Heshima kwenu wana Jf.
Mimi ni kijana ambaye nimetoka familia ya kipato cha kati yani tutachelewa kula lkn hatuwezi kulala njaa. Ni msichana wa miaka 23 mpaka sasa. Sina mali zaidi ya shamba la nyumbani na vitu vya gheto yani kitanda, godoro, jiko, redio, n.k.
Nimeingia chuoni mwaka 2017, nilikuwa na malengo ya kupata mwanga nikiwa nipo masomoni lakini tuseme niliangukia pua. Nikiwa mwaka wa kwanza nilijiingiza ktk kilimo cha mahindi japo nilitumia resources za nyumbani lkn bado nilikula mweleka. Kulima nililimia ng'ombe za nyumbani na shamba lilikuwa la nymbani. Mi nilinunua tu mbegu mbolea na kukudi vibarua wa kupalilia na kuweka mbolea kuvuna nilivuna mwenyewe. Lakini sikupata mazao kama ambavyo nilitarajia kwani nilichelewa msimu.
Mwaka wa Pili, nikasema sasa sihusishi na kitu chochote zaidi ya kuweka savings ktk pesa yangu ya boom. Aisee ktk hili nashukuru sana Mungu kwani pamoja na kulipa Kodi ya nyumba, ada, na chakula lkn nilifanikiwa kuweka savings ya Tsh 680,000. Nikaenda field nilipo rudi mwaka 3 nikaamua kuanzisha tena goli la kuuza mitumba ya viatu. Nilienda na jamaa angu pale soko la Memorial Moshi nikachukua mzigo wa 500,000 nikakodi meza soko fulani hivi hapa Arusha nilikuwa nalipia 25,000 kwa mwezi. Nikauza kweli nilipata changamoto mwanzoni lkn nilianza kuzoea na maisha yalianza kuendelea vzr. Lkn mbuzi wa masikini hazai na akizaa anazaa dume hilo soko liliungua mwezi machi na katika ya waathirika wa ajari hiyo na mimi nilikuwepo.
Ikumbukwe kipindi hicho tulikuwa tumeangezewa likizo ya CORONA sema kweli nilichanganyikiwa sana. Ila nashukuru Marafiki na familia yangu walikuwa karibu na mimi mpaka nikazoea. Niliamua kwenda nyumbani mkoani Mwanza ili niangaliye maisha mengine. Nilienda nikaanza kufanya biashara ya uchuuzi wa dagaa pale mwalo wa Kayenze ndogo wenyeji wa Mwanza wanapajua vzr. Nilipiga miezi 2 kweli maisha yalienda hata likizo sikuijutia sana.
Matarajio yangu: kwa vile nimebakiza takribani wiki 11 kumaliza chuo nimejipanga kama ifuatavyo nimefanikiwa kukusanya 375,000 mpaka saiv nikiongezea na boom lijalo inaweza kufika 625,000 baada ya kutoa hela ya kumalzia ada na pesa ya chakula kwa muda wa wiki 5. Hiyo pesa nitaenda kuanzia biashara ya kuku huku mkoani Mwanza kuku nakuwa nawatoa mkoa wa Simiyu. Karibu kwa Ushauri na maoni
Nawasilisha