Maskini Ismail Aden Rage; sad | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maskini Ismail Aden Rage; sad

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, May 13, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,135
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  rage uwe makini siku nyingine mambo muhimu usikimbilie kweye vyombo va habari
  kama ulivyomuasa mussa mgosi awe makini tunakushauri na wewe ujipende uwe makini aibu isikukute tena mzee mzima hata hivyo tunakupongeza kuileta timu ya BNGM

  Mapokezi ya Asamoah usipime Send to a friend Thursday, 12 May 2011 21:10 0diggsdigg

  [​IMG] Mshambuliaji Kenneth Asamoah akiwa amezungungwa na mashabiki wa Yanga baada kuwasili jana asubuhi kwenye Uwanja Ndege wa Kimataifa ya Dar es Salaam (D.I.A) na kuvishwa jezi ya timu hiyo namba 30 yenye jina la Mwenyekiti wa Simba Aden Rage.Picha na Jackson Odoyo

  Jackson Odoyo
  HAYAWI HAYAWI yamekuwa, hiyo ndiyo ilikuwa kauli ya mashabiki lukuki wa Yanga waliofika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege jijini Dar es Salaam (D.I.A) kwa ajili ya kumpokea mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Kenneth Asamoah.

  Mashabiki hao waliongozwa na Mwenyekiti wa timu hiyo, Lyod Nchunga na Katibu Mkuu wake Mwesigwa Selestine pamoja na msemaji wa timu hiyo Louis Sendeu na viongozi mbalimbali waliokuwa wenye furaha kutokana na ujio wa mchezaji huyo aliyewasili uwanjani hapo saa 3:20 asubuhi.

  Furaha ya Wanajangwani hao iliongozeka baada ya kubaini kumpiga bao la kisigino Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage ambaye alikuwa akitangaza kuwa Simba wanamwania mchezaji huyo.

  Kwa kukejeri madai hayo ya Rage, msemaji wa Yanga, Sendeu aliamua kumvisha Asamoah jezi ya Yanga namba 30 yenye jina la mwenyekiti wa Simba kifuani ikisomeka A. Rage 30.

  Akizungumza na Mwananchi uwanjani hapo Asamoah alisema amekuja kukamilisha taratibu za kujiunga na Yanga.

  Kuhusu hatua ya kudaiwa kujiunga na Simba, Asamoah alisema, “mimi ni mchezaji wa Yanga isipokuwa nilishindwa kuitumikia timu hiyo msimu uliopita kutokana na taratibu ambazo hazikuwekwa vizuri kwa sababu ya muda kuwa mfupi.”

  Alisema hana mpango wowote wa kujiunga na Simba kwa sababu yeye ni mchezaji wa Yanga na kwamba hakuna mazungumzo yoyote yaliyokwisha fanyanyika kati yake na viongozi wa Simba mpaka hivi sasa.

  “Ishu hapa ni Yanga wala sio Simba, mimi viongozi wa Simba siwafahamu kwa sura wala kwa majina sasa iweje useme kuwa ninataka kujiunga na Simba, wewe niulize mambo ya Yanga na sio ya Simba,”alifafanua mchezaji huyo wa zamani wa Jogodina ya Serbia.

  Kuhusu klabu yake ya Jogodina alisema, “maamuzi ya kujiunga na Yanga ni yangu mwenyewe si klabu isipokuwa klabu hizi mbili zinapaswa kuzungumzia suala la mkataba ili ili niweze kuchezea Yanga.”

  Alisema mazungumzo baina ya Yanga na Jogodina yanaendelea vizuri na safari hii ana imani ataweza kucheza soka Tanzania kwa sababu mambo yameanza mapema tofauti na mwaka jana.

  Mghana huyo alisema,“mapokezi haya niliyoyapata hapa yamenipa deni kubwa, nina kazi ya kulipa deni kwa mashabiki wa Yanga na hilo nitalitimiza kwa kuifungia magoli mengi na kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu wa ndani na kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika pia.”
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Jana rage kamtukana ndimbo vibaya sana eti kazi yake ni ukarani yeye hashughuliki ni vi ajira vidogo vidogo
   
 3. freddie063

  freddie063 Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Longolongo kwa kwenda mbele..
   
