Bra-joe
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,846
- 1,443
Nimekaa na kufikiri nikaona kama Jk ameingia ulingoni kupambana ngumi (kuiongoza Tz) ktk ulingo usiokuwa na muamuzi (raia ambao ni walalamikaji tu) na kocha wake (bunge). Halina mbinu mbadala. Jk kaelemewa sana na mpinzani wake (matatizo yaliyopo nchini) uso wake (wananchi) hautamaniki jinsi ulivyovimba na kutapakaa damu, kocha wake wala hana mpango wa kutupia taulo ulingoni na ni round ya 9, maskini Jk, sijui mwisho wake itakuwaje! Hapa namaanisha Raisi wetu nchi imekwishamshinda na hakuna chombo chochote cha serikali kitakacho mnyang'anya Raisi madaraka mpaka atakapo maliza muda wake (huu ni udhaifu wa muundo wa kuiongoza serikali) wala wananchi hatuna ubavu wa kuingia street kumtoa Raisi, wabunge nao wanaona poa tu Raisi hajiwezi (DHAIFU) lakini hawachukui hatua yoyote kuliokoa Taifa. Nafikiri katiba mpya ni lazima kuwe na kipengele kinachosema kama itaonekana Raisi hajiwezi kuiongoza nchi (DHAIFU) basi aondolewe kikatiba kulinusuru Taifa.