Mashirika ya haki za Binadamu wamjibu Lukuvi, na kulisihi jeshi la polisi kumwachia

Janja PORI

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
817
225
Wadau pokeani tamko hilo toka mashirika ya haki za binadamu..
Naona wameliomba jeshi la polisi kumwachia mwandishi wa Chanel Ten aliyeshikwa Arusha
======
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Board of Directors: Dr. Helen Kijo Bisimba, Kharous Mpatani, Martina Kabisama, Tike Mwaipabipile, Joseph Parsambei, Saed Kubenea, Hamisa Mmanga and Ernest Kimaya.

Tanzania Human Rights Defenders Coalition [THRD-Coalition]
P. O. Box 105926 Dar es Salaam, TANZANIA Telephone: +255-22-2773038/48, Fax: +255-22-2773037, Mob: +255 783 172394 E-mail: defenderscoalition@rocketmail.com, web Tanzania Human Rights Defenders Coalition

KAULI YA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KWA WAZIRI WILLIAM LUKUVI NA HALI YA USALAMA MKOANI ARUSHA TAREHE 19 JUNI 2013

Mtandao wa Wateteziwa Hakiza Binadamu unaounganisha asasi za kiraia zinazotetea haki za binadamu zaidi ya mia moja, pamoja na mashirika wananchama Mkoani Arusha, tumesikitishwa na kushtushwa sana na kauli iliyotolewana Waziriwa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Uratibuna Bunge) William Lukuvi dhidi ya asasi zakiraia.
Katika kauli yake Bungeni tarehe 17 mwezi Juni, akizungumzia tukio la bomu dhidi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA), Lukuvi ameendeleza kile ambacho kwa muda mrefu serikalii liyopomadarakani imekuwa ikikifanya yaani kutumia lugha mbaya za kuwachonganisha wateteziwa hakizabinadamu na asasiza kiraia kwa ujumla na kuwaita kwamba ni wachochezi, vibaraka wa upinzani na lugha nyingine zenye dhihaka.

"Katika siku za karibuni, zimekuwepo jitihada za makusudi za baadhi ya vyama vya siasa, makundi ya kijamii na watu binafsi kupandikiza chuki kwa raia dhidi ya vijana wetu wa Jeshi la Polisi, kuwafanya raia wawachukie askari, kuwafanya raia wasiwaamini askari, kuwafanya raia wasiwape ushirikiano askari na hatimaye kuwa na taifa ambalo halitawaliki," alisema Lukuvi

Kauli kama hii kutolewa kiongozi mkubwa wa serikali tena katika Bunge la Tanzania ni kejeli kwa waliopoteza ndugu zao Mjini Arusha, na ni kauli ya vitisho dhidi ya asasi zisizo za kiserikali nchini. Nchi yetu imekumbwa na kasumba ya viongozi kuacha kutatua dalili zinazoashiria upotevu wa amani na kutaka kuonyesha kuwa asasi za kiraia na makundi mengine ndio chanzo cha matatizo hayo. Kauli kama za Mh Lukuvi zimeshatolewa ndani ya miezi sita iliyopita na mawaziri na viongozi wengine wasiopungua watano. Waziri Kagasheki alizishutumu wazi wazi asasi za kirahia zinazotetea haki za wafugaji Loliondo kuwa ni wachochezi wa mgogoro huo, wakati huo huo Naibu waziri wa Ardhi aliendeleza shutuma na vitisho hivyo dhidi ya Asasi zinazotetea rasimali ardhi nchini.

Tunamsihi Lukuvi, atambue kuwa imani ya wananchi dhidi ya jeshi la polisi nchini haijawahi kuondolewa na asasi za kiraia, bali huondolewa na matendo ya kidhalimu ya jeshi hilo dhidi ya wanachi na vyama vyao. Jeshi la polisi litaweza kurudisha imani kwa wananchi endapo tu litaacha kutumika na watawala kwa maslahi binafsi na kisiasa na sio kwa kauli za kubeza zitolewayo na viongozi wa serikali dhidi ya asasi za kiraia na makundi mengine. Itakumbukwa kwamba hivi karibuni katika uchaguzi wandani wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. JakayaKikwete, aliwatahadhrisha wana-CCM wasiendelee kulitegemea Jeshi la Polisi kamanguzo yake kisiasa. Viongozi waache mzaha katika hali ya usalama wa Taifa kwa sasa kwani hakuna anaependa amani ya Taifa itoweke. Hadi sasa matukio ya kutishia amani ya Nchi yamekuwa yakishika kasi bila kuona jitihada za makusudi za kukomesha hali hiyo. Toka kushambuliwa kwa wahariri Saed Kubeneana Ndimara Tegambwage, kutekwa na kuteswa kwa Dk. Stephen Ulimboka, kuuwa kwa Mwangosi, Mwenyekitiwa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda, kuuwa kwa mapadre na mashekh, mlipuko wa Olasit dhidi ya waumini wa Kanisa katoliki, migogoro ya kidini na mengineyo, hakuna hata limoja lillilopatiwa ufumbuzi wa kudumu.

USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI

Mtandao pia unalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwanyima uhuru waandishi wa habari, na kuwafukuza waandishi wa habari katika mikusanyiko ya mjini Arusha.Mtandao unalisihi jeshi la Polisi kumwachia mwandishi wa Chanel Ten Ashiraf Bakari, aliyekamatwa tarehe 18/6/2013 katika eneo la Soweto alipokuwa akichukua picha za matukio ya jeshi la polisi dhidi ya raia waliopiga kambi katika viwanja. Tunaalani kitendo cha jeshi la polisi kumkamata bwana Ashirafu aliekuwa na vitendea kazi pamoja na kitambulisho chake cha uandishi wa habari.

WITO WETU

1. Tunamsihi Waziri Lukuvi aifute kauli yake dhidi ya asasi za kirai aambazo kimsingi kwamujibu wa utendaji kazi zao ni Watetezi wa Hakiza Binadamu katika fani mbalimbali na hawahusiki kwa namna yoyote ile katika hali ya sasa ya uvunjufu wa amani unaondelea nchini.
2. Aidha tunaomba asasi kwa upande wao zisijihusishe naitikadi yoyote ya kisiasa baliwaendelee kuwatumikia Watanzania waitikadizote bilaubaguzi wowote.
3. Jeshi la polisi mkoani Arusha limwachie mwandishi wa chanel Ten bwana Ashiraf Bakari, na kuwapa uhuru waandishi kureport habari yoyote.
4. Viongozi wote wakiwemo wa madhebu mabalimbali walaani vikali hali inaoyoendelea Arusha kwa sasa.
5. Balozi mbalimbali na Mashirika mbalimbali kukemea hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea Mjini Arusha.
6. Viongozi watambue kazi za asasi za kirai na kuzieshimu na kuacha kuwaita wachochezi

Tarehe, 19/06/2013

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania! Onesmo Olengurumwa Mratibu Wa Taifa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu
 
Attachments

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,022
2,000

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
6,937
2,000
Hivi hizi asas za kiraia hapa nchini zimeshindwa kwenda kumweleza Obama haya yanayoendelea hapa nchini?
 
kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,020
1,225
Dingswayo Lukuvi darasa la saba kuwa Waziri wa idara kubwa hivyo lazima ajikombe tu na kulamba viatu vya wateule wake, unategemea afanye tofauiti anavyotumwa,ni Tanzania tu makapi kama Lukuvi naye kuwa msemaji wakati ni classless.
 
Last edited by a moderator:

mwene original

JF-Expert Member
May 26, 2013
248
0
Lukuvi wewe ni kiongozi kumbuka ni kiongozi wa selikali watu wanakusikiliza hivi nikuulize mara ngapi tunasikia kwenye vyombo vya habari polisi wamembambkia mtu fuvu la kichwa, mara polisi wamekamatwa na bangi, mara polisi wameua mfanyabiashara na kuiba hela, mara wameua wananchi wasio na hatia, mara utasikia wamepiga mahabusi hadi kukata roho? Usiegemee upande mmoja nao wanamatatizo siku hizi kama unawasifia kwa hili sawa lakini tunakusikiliza na tujaji kuwa makini wewe ni kiongozi wa selikali unaongoza wananchi wote wa ccm na vyama vyote
 
Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
May 16, 2013
1,338
0
Viongozi wetu wa dini wala usiwategemee wameshadhihirisha kuwa ni double dealers. Kampeni yao ya kutetea wakazi wa migodini iliishia wapi? Hao si wenzetu tu, wataitwa Ikulu watapiga gahawa na kuondoka kimya kimya?
 
RUT

Senior Member
Feb 6, 2013
139
195
wapeleke katika mahakama za kimataifa wajikombe hili wapate ngawila zaidi alafu nasikia bisimba cdm b.
 
Top Bottom