 4. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,807
  Likes Received: 1,142
  Trophy Points: 280
  Mko busy na kina asamoah gyan, mwenzenu rostam na wenzake wanahamisha midola,mizahabu,mialmas kwenye malori,mpaka muamke....,kazi ipo
   
 5. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Ni Kenneth Asaamoh na si Asaamoh Gyan soma vizuri kaka usikurupuke kama Rage. Kuhusu suala la Rostam kuhamisha almasi na Dhahabu hata wewe ni MTANZANIA unaouchungu wa Rasilimali za nchi yako anzaa kutuonyesha ushahidi ukipata wa kwanza mimi kukusaidia tukakamate Ok! Tupo katika masuala ya Burudani si kila mahali wizi ufisadi
   
 6. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Aden Rage na wenzake Ndolanga, Wambura na Mwamnyange hawafai kuongoza soka na sasa eti wanasiasa, ameshaua tayari Simba
   
 7. x

  xman Senior Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi hawa simba si wanamsemaji wa timu amabaye kazi yake kimsingi ni kutoa taarifa zilizo rasmi kuhusu timu, sasa inakuwaje tena mwenyekiti wa klabu tena ni mbunge anajiaibisha mbele ya vyombo vya habari kwa kuleta habari za uongo, ooh, asamoah hawezi kuja yanga kisa wamefulia, ona aibu mzee, mpira wamajungu haujengi kaka
   
 8. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Kaaazi kwelikweli soka la bongo, Eti cheo cha msemaji wa timu ni kidogo sana kwake. Katibu ndio anayeajiri makarani mh!!!
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Soka letu kama mchezo wa kuigiza!
   
 10. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,959
  Likes Received: 20,296
  Trophy Points: 280
  Najua rage ana maslahi ya kisiasa simba kuliko kuifanya Simba iende mbele, kwa sasa hivi yeye ndo anaongea kila kitu hata masuala ambayo yanaangukia kwa msemaji, hivi ile semina elekezi ya dodoma (serikali ya ccm) haikukufaa rage. Mbona unataka kuiharibu klabu ya simba kwa kuanza kuleta mgawanyiko, acha hizo, na usingekuwa upuuzi wako kwenye ubingwa tungekuwa tunaongea mengine:dance:
   
 11. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,389
  Trophy Points: 280
  who is that dude..?
  tuwekeeni profile ya huyo asamoah na mafanikio yake...
   
 12. R

  Renegade JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2011
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,760
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli Rage amenisikitisha sana, niliona hayo mahojiano kwenye TV Kwakweli sikuelewa kabisa kama ndio hii Tanzania au Macho yangu? Nchi hii imekosa maadili kabisa, Hivi mtu kama Rage ana credibility Gani? Ni kweli tunataka maendeleo ya kila sekta Tanzania?
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mbunge wa CCM huyo Tabora!
   
 14. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Rage si alilamba joka kule Tabora, ana kiburi huyoo saizi! Simba walie tu saizi maana Rage ni mwenyekiti pia ni Mbuge wapi na wapi, anataka uheshimiwa ndani ya soka. Na vijisenti vya bungeni atawahonga honga wazee wa simba watakaa kimyaa. Hapo ni washabiki inabidi waiokoe timu.
   
 15. D

  DURACEF JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  well said babu kijana,watu wanasomba rasilimali na kila kitu watu wanahangaika kumbeba asamoah baadae wanaanza ooh sijui hiki mara kile yule mwizi.wakati mnajitakia wenyewe
   
 16. R

  Rugishar Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: May 5, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  WATU KAMA RAGE NDIO WAMEHARIBU CCM . Sijui Bungeni atafanya nini!!!
   
 17. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,443
  Likes Received: 4,729
  Trophy Points: 280
  Jamani haijaandikwa Aden Rage imendikwa A. Rage.........Mambo ya Rostam yanaweza kujadiliwa kwenye jukwaa la Siasa ila tu hata na mimi ngoja nijiulize humu hivi huyu jamaa anawatumikia wananchi wake saa ngapi? atakuwa mbunge wa Simba huyu.....alitoa siku 100 ikiwezekana ajiulzulu............akaahidi uwanja wa kisasa nadhani umegekuka wa Kisiasa...... Asamoah ....tena kwa kuwaita Yanga Mbumbumbu...najua Mh Rais JK ni Yanga sasa sijui kama aliongea kimuktadha........!!!!??? Ngoja tuyaone ya BGM..na mengine mengi
   
