Mashindano ya bank abc super 8 cup - live updates

Mashindano ya bank abc super 8 cup - live updates

ndetichia

Platinum Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
27,769
Reaction score
6,589
KUNDI A
A1 Simba SC
A2 Jamhuri FC
A3 Zimamoto FC
A4 Mtende FC

Agosti 5, 2012
Simba SC vs Jamhuri FC (Saa 10:00 jioni, Dar es Salaam)
Zimamoto FC vs Mtende FC (Saa10:00 jioni, Mwanza)
Agosti 9, 2012
Jamhuri FC vs Zimamoto FC (Saa 2:00 usiku, Zanzibar)
Mtende FC vs Simba SC (Saa 10:00 jioni, Arusha)
Agosti 12, 2012
Simba SC vs Zimamoto FC (Saa 10:00 jioni, Mwanza)
Jamhuri FC vs Mtende FC (Saa 10:00 jioni, Dar es Salaam)

KUNDI B
B1 Super Falcon FC
B2 Azam FC
B3 Mtibwa Sugar FC
B4 Polisi Moro FC

Agosti 5, 2012
Super Falcon FC vs Azam FC (Saa 2:00 usiku, Zanzibar)
Mtibwa Sugar FC vs Polisi Moro FC (Saa 10:00 jioni, Arusha)
Agosti 9, 2012
Azam FC vs Mtibwa Sugar FC (Saa 10:00 jioni, Dar es Salaam)
Polisi Moro FC vs Super Falcon FC (Saa 10:00 jioni, Mwanza)
Agosti 12, 2012
Super Falcon FC vs Mtibwa Sigar FC (Saa 2:00 usiku, Zanzibar)
Azam FC vs Polisi Moro FC (Saa10:00 jioni, Arusha)
 
Matokeo ya gemu za Jana kwenye Super 8
Kundi A
Simba 1 - 1 Jamhuri

Kundi B
Azam 2 - 0 Super Falcom
 
Azam chini ya Mhindi sasa,haya all the best...hizo ndo zenu Azam na Simba
 
Mtende 3-2 Zimamoto, ilipigwa jana Mwanza, Mtibwa 2-1 Polisi Moro hii imepigwa leo Moshi.
 
Hayo ndo mashindano hadhi ya simba huko uchelewi kupewa penati3
 
pakiwa na mashindano mengi kama haya hakika timu zitaimarika
 
Haya makombe ya MBUZI haya!!! Je, yana masilahi yoyote kwa timu, wachezaji, vyama vya soka? Maana jamaa zetu wameshaanza zengwe, hadi kieleweke!
 
I had hoped uongozi wa Tenga, ungeturudisha miaka ilee kila mwaka tunaona timu kubwa na maaruf kutoka Ulaya zikija na kukipiga na timu zetu. Nikapata imani zaidi baada ya kuona sasa tuna uwanja mpya wenye hadhi ya kimataifa !! Lakini nimekuja gundua ni yale yale na huyu licha ya kuwa former national player ni fisadi na kakumbatiwa na mafisadi na wanasiasa na hakuna lolote zaidi ya kujinufaisha yeye. Hivi kweli na mahela yote ya FIFA, connections alizonazo anashindwa kuandika proporsals au kushawishi makampuni kama PUMA, Nike, hata Addidas kuleta timu kubwa kwa mechi mbili tatu kila mwaka (hata kama ni team B za ulaya bado ni kubwa tuu). Hata Tyson aka NdooLanga alikuwa anaweza kidogo..!

Hivi vimechi za tutimu uchwara havisaidii chochote zaidi ya kuumiza au kuchosha wachezaji. Yaani huyu kama Bayi tuu, na umaaruf na heshima zote tulizowapa sasa wao ni matumbo yao tuu.. !!
 
Mechi za leo, Azam 0-2 Mtibwa; Simba 2-0 Mtende; Polisi Moro 2-0 Super Falcon.
 
........lazima 'Anselm' kwa haya matokeo ya Simba atakuwa ameyakasilikia tu.

