bampami
JF-Expert Member
- Nov 5, 2011
- 5,697
- 4,107
Mchekashaji huyu ambaye amepata kibali kwa watanzania hasa wapenda comedy origino amekuwa akijiita AMEOKOKA tena MCHUNGAJI MTARAJIWA. Lakini matendo yake hayaendani kweli na watu hao, jana katika page yake ya facebook amejiweka picha yake akiwa anakunywa ulanzi na akaandika ulanzi.com. Katika comment ambazo fans wake walicomment, baaadhi yao walionekana wakishaangaa na kusitushwa na picha ana maneno yale.Kiuhalisia Massanja hajaokoka (mtazamo wangu) nikutokana na baadhi ya mambo anayoyafanya hayaendani na hao waliookoka, ctukatai kufurahisha jamii kwa njia ya sanaa ya vichekesho lakini anapojiita ni mchungaji mtarajiwa au ameokoka basi sanaa yake itumike kuelimisha jamii katika maadili ya kikristo kweli. Anachafua uhalisia wa dini ya kikriisto.