 18. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #18
  May 14, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi mwenyewe aliniudhi sana kwa kumwita afisa habari kuwa ni karani kama kaskta kadogo sana kwenye klabu.Mzee acha dharau ebu piga mzigo ili simba sc. isonge mbele
   
 19. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WAKATI Shirikisho la Soka Afrika CAF likiiweka Simba katika Kundi B, kocha Moses Basena amesema anaamini wachezaji wake ni kama kikosi cha askari jeshi hivyo wapo tayari kuwavaa Wydad Casablanca na kuiondosha katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Katika ratiba iliyotolewa jana na CAF, Simba itakuwa kwenye Kundi B kama ikifanikiwa kuwatoa Wydad Casablanca na itakuwa pamoja na Al Ahly (Misri) EST (Tunisia) na Moloudia Club d'Alger (Algeria).

  Simba inacheza na Wydad Casablanca mwishoni mwa wiki hii baada ya kushinda rufaa yake waliyoiwasilisha katika kamati ya mashindano ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kupinga kitendo cha timu ya TP Mazembe kumchezesha mchezaji Janvier Besala Bokungu wakati timu hizo zilipopambana.

  Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya mashindano ya CAF iliyotolewa juzi, Mazembe imepokwa ushindi kwa madai ya kufanya udanganyifu na kukiuka kifungu VIII, kifungu 24, kifungu 26(sifa za mchezaji) na kifungu 29 ambapo sasa nafasi yake imetwaliwa na Simba ambayo itaivaa Wydad ya Morocco katika pambano litakalofanyika sehemu huru wiki moja ijayo.

  Akizungumza na Mwananchi jana Basena alisema licha ya kwamba uamuzi wa CAF umekuja wakati wachezaji wa Simba wakiwa mapumzikoni haimaanishi kwamba uwezo wa wachezaji umepotea kabisa.

  "Kuwa likizo haimaanishi uwezo wa wachezaji umepotea mpaka asilimia sifuri, wapo wanaocheza Harambee Stars (timu ya taifa ya Kenya),Taifa Stars(Tanzania)na The Cranes(Uganda)watakuwa na msaada mkubwa.

  "Sisi ni kama askari wa jeshi ambao muda wowote unaweza kuitwa vitani ukapigane hivyo sioni cha kuhofia naamini tutapambana na kushinda pia,"alisema Basena.

  Basena ambaye pia amewahi kutwaa ubingwa wa ligi kuu Uganda na timu za KCC, Simba na URA alisema kikosi chake kitaingia kambini leo kujiandaa na mechi hiyo pamoja na michuano ya Kombe la Kagame.

  "Kesho(leo) tunaanza mazoezi, jambo muhimu naomba uongozi uwaite haraka, hii ni fursa ya aina yake tunatakiwa tujipange ili tuweze kupambana na kupata matokeo mazuri,"alisema Basena.

  Alisema anaandaa programu ya muda mfupi ya wachezaji ambapo watakuwa wakifanya mazoezi kutwa mara tatu kwani wana muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda katika mchezo huo.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu alisema,"Simba itawatumia wachezaji wake waliosajiliwa kushiriki mashindano ya klabu bingwa wakiwemo wale waliouzwa TP Mazembe."Alisema,"Wachezaji hao bado ni mali ya Simba ingawa wameshauzwa, lakini uhalali wa mchezaji kuuzwa ni ITC na mpaka hivi sasa TP Mazembe haijaomba ITC ya wachezaji hao, hivyo bado wanahesabika kama wachezaji halali wa Simba katika mashindano haya".

  Mbali na kuwatumia wachezaji hao pia Kaburu alisema, "Wachezaji wa Simba waliokuwa likizo na wengine waliokuwa katika mashindano mbalimbali tayari tumeishawandikia barua na watawasili kesho asubuhi (leo)."

  Makundi
  Kundi A
  Hilal (Sudan)
  Coton Sport Garoua (Cameroon)
  Enyimba (Nigeria)
  Raja (Morocco)

  Kundi B
  Ahly (Misri)
  EST (Tunisia)
  Moloudia Club d'Alger (Algeria)
  Simba (Tanzania) au Widad de Casablanca (Morocco)
   
 20. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Msanii huyo,alilikoroga ndo akafungwa,kaanza tena.
   
Loading...