Masuala mazito yote tuletewe wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masuala mazito yote tuletewe wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MrFroasty, Jan 29, 2010.

 1. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35

  Masuala mazito yote tuletewe wananchi


  Kwa kweli sijuwi kama Msekwa, Makamba na vibaraka vyao wamezidiwa na uzee?Mimi napenda kuamini kama msimamo unaendelea sasa hivi Barazani kutoka kwa ndugu zetu wa CCM, ni msimamo uliokuja kusisitizwa au kutisha wana CCM hapo Zanzibar katika kikao cha Jumapili iliyopita na kuzua msimamo wa kura ya maoni.

  Kwanini kura ya moani?CCM Zanzibar (Mkema, Samia) wametumwa waje watwambie kama kila kitu ni lazima kifuate agizo la Butiama.Kama akili zenu zimedumaa na kuwafanyeni mukawa watumwa wa Bara, basi hilo ni tatizo la kiakili na kiafya linaloendelea kuwasibu na itatubidi tuwaombeeni dua mupate afya njema.Maana katika akili zangu mie hoja ya kura ya maoni, haina mshiko.Na ni matumaini yangu kila mwanaadamu na mpenda amani atakubaliana na mimi kuwa matatizo ya migogoro ya uchaguzi hayawezi kutatuliwa na uchaguzi.

  Hapa sina maana ya kudharau kazi inayofanywa na ZEC, bali uhalisia wa hili tatizo ni kuwa ZEC ni sehemu moja ya huo mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.Hili nina hakika kuwa munalifahamu, sasa kwa vile mmeshindwa kutueleza hoja za kung’ang’ania kura ya maoni.Mimi naomba kutoa masharti au maoni yangu juu ya hii kura itakavyofanyika.Natoa masharti nikijua wazi kuwa mutapinga kwa nguvu zote, kwani malengo yenu ya kukimbilia kwenye kura ya maoni yashafahamika katika jamii ya kizanzibari.Tuna uwezo kuzichambua hizo siasa zenu za kijima zinalenga nini na munataka kutupeleka wapi.Lakini tunaonya kwa maandishi yetu kuwa sisi hatutorudi gizani na kuingia mitafaruku ya wenyewe kwa wenyewe.

  Ni imani yangu kuwa wengi wanaoshadidia kura ya maoni watakuwa na sehemu nyengine ya kwenda kuishi, na hivyo hawajali au Amani ya visiwani Zanzibar haina thamani kwao kwa vile wanazo sehemu za kwenda kukimbilia.Sisi wazanzibari hatuna sehemu nyengine, visiwa hivyo ndio sehemu pekee duniani ambayo tunaweza kujiskia kama ndio makwetu.Baada ya kuonesha kama hatuna pa kukimbilia, basi mujue kama hatutokubali kuharibiwa mazingira yetu ya kuishi kwa utashi wenu wa madaraka.Tushasubiri vya kutosha, na ustahamilivu wetu mushauchezea hadi sasa ile mbivu tunayosubiria iko njiani kuharibika.

  Kwa vile wana CCM Zanzibar mlipewa ujumbe na vitisho muthamini Butiama na kutupilia mbali Zanzibar na maslahi ya watu wake.Nami nitatoa mashari ya utekelezaji wa kura hiyo:

  Masharti ya kutekeleza kura ya maoni:

  * Msimamizi wa kura hiyo awe kutoka nje ya Tanzania, ikiwezekana Umoja wa Mataifa.
  * Kutokana na hoja ya wana CCM kudai kuwa hili suala la GNU ni zito, na hivyo hawawezi kulitolea maamuzi.Basi kuanzia sasa masuala mazito yote yaletwe kwetu wananchi tuyatolee maamuzi kwa vile kazi imekushindeni humo Barazani.Nitatoa orodha ndogo ya masuala ambayo itawabidi SMZ mutuletee wenyewe wananchi tuyatolee maamuzi

  1. Muungano na mfumo wake upelekwe kwa wananchi ukafanyiwe maamuzi kama wanataka Muungano, na kama hawataki watoe maamuzi ni mfumo gani wa serekali wanaopendelea.
  2. Wananchi pia tupewe fursa ya kuyajadili masuala mazito kama passport kwa wageni kuingia Zanzibar.
  3. Nafasi ya rais wetu wa Zanzibar katika serekali ya muungano (mara baada ya kukubaliwa muungano wenyewe)
  4. Na mjadala mzima wa kitu gani kiwe chini ya muungano na kipi kitolewe .

