Maswa: Silvester Kasulumbayi arejea CHADEMA

Duh kanikumbusha mbali sana jinsi Chadema illiteka Shinyanga nzima. Kuna Sylvester Kasulumbay, Meshack Opulukwa, Shibuda na Professor Kuliyokela Kahigi!

Aisee hiyo roster ilikua si mchezo. Pale Shinyanga mjini tulishinda wakaiba, tukaenda mahakamani wakamuua mgombea wetu otherwise tungebeba mkoa mzima!!

Naona moto ule ukirejea 2025
 
HUYU HAFAI, KESHO ATAHAMA TENA FURSA ZIKIPATIKANA KWINGINE. HANA ANALOLIPIGANIA ISIPOKUWA TUMBO LAKE. ANAONA SAA KUNA UWEZEKANO MKUBWA CHADEMA IKASHINDA CHAGUZI NA NAFASI NYINGI,HIVYO ANAVIZIA FURSA
Uko sahihi kabisa, ilitakiwa hawa wapigania tumbo wapokelewe bila kupewa Airtime kubwa, na wasipewe nafasi yoyote ya kugombea hadi ipite miaka 7.

Hawa wachumia tumbo wamechangia sana kuvunja moyo wafuasi wa upinzani kwa kutangatanga kwao. Mtu asiye na msimamo au uvumilivu, ni wa kumpiga kushoto abaki anashangaa.
 
Wapokelewa kimya kimya..na kama ulivyosema wasipewwe nafasi yoyote mpaka say miaka 5. Unapina nia yao kwanza kabla ya kuwaamini
 
Tunawalaumu Bure tu ila hakuna ambaye angebaki upinzani kwa ukatili ule ulikua unafanyika.

Huku napoishi wadhamini wa Chadema walinyooshwa uwe una hardware inapigwa fine Kila kukicha, aliyekua na hoteli naye figisu zikaanza, aliyekua na kampuni ya ulinzi naye akapigwa biti na kunyimwa tenda. Mkuu CCM ni zaidi ya mashetani so ukiwa upinzani ni zaidi ya kujitoa kafara tu.

Lakini kwa kuwa ameshaondoka nadhani ni wakati wa kuongeza nguvu kumsulubu CCM hiyo 2025. Hakuna wakati ushindi uko karibu zaidi ya 2025 maana ni wadhaifu kuliko wakati wowote ule.
 
Kabisa, sio mtu anapokelewa leo, kisha ndani ya muda mfupi anataja nafasi ya uongozi, akinyimwa nafasi anaanza nongwa, na hata akichaguliwa inakuwa rahisi kushawishika, maana price tag yake tayari wanaifahamu.
 
Tunawalaumu Bure tu ila hakuna ambaye angebaki upinzani kwa ukatili ule ulikua unafanyika.

Huku napoishi wadhamini wa Chadema walinyooshwa uwe una hardware inapigwa fine Kila kukicha, aliyekua na hoteli naye figisu zikaanza, aliyekua na kampuni ya ulinzi naye akapigwa biti na kunyimwa tenda. Mkuu CCM ni zaidi ya mashetani so ukiwa upinzani ni zaidi ya kujitoa kafara tu.

Lakini kwa kuwa ameshaondoka nadhani ni wakati wa kuongeza nguvu kumsulubu CCM hiyo 2025. Hakuna wakati ushindi uko karibu zaidi ya 2025 maana ni wadhaifu kuliko wakati wowote ule.

Hatukatai hao waliohama kutokana na kufanyiwa figisu, maadamu mazingira ya figisu bado yako, na wao hawawezi kuvumilia figisu, isitokee wakapewa nafasi za uongozi, bali wabaki wahamasishaji tu. Hao ndio kama akina Kambaya, wanaingia kwenye chama ili kupata nafasi ya madaraka, wakikosa wanaondoka. Kisha wakishaondoka wanaishia kukipaka chama matope kwa propaganda sijui chama kina wenyewe ambao ni watu wa kaskazini.

Tusirudie makosa, aliyeondoka kwa kushindwa kuhimili uhayawani, arudi na apokelewe, lakini sio nafasi ya uongozi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom