Mastaa 10 waliofanya upasuaji kutengeneza shepu

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
WANAWAKE wengi wanapenda kuonekana warembo, wenye sura nzuri, maumbo yaliyogawanyika vizuri kiunoni, vifua vizuri na makalio. Kwa bahati mbaya, katika uumbaji wa Mungu huwezi kumpangia namna anavyotaka kukuumba!


Hali hiyo imesababisha mastaa kadhaa, mbele na hata hapa Bongo kulazimika kutafuta njia mbadala ya kuwafanya wawe na maumbo mazuri na kwa wenye nazo, wengi wamelazimika kwenda kufanyiwa upasuaji, iwe ni wa kuongeza au kupunguza ukubwa wa matiti, kuongeza makalio na kadhalika. Wafuatao ni mastaa kumi (10) duniani waliofanya upasuaji wa kutengeneza shepu zao;


  1. KRISS JENNER
Kris+Bruce+Jenner+Arriving+Kim+House+4SALpCxnrkQx.jpg

Huyu ni mama mzazi wa Kim Kardashian na kama ilivyo kwa mwanaye, naye amekuwa akitajwa kwamba amefanya upasuaji wa kurekebisha shepu yake, azidi kuonekana kijana. Mwanamama huyu aliyejipatia umaarufu kupitia Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, amewahi kukiri kufanya upasuaji wa kurekebisha uso wake.


  1. IGGY AZALEA
Iggy_Azalea_for_REVOLVE_embed_2.jpg

Jina halisi anaitwa Amethyst Amelia Kelly, ni staa wa Hip Hop, mzaliwa wa Sydney, Australia. Anatajwa kuwa miongoni mwa mastaa waliowahi kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha shepu zao. Ushahidi wa picha zake za zamani na jinsi alivyobadilika kwa sasa, ni miongoni mwa mambo yanayompa wakati mgumu kukanusha tuhuma kwamba alifanyiwa upasuaji na kuna wakati pia amewahi kukiri kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha matiti yake.


  1. HEIDI MONTAG
heidi-montag-plastic-surgery-breast.jpg

Heidi Pratt, mwimbaji, mbunifu wa mavazi, mwandishi na mtangazaji mwenye makazi yake Colorado, Marekani, naye anaingia kwenye listi hii. Inaelezwa kwamba aliwahi kufanya upasuaji wa kurekebisha uso ambao hata hivyo, haukwenda vizuri na kumsababishia matatizo makubwa ya kiafya.


Amewahi kukaririwa akijutia uamuzi wake wa kufanya upasuaji wa kurekebisha sura akieleza kwamba umemsababishia matatizo makubwa kuliko alivyodhani. Lakini pia, tofauti na mstaa wengine, Heid amewahi kukiri kwamba alifanyiwa upasuaji wa kurekebisha matiti na kukuza makalio.


AMBER ROSE

amber-rose-kanye-28jan16-15.jpg

Mwanadada huyu machachari ambaye amewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na marapa Kanye West na Wiz Khalifa kwa nyakati tofauti, naye anaingia kwenye orodha ya mastaa waliofanya upasuaji wa kurekebisha shepu zao.

Licha ya shepu yake ‘amazing’ kuwa gumzo mara kwa mara, mwenyewe amekuwa akikanusha mara kwa mara kwamba hajawahi kufanyiwa upasuaji wowote na kwamba amekuwa na shepu hiyo kutokana na mabadiliko yaliyomtokea baada ya kuvunja ungo na kufanya sana mazoezi.


BLAC CHYNA

blac-chyna-flaunts-curves-during-photo-shoot-pp-.jpg

Jina lake halisi anaitwa Angela Renée White ingawa wengi wanamfahamu kwa jina la Blac Chyna. Huyu ni mwanamitindo na mjasiriamali kutoka nchini Marekani. Picha za zamani za mwanamitindo huyu, zinamuonesha akiwa na umbo tofauti kabisa na jinsi alivyo sasa ambapo anaonekana kuwa na mvuto zaidi.

Inasadikika kwamba Blac Chyna alifanyiwa upasuaji wa kurekebisha makalio yake na kuyafanya yaonekane makubwa, pamoja na miguu yake. Gumzo likawa kubwa zaidi baada ya kipindi fulani, shepu hiyo kuanza kuporomoka kwa kasi kubwa ambapo daktari mmoja jijini Los Angeles, Marekani alikaririwa na chombo kimoja cha habari akieleza kwamba upasuaji wa Blac Chyna haukufanyika kikamilifu.


