Masogange akamatwa kwa tuhuma za kuhusika na Dawa za Kulevya

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF,

TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba Video Queen maarufu Tanzania, Agness Gerald almaarufu "Masogange", anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.

IMG_3342.JPG


Masogange alikamatwa na Polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba mpaka sasa bado anashikiliwa central.

Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu nchini, walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na sakata la matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya, katika vita kali inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Masogange zitafuatia...

Ikumbukwe kuwa tuhuma za Mlimbwende huyu kuhusika na mtandao wa baishara za Dawa za Kulevya zilishawahi kujadiliwa katika uzi huu => Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya
Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Kesi kusikilizwa
Tetesi za kuachiwa huru
Hukumu
 
Taarifa zilizotufikia, zinaeleza kwamba video queen maarufu Bongo, anayefahamika kutokana na shepu yake matata, Agness Gerald almaarufu Masogange, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.

Masogange alikamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba, mpaka muda huu bado anashikiliwa central. Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu Bongo, walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na ishu ya matumizi na biashara ya madawa ya kulevya, katika vita kali inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Masogange na kinachoendelea, zitaendelea kukujia kupitia hapahapa, endelea kufuatilia mtandao huu na pia kufuatilia Global TV Online.

Source: Global Publisher
 
Back
Top Bottom