Ha ha ha ha Mkuu PrN niyakasirikie haya matokeo dhidi ya team isiyojulikana katika medani ya soka la Zanzibar? (wewe tangu umeanza kufatilia masuala ya soka umeshawahi kuisikia hiyo team Mtende sijui Mtendeni) nafikiri hii ndo 1 ya zile team zilizopanda sijui kushuka daraja zilizojumuishwa kwenye hiyo michuano,halafu sasa....kama kawaida yenu,goli zote za penalt huku Jamaa wakicheza pungufu,haya kweli yanaweza kuwa matokeo ya kutia moyo?
 
Nilijua tu, hukosagi cha kuongea, kumbuka kwamba Simba ina Hasira; kufungwa au kutoshinda kwenye hizi mechi za Kirafiki, Super 8 na Kagame kwa kipindi hiki kifupi cha Julay-August ni Neema tosha kwa Simba kwani mpaka ligi kuja kuanza itakuwa imeisha jua ni wapi imejikwaa na kufanya malekebisho stahiki; wasiojua falsafa ya Soka watabaki wakitegemea Simba iendelee kuvurunda kumbe inakuja kwa style na speed nyingine.
 
Halafu kingine kinachonipa faraja mimi kama mwanasimba ni kwamba simba kuna wachezaji wengi, waliocheza dak45 za kwanza siku ya nane nane ni wengine na kipindi cha pili waliingia wachezaji wanane kama sub, hicho kimemfanya kocha kuona makosa yako wapi, kikosi cha vijana bado kuna vijana kadhaa wameenda Nigeria lakini waliobaki wanafanya mambo ya kutisha. Na magoli yaliyofungwa si yote ya penati kama anavyopotosha mdau mmoja, goli moja tu ndo la penati na penati haipatikani katikati ya uwanja inaonekana kikosi ni kizuri kama kinafika hadi kwenye sebule ya mpinzani na naye anacheza faulo unategemea nini?
 
Nilijua tu, hukosagi cha kuongea, kumbuka kwamba Simba ina Hasira; kufungwa au kutoshinda kwenye hizi mechi za Kirafiki, Super 8 na Kagame kwa kipindi hiki kifupi cha Julay-August ni Neema tosha kwa Simba kwani mpaka ligi kuja kuanza itakuwa imeisha jua ni wapi imejikwaa na kufanya malekebisho stahiki; wasiojua falsafa ya Soka watabaki wakitegemea Simba iendelee kuvurunda kumbe inakuja kwa style na speed nyingine.

Halafu kingine kinachonipa faraja mimi kama mwanasimba ni kwamba simba kuna wachezaji wengi, waliocheza dak45 za kwanza siku ya nane nane ni wengine na kipindi cha pili waliingia wachezaji wanane kama sub, hicho kimemfanya kocha kuona makosa yako wapi, kikosi cha vijana bado kuna vijana kadhaa wameenda Nigeria lakini waliobaki wanafanya mambo ya kutisha. Na magoli yaliyofungwa si yote ya penati kama anavyopotosha mdau mmoja, goli moja tu ndo la penati na penati haipatikani katikati ya uwanja inaonekana kikosi ni kizuri kama kinafika hadi kwenye sebule ya mpinzani na naye anacheza faulo unategemea nini?.

Doh I can see wana'Simba sasa mnafunguka,MUNGU endelea kujalia katika michuano hii ya ABC hii team iendelee kukutana na team zilizopanda daraja huko Visiwani na Tanzania Bara,huku ukiendelea kuishushia neema za penalt kupitia hawa Waamuzi wetu wa kibongo ili iendelee kushinda, Simba inaposhinda Wana'Simba wanachangamsha sana hili jukwaa letu,ilivyokula 3-1 toka kwa Wakusanywa wa Nairobi Rafiki zangu Masuke na PrN walipotea kabisa humu,wamekuja kurudi baada ya ushindi wa jana.
 
Back
Top Bottom