  Sisi huku Zanzibar tutafurahi sana kama na hili agizo la Butiama, kama halitokuwa tuu ni kuhusiana na GNU bali pia itabidi maswala mazito yote niliorodhesha hapo juu tuletewe wenyewe wananchi tutie baraka zetu.Kama agizo la Butiama litaweza kufanya hivi basi naona inabidi lienziwe kweli kweli….

  GR

  Mrfroasty
   
 2. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MrFrosty,
  Sijui ni nani alikwambia kuwa CCM Zenji walipewa vitisho, hebu tupe ushahidi.

  Kama wewe huutaki muungano kwa sababu zako binafsi, hiyo ni haki yako. Hata hivyo kumbuka kuwa 'You are a single entity', wako wengi wanaouombea muungano udumu.

  Muungano una karibu miaka 50, kwa hiyo hauwezi kuburuzwa kaburini kwa vile tu MrFrosty hautaki.

  Ndio kuna kasoro katika Muungano zinazohitaji kutatuliwa, lakini hatuhitaji wakoloni kutusimamia katika kutatua. Miaka 50 ya ndoa inayo uwezo wa kutatua mengi hata kama ni jinsi ya kugawa siku za kulala nyumba ndogo na kwa bi mkubwa.

  Yakhee, tukiua muungano, sio ajabu utafuatia wa Pemba na Unguja, halafu Mkoani na Wete n.k, n.k, kisa kila mtu ana vijisababu vyake. Hivi tutafika mwarabu wangu kwa tabia hii ya kukimbia au kutunga matatizo?

  Usisahau karibu Konde yote ni ya wasukuma na wanyamwezi wa Tabora, utawafukuzia bara ili ubaki na washirazi? Tuache utoto wa kulia lia nyau tutatue matatizo ya Muungano wetu. Hata Mwani huota unapowekewa vigingi licha ya mawimbi ya bahari.
   
 3. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mara baada ya kikao cha jumapili, kiongozi mmoja wa CCM:
  “Wajumbe wote wa CCM katika Baraza la wawakilishi wanapaswa kutetea na kulinda azimio la Butiama, na atakayekwenda kinyume ataadhibiwa,” alisema Vuai.

  Who told you that I am the only against this evil union?...if you think I am just a single entity, think again.

  Muungano una karibu miaka 50, lakini kama wewe unajua kuchora graph ya development against time...basi utaona kama maendeleo ya Zanzibar yamezorota au kukwama au kuanza kuchukua -ve slope...right after the union.

  Kwanini unataka kupoteza rasili mali za wanyonge kutatua na complicate maisha...wakati kitu simple hizi nchi zetu ni masikini hazihitaji kuwapotezea nguvu wananchi kwa kufikiria jinsi ya kutatutua complexity ya muungano....suluhisho ni kuvunja.

  Hizi ni theory za Nyerere kuwa muungano ukivunjika, basi Pemba na Unguja zitaparaganyika.Muungano una miaka 50, wakati taifa la Zanzibar lipo miaka mingapi?...sasa usiwe kama kasuku kurudia maneno ambayo usiyo weza kuyatetea.Mwache Nyerere aseme maneno haya, lakini sio wewe.Nina uhakika Nyerere alikuwa na sababu nzuri za kutuletea ujamaa, na wala huwezi kumshinda kwa hoja...lakini hoja ujamaa na sera za Nyerere=umasikini.

  Ushawahi kufika Pemba lakini?Au umesoma kwenye hotuba za Nyerere?
   
 4. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbe hivyo ndio Vitisho tena toka kwa Mzanzibari? Au ni kwa vile maazimio yalifikiwa Butiama?

  Yaah! This evil union brought you to where you are.

  Chora pia graph ya bei ya karafuu utamjua mchawi wa hayo maendeleo unayoyalilia. Utegemezi wa karafuu halikuwa wazo la Nyerere.


  Ningekushauri utoe sababu zako halisi za kuupinga Muungano ili nia yako ieleweke. Usizifiche, otherwise zip it up na utuachie tuendelee kuulea na kuudumisha Muungano wetu.  Uvunje wewe Muungano uliyeuona leo. Kama nilivyokuambia, mawazo yako ni yako usijifanye kuwa unawakilisha kundi chochote.  Tell it to the USSR, Yugoslavia n.k. Wale wote waliokufa kulinda miungano yao, leo hii ndio wanaotawala dunia. Waliovunja yao sasa wanategemea wengine. Achana na ufinyu wa mawazo.


