Mimi ninayo ekari 16 ya shamba kando kando ya Bwawa lililojengwa na Serikali kwa ajili ya umwagiliaji. Katika majira ya kiangazi kuanzia Mwezi wa Mei mwishoni nataka kuanza kilimo cha vitunguu kwa njia ya umwagiliaji. Katika kilimo hiki nataka kununua mashine ya maji kwa ajili ya kumwagilia ekari kama tano za vitunguu nitakazolima. naomba ushauri wenu wana jamii Forums ni mashine gani ya maji inayotumia dizeli ninayoweza kununua?. Naomba nipate jina la Kampuni, Aina ya mashine, Horsepower yake, Bei yake ikijumuisha vipuri vitakazoandamana na mashine hiyo kama bomba toka bwawani mpaka shambani ambayo ni mita kama mita mia tatu hivi. Ahsanteni nataka niwe mjasiriamali.