Maskini Watanzania

Maskini Watanzania

Felix Ben

New Member
Joined
Aug 9, 2012
Posts
3
Reaction score
1
Maskini Watanzania tunaenda hatua mbili mbele kisha tunarudi tatu nyuma ,ni kwa maslahi ya watu wachache wasiopenda bibi yangu kule kijijini asipate huduma bora ya afya ni hao hao ikifikia wakati wa uchaguzi wanamdanganya bibi yangu kwa kanga ambayo akifua mara mbili rangi yote inatoka masikini sasa wanang'ang'ania kubadilisha rangi nyeusi kuwa nyekundu na masikini hawana cha kufanya zaidi ya kukubali kuwa mwezi una siku 25 hata kama kwenye kalenda zipo siku 31 ndio inabidi akubaliane na hali halisi sasa atafanyaje kama elimu anayopata haijampa uwezo mpana wa kufikiri.

Mimi nadhani wakati huu si wakati wa kudanganyishiwa peremende na watanzania tusitamani nchi yetu iingie kwenye machafuko nina hofu maana yule bibi yangu sidhani kama atakuwa na uwezo hata wa kushika mkuki maana hata macho sasa hayaoni vyema kutokana na moshi wa kuni eeeh si umeme walihaidi toka uchaguzi uliopita ila hadi sasa sioni hata nguzo,

Binafsi natazama jinsi nchi yetu inavyokwenda sasa ni kama hakuna mwenyewe yaani tumekata tamaa , watu wamekosa uzalendo, wenyewe kwa wenyewe upendo umekuwa mbali nasi sijui nini hatma,ila leo nashawishika kusema tasnia ambayo tulidhani itakuwa mkombozi wetu wananchi, sasa naona baada ya maadui wale watatu aliowasema Mwalimu Nyerere.

Naona sasa tasnia ya Habari ameongezeka kuwa adui namba 4 yes adui huyu amekuwa haeleweki mara ajifanye rafiki atusaidie baadhi ya mambo kumbe ni unafiki tu sasa rafiki huyu ametutenga watanzania hatupati tena radha wala ukweli wa habari sasa tunapata habari zenye sura ya mipasho, samahani kwa kutumia neno mipasho, Mfano Felix kaiba Mayai wenyewe wanasema kaiba Kuku, ila kifupi sioni radha ya habari na nashawishika sasa kusema nakosa uzalendo kufuatilia vyombo vya habari vya nchi yangu maana kila siku sioni habari ya matumaini ya kumkomboa bibi yangu kule kijijini .

Ikumbukwe sasa taifa linakabiliwa na mambo muhimu ikiwamo maandalizi ya Katiba mpya ni hatua muhimu katika mustakabali wa nchi yetu ila watu sasa wamesahau kuhusu katiba tunafikiri nani amefanya nini au nani atafanya nini na sijui ili iwe nini kwetu!..,

kesho kutwa timu yetu ya Taifa inacheza na morroco ni mechi muhimu maana huko kwenye soka kunaweza saidia vijana wengi wa kitanzania kupata nafasi za kucheza soka nje ya nchi na kupanua wigo wa ajira kwa vijana wa kitanzania wenye talanta ya soka lakini badala ya kuelekeza nguvu zetu huku tunawaza nani atakakuwa bosi TFF, yapo mengi sana ila hii ya Taifa stars ni mfano tu ila wadau mnaweza mkaongezea kama suala Elimu nk.


"Just know, when you truly want success, you'll never give up on it. No matter how bad the situation may get."

​
 
Back
Top Bottom