Masikini wanaharakati na wanasiasa hawa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masikini wanaharakati na wanasiasa hawa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kageuka, Jul 7, 2012.

 1. K

  Kageuka JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu kutokana na mgomo wa madaktari (ni sahihi kusema baadhi ya madaktari kwani si wote waliopata kugoma), nimegundua mambo kadhaa kuhusu wanasiasa na wanaharakati wetu (baadhi). Nimegundua wanaharakati wetu na hasa Hellen Kijo-Bisimba na mwenzake Ananilea Nkya hawana ufahamu wa kutosha kuhusu msingi wa haki za binadamu. Sababu ni hizi.

  1. Msingi wa haki yoyote ya binadamu ni kuishi. Kwa hiyo si sahihi kwa watu kutetea mishahara na posho nzuri pamoja na mazingira ya huduma bora kwa wagonjwa (ili umma uamini unatetewa) lakini wakati huo huo kuna haki ya msingi (haki ya kuishi) inavunjwa na hao hao watetezi. Kwa uelewa wao mdogo, walikuwa wakitetea haki za 'wagonjwa' watarajiwa kwa kushabikia uvunjifu wa haki ya kuishi waliyonayo wagonjwa wakati wote wa mgomo.

  2. Katika matukio mengi yenye mwelekeo wa kisiasa na hasa siasa zinazofanana kuendeshwa na Chadema wamekuwa mashabiki wakubwa. Sikusikia sauti zao za kutosha katika mauaji ya maalbino kama nilivyosikia kwenye mgomo wa madaktari. Wakati wabunge wa CDM wanang'ang'ania mjadala wa madaktari bungeni (ili mkakati wa kisiasa utekelezwe) wao pia walikuwa wakitaka Bunge lijadili mgomo. Je, kipaumbele ilikuwa wagonjwa kusikia mjadala wa wabunge au madaktari wafike wodini kuwahudumia? Hapa, sipati mantiki ya wao kushabikia Bunge lijadili hali hiyo badala ya wao kubaki upande wa wagonjwa ili madaktari warejee wodini kutibu na serikali itimize wajibu wake

  3. Chama cha Waandishi wa habari wanawake kimepoteza mwelekeo kabisa, naungana na wale wanaotaka chama kipya kisajiliwe. TAMWA kilikuwa chama cha masuala ya taaluma na si chama cha kupiga kelele ili kuonyesha mgogoro mkubwa nchini ili hatimaye kuzoa mabilioni ya wafadhili.


  4. wanaharakati wetu wameshindwa kuonyesha busara ya kuwa chemichemi ya mawazo mbadala katika suala la ushawishi kwa pande zinazovutana nchini, badala ya kuwa na mawazo 'neutral' wao walikuwa upande wa kushabikia mgomo kwa mwekeleo wa kuunga mkono siasa za CDM.

  5. Nimegundua CDM kinaendesha siasa za kujijenga kupitia matukio ya kuandaa au kushabikia yaliyokwishaandaliwa na wengine, wakati CCM wamebadili mwekeleo wao kwa sasa wanakusudia kuendesha siasa za kuwaletea maendeleo wananchi. yaani siasa za maendeleo na kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wananchi kwa kadiri inavyowezekana wakati CDM wabajipanfga kkila kukicha kuharibu mipango ya maendeleo.


  wakatabahu!
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu Tz hakuna wanaharakati bali tuna waganga njaa na vibaraka wa nchi za magharibi kuleta mambo yasiyo faa kwenye maadili yetu km ushoga nk
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Siwaelewi mafafanue mnachomaanisha.
   
 4. mnyongeni

  mnyongeni Senior Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Napita tu.........
   
 5. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wanaharakati wamepima na wameamua kuwa upande wa madaktari, ambao pia wanaamini ndio upande wa wananchi. Kwa kiasi kikubwa wanaharakati wanaungana na madaktari kuhusu umuhimu wa kuboresha mazingira ya vituo vyetu vya huduma vya afya, pamoja na mazingira ya kazi ya watoa huduma!
  Wagonjwa kukosa dawa, kulala chini imekuwa kama kawaida...hivi si sahihi, nilazima jitihada za makusudi zifanyike kubadilisha mtazamo/ hali hii...
   
 6. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Maskini ni wewe usiyejua kufikiri, na bila shaka we ni mchumia tumbo, hebu soma historia za wenzetu kama uingereza, ugermany,egypt,libya, na hata kenya hawakuanza hapo walipo........kufa kila mtu lazima atakufa..........na ni bora wanaokufa kwa ajili ya vizazi vijavyo kuliko we mwoga kwa ajili ya tumbo lako,,,,,,,nimekujibu hapo mwanzo tu..........hakuna kitu thread inaonyesha jinsi ulivyo mwoga na mbinafsi
   
Loading...