  Nikuulize wewe kama umefika Pemba unayetaka kuuvunja Muungano wetu tokea kwenye ka-Laptop kako. Usifikiri ni wewe tu ndie mwenye kumiliki uZanzibari.

  Wasalaam,
  Mkulima wa Mwani,
  Vumba, Pemba, Tanzania
   
 5. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35


  Hapo nilipopiga bold, unaonesha wazi wewe ni copy paste ya Nyerere with a bit of dictatorship mind....

  Mimi nilichokifanya nimetumia haki yangu ya kutoa maoni.Lakini mwenzangu unaonekana umekerwa sana na kuwa mimi sipendelei muungano.Samahani sana kwa hilo, lakini hii haiwezi kunisaidia kubadili msimamo wangu.

  Mimi nitaendelea kudai haki yangu ambayo imetekwa na Nyerere ya kuniondoshea utaifa wangu na kunibandika kikofia cha kimasai (i.e kitanzania) hadi nitaingia kaburini au kutatokea marekebisho.Wewe kama utasusa fanya hivyo...

  Sasa mimi nikupe sababu za kupinga muungano wakati mwenyewe tayari umekubali kama muungano una matatizo?

  Mimi sitaki sitaki na wala sijiskii peace kuitwa mtanzania, nataka niitwe mzanzibari na nijulikane kama ni mzanzibari....thats what feels right and natural to me, whats so hard for you to understand that?
   
 6. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mtanzania halisi MrFrosty,
  Wewe ni Mtanzania ukijishaua na Uzenji sio vibaya. Ni sawa na mtoto mdogo anapovaa viatu vya mama yake ingawa yeye ni mvulana. Hawezi kubadilishwa na viatu. Kwa hiyo na wewe jishaue tu unavyotaka lakini ujue kuwa wewe ni Mtanzania.

  Inavyoelekea ni kuwa wewe huna sababu za kuupinga Muungano na umeishiwa na hoja bali una kelele nyingi tu na ndio maana nikakwambia kuwa kama huna point ya kupingia Muungano, basi Zip it, maana ndoa ya miaka 50 haiwezi kuvunjwa kwa kelele za watoto.

  Defend your position if you can, otherwise accept your true identity ya uTanzania na ukae kimyaa kama unayenyolewa.

  Ukitaka kujishaua na kujiita Mzanzibari, rukhsa, sawa na Muha akijiita Mkigoma, lakini wote tutabakia waTZ.

  Zaidi ya yote, asilimia kubwa ya waliopo Zenji wana asili ya bara. Wachache waliobaki ni wa ngazija na wengine wamechangia damu na waarabu na waajemi. Sijui wewe mwenzangu ni wa kundi lipi lakini hawa mashombe ndio wengi wenye kuusagia muungano kwa sababu wazijuazo wenyewe. Au unabisha mwarabu wangu?

  Sasa hebu tetea hoja yako ya kuvunja muungano kama ulivyouita the 'evil union' ila kama huna hoja basi tuuache muungano wetu urekebishwe na kunawiri.
   
 7. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sasa unataka kujadili hoja au unataka kujua asili yangu halafu ndio uanze na mifano yako ya kutusi watu kwa kufananisha muungano ni sawa na ndoa...halafu sisi ndio majike na nyie ndio madume.

  Hizi ndio hoja zako ambazo ndio unajisikia kuwa una hoja...hizi haziitwi hoja ni matusi kufananisha wanaume kuwa wameolewa.

  Mimi nishakutana na watu humu JF wenye hoja...lakini wewe humo na wala hujuwi historia wala hiyo Zanzibar huifahamu.Hiyo inathibitika hapo unaposema kuwa wazanzibari wengi asili yao ni kutoka nje ya Zanzibar.Hii statement inanipa ushahidi tosha kuwa hujuwi unachokizungumza...na wala sina haja ya kupoteza muda wangu.

  Kila la kheri...ukumbi wako nitaendelea kuchangia nikiona wanaume waliokuwa hawajaolewa wakitoa hoja za msingi za kutetea au kuvunja muungano.
   
