Eddy Tarimo
Member
- Nov 27, 2016
- 27
- 38
BEN PAUL: Bernad Paul ndilo jina alilopewa na wazazi wake. Huyu ni mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva na nyimbo nyingi anazoimba na uimbaji wake ni mzuri lakini imekuwa ni vigumu kutoboa kimataifa pia kwa Bongo tuzo nazo zimekuwa zikimpitia mbali. Ben Pol ametamba na ngoma kali kama jikubali, unanichora, Sophia na nyingine nyingi.
BARNABA: Barnaba Elias ni mwanamuziki mzuri unaweza kusema anamshinda hata Diamond kiuwezo kwani amefanya kazi kadhaa zikakubalika. Kwanza ni mtunzi wa nyimbo mbalimbali za wasanii wenzake na za kwake mwenyewe. Pili anajua kuimba na tatu anajua kutumia vyombo vya muziki tofauti na wanamuziki wengi ambao wanajua kuimba tu. Barnaba amefanya vizuri kwa nyimbo zake kama Suna, Siri aliofanya na Vannesa Mdee, Wahalade ambayo ilipendwa sana na mashabiki wengi na nyingine nyingi ambapo ameshindwa kufika levo za Diamond wakati anastahili hata kumpita.
BELLE9: Wimbo wa Masogange ndiyo uliomtambulisha kwenye anga la muziki. Abednego Damian ‘Belle 9’ aliutendea haki wimbo huo na nyingine alizowahi kuimba kama shauri zao, listen na nyinginezo lakini ameshindwa kutoboa kimataifa kama walivyo akina Ali Kiba na Diamond wakati ni mwanamuziki mzuri.
RICH MAVOCO: Richard Martin ni jamaa aliyebamba na nyimbo kama pacha wangu, labda niseme, roho yangu na moyo. Ana kipaji lakini amejikuta akififia kadiri siku zinavyosonga mbele. Mwanamuziki huyu hajawahi kufanya kolabo na msanii wa nje ya Bongo na amewahi kusema kwamba hana mpango wa kufanya kazi na wasanii wa kimataifa kwa sababu anaamini atatoka mwenyewe.
MO MUSICMOSHi KATEMI a.k.a Mo Music ni mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye amefanya ngoma kali kama Basi nenda, Simama na Nitazoea. Kiukweli jamaa anajua kuimba na kila anapotoa wimbo unabamba na kuwashika vilivyo mashabiki wake. Mo Music nyota yake imeshindwa kung’aa labda kutokana na kwamba hajaingia moja kwa moja kwenye muziki au la kwani alikuwa masomoni huku akiimba.
Mtaje ambae unahisi anakipaji na nimemsahau apo. .