Masudi Kipanya akemewe kabla hajaleta machafuko kama Lars Vilks

happyxxx

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
568
1,847
Lars Vilks ni mchora katuni maarufu ambaye aliingiza dunia kwenye machafuko mpaka kutokea vifo na migogoro mikubwa baada ya kuchora katuni ya kumkashifu Mtume Muhammad SAW. Cartoonist huyu ambaye kwa sasa ni marehemu alifikia hapo baada ya kunyamaziwa kwa muda mrefu akaona anayo haki ya kuchora chochote na kudhalilisha yoyote kwa mgongo wa uhuru wa habari.

Hiki ndio ameanza kukifanya Masudi Kipanya anaetumia katuni zake kushambulia kabila la WASUKUMA. Tumkemee sasa kabla hajaamsha hisia za ukabila ambazo zinaenezwa sasa na wanasiasa wa Chadema na wachache ndani ya CCM. Mashambulizi dhidi ya kabila fulani hayapaswi kushabikiwa na mtu yoyote yule kwa maana kuna ku-fight back hapo ndio uja machafuko au kugawana fito.

Sukuma gang = Wasukuma

20230328_090538.jpg
 
Sasa unaanzaje kufananisha kukashifiwa mtume wa Mungu na hicho kikundi ulichokitaja?
Huyo mtume kwanza alishakufa na hata angekuwa hai sio ndugu yetu yule na hata yule mwarabu akikashifiwa haitudhuru chochote sisi wamatumbi , ila sisi kukashfiana sisi kwa sisi inachochea ukabila na ni sumu.mbaya sana
 
Mtoa mada wewe ni mgonjwa. Maana ya Sukuma Gang imefafsnuliwa mara kadhaa humu humu na ikaeleweka. Kwani Kabudi ni Msukuma, vipi Lukuvi na Bashiri.
Sukuma ni kabila. Nahitaji nani anifafanulie kuwa sukuma ni kabila au la?
 
Hata kama angeandika sukuma gang, bado haiwezi kuwa sababu ya kuleta machafuko. Ni mtazamo tu wa mtu.
Masoud ana akili sana au kama ni mtu mwingine anampa wazo la kuchora, basi wanapaswa kupewa tuzo
Ila akiandikwa mchaga ni tatizo?
 
Back
Top Bottom