 8. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  This is really heart breaking for a man to come with this homophobic examples in front of real men. :confused:
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  Mrfroast nimefurahi kukuona humu JF.mimi sio mzanzibari ni mtanganyika,umekuja na hoja nzuri sana hapa. kwanza ningependa kuwapongeza wanzazibari kwa kujitambua kuwa wao sio CUF wala CCM,Mola awabariki sana na nina hakika atawasaidieni mpate HAKI yenu.kwanza baada ya nyinyi kujitambua mmeokoa maisha ya watu wengi sana na usumbufu ambao ungeweza kutokea baada ya uchaguzi.kila mtu anajua kuwa CCM hawana uwezo wa kushinda tena Zanzibar hata wenyewe wanalijua hilo.nikirudi kwenye muungano sioni faida yoyote ninayoipata mm kama Mtanganyika kutoka kwenu huko Zanzibar.wenye matatizo na wanaoutaka huo muungano inabidi watueleze siri yake.but my take ni kuwa muungano ufe.
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  Big up Mzalendo.net na JF;
  Nakumbuka hotuba moja ya Mwalimu alisema kuwa dhambi ya kuvunja muungano itaanza kufanya kazi hapohapo.In my side napingana naye kwa nguvu zote, hizo zilikuwa ni fikra zake tu na zimeshapitwa na wakati,ok. kwani ujamaa uko wapi sasa hivi?? ulishakufa.mimi naona ule wakati wa ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI umeshapitwa na wakati. inabidi sasa hivi tuendane na wakati fikra za elimu ya mkoloni hatuzitaki.MR FROAST listern ukimuuliza mtanganyika yeyote akuambie faida ya muungano ataishia kukuambia tu kuwa watanganyika wamefunga ndoa na nyinyi(wazanzibar) wamewaoa and nothing else i think umeshapata hilo jibu juu hapo.sasa let say aliyekujibu hivyo ni msomi na huwezi jua labda yupo hata serikalini(KIGOGO)ok, let say nenda mjini pale kariakoo muulize kijana yoyote muungano wetu una faida gani au ni nini,huyu atakachokujibu nina hakika utalia hata kutoa machozi.
  "aluta kontinua hadi muungano ufe"
   
 11. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwanza naomba kueka sawa baadhi ya vitu ambavyo vimeibuka na kuonesha hisia kali juu ya muungano.Wakati nachapa hii thread, lengo langu ni kujibu hoja ya CCM ya kura ya maoni kuhusiana na mswada wa GNU ulioko Barazani hapo Zanzibar.

  Na nimeainisha vizuri kuwa hii hoja ya kura za maoni haina mshiko, na nimesema kutaka kuonesha kama haina mshiko mie sitoipinga bali nitaendelea kuitetea kama walivyotaka hao wana CCM kwenye agizo lao la Butiama.

  Na nilijua kama hili chapisho litazua upinzani mkali kutokana na ukweli ni kuwa CCM lengo lao sio kura ya maoni.Hawa jamaa viongozi wao ni wazee wenye mawazo ya mgando.Hivi vijana wa leo wanavyofahamu siasa na kujua haki zao, utaweza kuwadanganya kuwa ati hili suala ni zito...hivo lifanyiwe kura ya maoni?

  Sasa mie nilitaka kuibua hizo hisia na kuonesha udhaifu wa hiyo kura ya moani, ndio nikaiunga mkono kwa kitendawili kikali.Kwanza nikakitegua hapo kwenye msimamizi wa kura....halafu kwa vile hoja ya wazee wetu wa CCM kuwa kila suala zito wao hawawezi kulitekeleza...hivyo wapelekewe wananchi, hivyo na muungano nao ni suala zito halina budi kuletwa kwetu.

  Sasa hapo sijasema kama mimi sitaki au sipendi muungano, nilichotaka lipelekwe kwa wananchi kwa kisingizio hicho cha agizo la Butiama la kutumia uzito.

  Sasa "Kubwajinga" naona hata hukufuhamu hiyo thread...umeanza na personal attacks na kuona mimi nataka kuvunja muungano kwa laptop.Hivi hii dhana umeitoa wapi?Kwani referendum manaake ni kukataa kitu au kuchukua maoni ya walio wengi? :rolleyes:
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,514
  Trophy Points: 280
  Mbaya wenu ni nani? let see wat gonna hapen.
   
Loading...