Maslahi ya taifa kwanza, siasa baadaye-Mengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maslahi ya taifa kwanza, siasa baadaye-Mengi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 24, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Maslahi ya taifa kwanza, siasa baadaye-Mengi


  Na Omari Moyo, Arusha

  SERIKALI, vyama vya kisiasa na viongozi wa kidini wametakiwa kushirikiana katika utatuzi wa migogoro inayojitokeza nchini hasa ya kisiasa kuhakikisha amani ya
  nchi haichafuki kama ilivyowahi kutokea kwenye nchi za Rwanda na Burundi.

  Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi wakati akizungumza kwenye mahafali ya 19 ya kidato cha sita cha Shule ya Sekondari Ilboru, mjini Arusha.

  Alisema kwamba malumbano ya kisiasa yanayoendelea nchini na matamko mbalimbali ya viongozi wa dini na wa kisiasa hayana faida kwa mustakabali wa taifa la Watanzania, kwa kuwa matamko hayo yanaashiria machafuko, siyo kuleta amani.

  Bw. Mengi alishauri kuwa ni vyema dini zingekuwa zikitoa matamko yasiyokinzana na yasiyokuwa na muelekeo wa kisiasa na kuwataka viongozi wa kisiasa badala ya kuchafua zaidi hali ya hewa, wakae chini na kukubaliana kuhusu tofauti zao, kwa mustakabali wa Tanzania.

  “Hawa viongozi wa dini, wa siasa na serikali zisifanye maamuzi kwa ajili ya matakwa ya wachache, lazima waelewe wazi kwamba hakuna jambo muhimu kama la kuweka maslahi ya taifa mbele. Wakubaliane kwenye hoja za kuliondoa taifa kwenye machafuko, kwanza wazungumze ya kwao, na wajue kwamba yaliyotokea nchi za Burundi na Rwanda hata Tanzania yanaweza kutokea,â€� alisisitiza Bw. Mengi.

  Aliongeza, “mimi mmenialika hapa Arusha shuleni kwenu, na nimekuja kwa raha kabisa na kifua mbele, je, kungekuwa hakuna amani ningekuja? Kwa hiyo ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha suala la amani ya Watanzani mbele ndipo yafuate mambo mengine,â€� alisema Bw. Mengi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Hakuna masilahi ya taifa kulindwa kama kwa kufanya hivyo kunajumuisha kuulinda dhuluma inayoendeshwa na serikali ya JK dhidi ya watanzania.............................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,924
  Trophy Points: 280
  Mengi awatahadharisha viongozi wa dini
  • Walemavu nao walilia Katiba mpya

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amewataka viongozi wa dini nchini kuacha kuhubiri kwa kutoa maneno ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
  Mengi alisema hayo jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya chakula cha mchana na watu wenye ulemavu.
  "Ninawaomba viongozi wa dini zote nchini kutohubiri kwa kutoa maneno ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwa chanzo cha kuhatarisha amani na utulivu wa nchi," alisema.
  Mwenyekiti huyo alisema pindi kunapotokea uvunjifu wa amani kundi la walemavu huwa la kwanza kuathirika.
  Alisema amani na utulivu uliopo nchini unatakiwa kuwa endelevu ili nchi iendelee kusifiwa ndani na nje.
  Aliongeza kwamba walemavu wanaweza kupata fursa sawa na kundi lingine la jamii endapo suala la amani na utulivu litazidi kushamiri nchini.
  "Kwa niaba ya kundi hili na wengine wote nchini, ninatoa rai ya kuwataka kudumishwa kwa amani na utulivu nchini," alisema Mengi.
  Awali, Mwakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), Lupi Naswanya, alisema wanahitaji Katiba mpya kwa maslahi ya taifa na jamii hiyo kwa ujumla.
  Lupi alisema serikali haina budi kuwashirikisha katika mchakato wa kuandaa Katiba mpya kama moja ya jamii ya Watanzania.
  "Tunahitaji kushirikishwa katika mchakato wa kuandaa Katiba mpya, Katiba iliyopo inahitaji mabadiliko makubwa kutokana na kutotupa fursa sawa katika jamii," alisema.
  Aliongeza kwamba endapo Katiba itakuwa nzuri, jamii yote itaboreka, hivyo bado kunahitajika maboresho katika Katiba ya sasa," alisema.
  Mengi amekuwa na utaratibu wa kila mwaka wa kuandaa tafrija kwa ajili ya jamii ya watu wenye ulemavu na kupata nao chakula cha mchana na kubadilishana nao mawazo.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mengi anatakiwa atambue kwamba in the absence of freedom and justice peace will always elude this country,which doesn't serve any one but the greedy corporates and corrupt politicians!
   
Loading...