  1. COCO AUSTIN
c9482eb38697ff9539b488cd1ab9a993.jpg

Mwanamama huyu mwenye bonge la shepu, ambaye jina lake halisi anaitwa Nicole Natalie Marrow, inadaiwa shepu aliyonayo hakuzaliwa nayo, bali ni matokeo ya kufanyiwa upasuaji wa mara kwa mara wa kurekebisha viungo kadhaa katika mwili wake.


Kazi yake iliyompa umaarufu ni uigizaji, uanamitindo na wakati mwingine, amekuwa akifanya kazi ya udansa. Ni mke wa rapa na mwigizaji maarufu, Ice T na amewahi kukiri hadharani kwamba alifanya upasuaji wa kurekebisha matiti yake ili aonekane kama binti wa miaka 18 ingawa amekuwa akikanusha kufanyiwa upasuaji wa kukuza makalio yake.

NICK MINAJ

nicki-minaj-perform-2015-bet-experience-los-angeles.jpg

Rapa huyu machachari ambaye jina lake halisi anaitwa Onika Tanya Maraj, mbali na muziki pia ni mwanamitindo, mwigizaji na mwandishi wa nyimbo.

Ipo wazi kwamba mwonekano wake umebadilika kwa kiasi kikubwa tangu aanze kupata umaarufu japokuwa mwenyewe amekuwa akikanusha kufanyiwa upasuaji wa kukuza matiti na makalio, vyombo vya habari nchini Marekani vimekuwa vikimuandama mara kwa mara. Pamoja na kwamba amekuwa akikanusha, lakini amewahi kukaririwa akisema anafurahi jinsi watu wanavyoshoboka na shepu yake, hasa wanaume ambao mwenyewe amekiri kwamba huwa wanafurahia kumtazama makalio yake.

KHLOÉ KARDASHIAN

k5.png

Huyu ni mdogo wa Kim Kardashian ambaye amepata umaarufu mkubwa kupitia Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians. Pia ni mwanamitindo mkubwa na mfanyabiashara., Kama ilivyo kwa mama yake na dada yake, Khloe pia amekuwa akitajwa kufanya upasuaji wa kurekebisha shepu yake huku ushahidi wa picha za kabla na baada ya upasuaji, zikithibitisha madai hayo. Mwenyewe amekuwa akieleza kwamba mabadiliko hayo ya shepu yake ni kwa sababu ya kufanya sana mazoezi ya gym.

KIM KARDASHIAN
956242536.jpg

Jina lake halisi anaitwa Kimberly Noel Kardashian, ni mwanamitindo, mtangazaji wa runingani na mjasiriamali ambaye pia ni mke wa rapa Kanye West. Umaarufu mkubwa alionao mwanadada huyu anayefanya poa kwenye kipindi cha runinga cha familia yao cha Keeping Up With The Kardashians, ni umbo matata alilonalo ambalo naye kwa makusudi, amekuwa akilianika mara kwa mara kwa kupiga picha za utupu.


Licha ya mwenyewe kusisitiza kwamba umbo alilonalo ni halisi na hajawahi kufanyiwa upasuaji, vyombo vya habari nchini humo vimekuwa vikimtuhumu kwamba alifanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio kwa kutumia teknolojia iitwayo Fat Injections katika kipindi cha kati ya mwaka 2006 hadi 2010 ambapo ndipo hasa umbo lake lilipoanza kuwa gumzo duniani kote.



  1. JENNA JAMESON
Sexy+Jenna+Jameson+photosalbum+%252853%2529.jpg

Huyu ni mjasiriamali mkubwa nchini Marekani ambaye awali aliwahi kuwa mcheza video za ngono (porn star). Amekuwa akituhumiwa kwamba amewahi kufanya upasuaji wa kukuza matiti yake pamoja na kurekebisha mwonekano wa makalio yake sambamba na hips zake, jambo ambalo mwenyewe amekuwa akilikanusha.
 
Wanawake bana kazi sana kuwaelewa, hawa wabongo wamepewa matako original ila wanataka weupe wa wazungu, wazungu nao wamepewa weupe ila wanataka matako ya kibantu.
 
Back
Top Bottom