Shukrani kwa taarifa,umejibu swali moja tu kati ya hayo 10 na jibu lako hayajitoshelezi kabisa.

Unakumbuka gaidi wa Arusha alivyojaribu kutoroka? Unakumbuka Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya alivyojaribu kutoroka Kisutu mahakamani?

Wote hao walithibitiwa na kuuawa inakuwaje gaidi huyo aliyeteka silaha kwenye vituo vya polisi atoroke kirahisi tena mbele ya trained police?

Kwa mujibu wa taarifa ya Chagonja aliyeuawa ni askari JWTZ sasa ilo ambushi wakati linatokea si walikuwa maaskari polisi peke yao tu? Hao wanajeshi si walikuja hawamu nyingine,mbona kuna contradictions?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom